Sunday, January 6, 2013

SIJUI JINSI YA KUMBEMBELEZA MPENZI WANGU, NISAIDIENI

Habari ya kazi Voiet. Mimi ni kijana wa kiume, i have 18yrs, hadi sasa naishi Zanzibar katika wilaya ya Mjini. Nilikua nikitembelea kwa siku nyingi katika blogi zako zinazohusiana na suala zima la MAPENZI, katika utafiti wangu juu ya suala hilo, nimefaidika na mambo mengi sana yanayohusu MAPENZI, kwa mfano, jinsi ya kumpata mwanamke akupendae, pia vipi utaweza kuishi kuishi nae, na vipi munaweza kuboresha na kudumisha mapenzi yenu na mengineyo. Nashkuru sana nimefaidika kwa kiasi kikubwa sana kupitia BLOG zakoAnt Voilet.
              Ila lakini, pamoja na yote hayo, niliyoyapata kupitia BLOG zako bado mimi nina tatizo moja tu ambalo linanikwaza katika MAPENZI yote kwa ujumla, kwa kutumia TAALUMA ambayo nimeipata kupitia BLOG zako, nahisi nikitu MUHIMU sana katika MAPENZI pia inaweza ikapelekea kuachana na MPENZI wangu na ni kitu ambacho mimi sijakipanga maishani mwangu kumsaliti yeye kwani NAMPENDA.
              Tatizo langu Ant Voilet ni kwamba mimi hadi sasa bado sijajua jinsi gani ya KUMBEMBELEZA MPENZI wangu, kwani yeye kila siku ananmbia NIMBEMBELEZE wakati wa usku asa na mimi sijui kwa sababu mimi nilitaka kuyajua MAPENZI kabla ya kumpata MPENZI,aidha naliyasoma kwanza yakoje halafu ndo nikaingia,bali yeye anambia nimwambie MANENO MAZURI YA MAPENZI YENYE KUMLIWAZA WAKATI WA USIKU ANAPOTAKA KULALA, husema yeye hapati usingizi na mimi pia nimeshachoka kumdanganya, kwaiyo nakuomba Ant Voilet kwa ROHO YA UNYONGE na nainamisha kichwa changu chini na napinda magoti yangu chini na nainua mikono yangu juu kupokea MSAADA wako kwani nakuomba unisadie juu ya hilo kwani NAMPENDA ZAIDI YA ANAVYOFIKRIA na sitaki nimpoteze. Pia nimeshamuahidi Mungu ikiwa hatochukua roho ztu nitakuja kufunga nae NDOA.

                                                          Ni matumaini yangu yakua ombi limefanikiwa
na litajibiwa.
                                                                                        Ant Voilet ndio tumaini langu la pekee.

5 comments:

 1. INASIKITISHA NDUGU YANGU KUUDHIHIRISHIA UMMA KWAMBA SASA UNAVUNJA AMRI YA SITTA HADHARANI. SI UFAKHARI.MUDA MUAFAKA UKIFIKA UTAJUA NAMNA YA KUM'BEMBELEZA MWANDANI WA UKWELI NA SI HUYU '''FAKE''' ULIYENAYE KWANI KESHAKUONA KWAMBA U MWANAFUNZI KATIKA FANNI NDIO MAANA ANAKUPELEKESHA PUTA KWA KUKUTAKA UM'BEMBELEZE.

  ReplyDelete
 2. Kijana mbona bado wewe ni mdogo sana kuhangaika na mambo hayo katika hali hiyo?Vipi shule umemaliza masomo?Naona kama unataka kujipatia vidonda vya tumbo kwa kwa kuparamia mapenzi kihivyo.Jambo la kubembeleza mapenzi halina ujuzi wala elimu yoyote.Ni jinsi tu unavyoweza kujituma mwenyewe.Unapata shida ya jambo hilo kwa sababu wewe bado ni mdogo sana licha ya kuwa na umri wa 18 ambayo wengi hujidanganya kuwa wamkuwa watu wazima.Usikonde kwa mambo kama hayo.

  ReplyDelete
 3. mpe nyama ya ulimi

  ReplyDelete
 4. mimi ni msichana mwenye miaka 32,nimezaliwa kilimanjaro.nina elimu ya chuo kikuu.nimeajiriwa serikalini.umbo langu ni mfupi, mweupe,si mnene wala c mwembamba.natafuta mume mwenye mapezi ya dhat atakayenipenda jinsi nilivyo,mwaminifu,mcha mungu na muumin wa kikristo.mpenda maendeleo na asiyetumia pombe.wasiliana nami kwa ndeku1981@hotmail.com

  ReplyDelete