Saturday, November 3, 2012

MPENZI WANGU ALINIACHA, AKAAMUA KUISHI NA MWANAMKE MWINGINE, SASA ANAOMBA NISAMEHE TURUDIANE, NAOMBENI USHAURI


mambo vai
mm ni msichana mwenye umri wa miaka 28, cjaolewa ila nimebahatika kupata mtoto mmoja ambaye tangu amezaliwa ckuwahi kuishi na baba yake na kumlea inshort, tulishaachana

Baadae nilibahatika kumpata kijana mwingine ambaye tulipendana sana Nilijisikia furaha sana kuwa nae matokeo yake bila mm kujua kumbe alikuwa na mahusiano mengine na mwanamke ambaye alimpa ujauzito na baadae kujifungua ambapo mm nilipokuja kujua na niliumia sana, ckuumia kwa sbb ya yy kupata mtoto niliumia kwa sbb alinificha hakuwa mkweli kwangu.
 
Siku tuliyokutana alinipokea vzuri na kuomba msamaha sana kwa sbb aligundua kuwa amenikatisha tamaa na ckuwa najisikia vzuri, katika mazungumzo yetu nikamuuliza swali moja tu una mpango gani ss na huyo dada, akanijib hawezi ishi nae ktk maisha yake,jibu lake lilinipa amani tukarudiana,.

kadri siku zilivyozid kwenda nikaona anaanza kubadilika nikimpigia hapokei, msg hajib kumbe yule dada alishahamia kwake nilipojarib kumuuliza akasema ndio kwani ni dhambi yy kukaa na mwanae ? niliumia sana nikasema ngoja niachane nae na siitaji kuwasiliana nae awe free na familia yake

 juzi nimebadili cm ambayo naitumia nikaona ananzaa kunisumbua na kuomba msamaha kuwa anataka kuendelea na mm, na c mara moja kwa kuhesabu ni zaidi hata ya mara ishirini anaomba msamaha, nimekuwa cimuelewi kwa sbb kama anaishi na mtu iweje aendelee kuomba msamaha na anasubutu kusema hawezi kbs kuishi bila mm kwa yale niliyomfanyia na nilivyokuwa namjali na kumyenyekea, ameona mm ni mwanamke ambaye alikuwa naniitaji ktk maisha yake, naomba ushauri hv huyu kijana anamaanisha au ni msanii tu, ingawa bado nampenda ila nimekuwa muoga sana


8 comments:

 1. Pole rafiki yangu kwa hilo lililokupata, coz najua kabisa maumivu ya mapenzi yalivyo, hasa kwa yule uliempenda sana, halafu yeye asithamini pendo lako, inauma sanaa, yani sana tu, lakini kitu ninachoweza kukushauri mimi binafs nikwamba, huyo kijana, hana msimamo na maisha, hajajipanga, ana tamaa, kiufupi, HAKUFAI, atakuja kukuumiza zaidi ya hapo, achana nae, tulia, omba Mungu, akupe mume mwema kwako, huyu kijana ni chenga, yani anaonekana ana mambo mengi sana kichwani kwake, kweli shost, huyu atakusumbua na kukutesa sana,, hata kama unampenda vipi, wewe jikaze, utaumia kwa muda tu na utakuja kuzowea, utamuona wa kawaida,, ameshakuwa muongo kwako, alikuficha baadhi ya mambo, ssa hivi anahitaji nini tena toka kwako?? my dear, achana nae, mwambie asikusumbue kabisaaaa akuache kiroho safi.

  ReplyDelete
 2. Pole sana mamy,hyo mwanamme hakufai kabsaaaa,hv mtu anayeishi na mwanamke tayar dn anakuja na maneno yke unamwamini,achana nae kikubwa Muombe Mungu atakupa mume mwema na bora dia
  Neema

  ReplyDelete
 3. na mimi na ungana na violet kwa mchango wake inshort huyo kijana hakufai kabisa ukimrudia atakusumbua sana hana msimamo hajui anataka ninimwombe Mungu akupe mume wa kweli atakae kupenda kwani mume wa kweli anatoka kwa Mungu usikate tamaa yuko alieandaliwa kwa ajili yako gudluck

  ReplyDelete
 4. Dada usijaribu kurudia makapi.Nitakushangaa kama bado unaweza kupoteza muda kufikiri juu ya kurudiana na huyo kijana.Kwanza maneno anayokuambia ni kama anamwambia mtoto mdogo asiye na akili.Wewe ni mtu mzima sidhani kama unaweza kuamini maneno kama hayo na mwenyewe umeshuhudia vituko vyake.Labda kama wewe hujiamini na unaona huwezi kupata mwanaume mwingine.Mwenye macho na masikio haambiwi tazama wala ona maana umetazama na kuyaona mwenyewe wazi.

  ReplyDelete
 5. Huyo Mwanaume anajua unampenda anatumia mwanya kukurubuni, anajua akiomba msamaha utamsamehe aendelee kukutumia, muepuke kwa nguvu zote maana hana mapenzi

  ReplyDelete
 6. HUYO HAMFAI MAANA HANA MSIMAMO. NAMSHAURI HUYO DADA AENDELEE NA MAISHA MUNGU ATAMSAIDIA NA ATAPATA MUME

  ReplyDelete
 7. Mie naungana na wengine wote waliokushauri kabla yangu,huyo mwanaume hakufai na anatumia mwanya wa ww kumpenda kwa nia ya kukubabaisha.achana nae hakufai hata kwa dawa.

  ReplyDelete
 8. Maisha ya kuishi wawili yana misuguano...hivyo usibabaike kwa kukuomba msamaha...ukikubali, jua fika si mapenzi, anataka kukutumia kupunguza stress za nyumbani. Move on unawekewa giza bila kujijua.

  ReplyDelete