Monday, September 3, 2012

NINA MWANAUME AMBAE ALISHAOA, LAKINI WAMETENGANA NA MKE WAKE,, JE NISAHIHI MIMI KUOLEWA NAE??

kwanza hongera kwa kazi nzuri unayoifanya dada yangu Mungu akubariki.nahitaji kushauriwa, mimi ni binti nina miaka 27,sijaolewa bado.nimewah kudate 2 men bt hatukufika mbali kwa sababu mbalix2,sasa nimetokea kupendana na kaka mmoja  ye alishawah kuoa bt wako separated na mkewe kwa muda mrefu sasa,when i met him tayar alishatengana na mkewe so sijahusika kabisa kumuumiza mwanamke mwenzangu bt hawajavunja ndoa rasmi sabab ya process za divorse zinavyokuwaga.uwa ananiambia ndoa yake ilikuwa chungu isiyo na furaha so he cant go back to his wife na anataka kuwa nami maisha yake yaliyobaki,yuko kwenye 30'syrs,he loves me and i love him  so much.ombi langu kwa ushauri, je niko halali kuendelea nae nikisubiri avunje ndoa yake au nitakuwa bado na hatia kwa mkewe thou hawakai wote?am confused.
usitoe email yangu dada yangu.
asante sana.thou sijawah kukuona live bt napenda jinsi ulivyo dada vaileth.God be with u.


18 comments:

 1. Sikushauri kuoelewa nae bila kuchunguza kwanza kilichomtoa mwenzio ndani ya ndoa ni nini? mdogo wangu wanaume wanajua sana kuficha makucha. so fanya uchgunguzi wa kina kwanza.. hilp moja, la pili huyu mwanaume alishazaa na mkewe watoto wangapi?? una uwezo wa kulea watoto wa nje?? to be honest, sikushauri kuolewa na mume ambae alishaoa teyari

  ReplyDelete
 2. tafuta mume wako dada, umri wako ni mdogo bado kwenda kuparamia waume za watu, hata kama waliachana wewe unaijua sababu????

  ReplyDelete
 3. Tafakari kwanza mama, msome na mchunguze vilivyo huyo mtu wako.Usikimbilie mzoga eti kwa sababu umetupwa hapo hauna mlaji,je unajua walioua labda waliweka sumu ndani yake?je unajua chanzo cha matengano yao?Mbona kitu talaka wala hakichukui muda mrefu kama kweli wameamua kuachana si wangeachana.?Una hamu ya kuwa nammtu haraka,lakini hujui unataka nini hasa kwa mtu unayemtaka haraka kihivyo.Bila shaka utakuwa na wewe una dosari ndio maana mahusiano yako ya awali na wanaume wawili yalikushinda.Jiangalie vizuri na ujichunguze, utabeba jiwe badala ya mwana.

  ReplyDelete
 4. achana na mtu aliekuwa kwenye mahusiano teyari, tafuta atakae kuwa wa kwako peke yako

  ReplyDelete
 5. To me umehusika kwa asilimia fulani kuivunja hiyo ndoa,reasons,1)hawajadivorce bado,2)kungekuwa na uwezekano wao kureconcile ila wewe umeingilia kati,kumbuka aliyekiunganisha Mungu binadamu asikitenganisha.dada mara nyingi ndoa kuwa chungu ni shetani tu anaingilia,kama wakizinduka wakamrudia Mungu wewe utachomeka na maumivu,halafu hata iweje huyo kaka alimpenda sana sana mkewe ndio maana akamuoa,sasa je unahakika gani kama atamrudia??ushauri wangu,TUBU KWA MUNGU,ACHANA NAYE HARAKA SANA,TULIA UTAPATA MUME WAKO

  ReplyDelete
 6. We endelea kula asali na uchonge mzinga kabisaa na huyo divorceee tapeli,utakuja juta sana,kwanza Mungu anakuona na wewe utakuja kuachwa kama huyo,kwanza jiulize wewe unatofauti gani kuliko mkewe wa ndoa,halafu ndio uvuruge ndoa yake,mume wa mtu sumu dada.

  ReplyDelete
 7. Nakushauri muache haraka sana huyo bado ni mume wa mtu na wewe ni kipoozeo tu! Anampenda sana mkewe ndio maana hajampa talaka mpaka leo! Hapo dada unatumika tu uambukizwe na magonjwa bure ilhali umri wako bado mdogo! Na kama wana ndoa ya kanisani umeula wa chuya dada, uchungu wa ndoa si kigezo cha talaka!
  Kuolewa na kijana mwenzio kuna raha yake bwana! Chukua tahadhari jiulize maswali yafuatayo: Huyo bwanako ujana ale na mkewe msuli aje avae na wewe? unajua mapungufu yake? kisa cha kutengana na mkewe unakijua? ndoa ilikua chungu nani alichangia huo uchungu? Je wewe utapenda wanao walelewe na mama wa kambo? (mind you hata ukiroga amuache mkewe na wewe ujue talaka yako inakuja maana hata wewe pia ukishaingia ndani utageuka mchungu)?
  Hebu muache huyo bwana arudi kwa mkewe tena wewe ndio shetwani mkubwa unavuruga kichwa ya yule bwana hata asiwaze kurudi kwa mkewe, tena unachangia kwa asilimia 110! Nimekuchukia na nina hasira na wewe hata kama sikujui! Nadhani tatizo lako unaona mileage imesoma sana unaogopa kudoda kwenda kuparamia mume wa watu hata haya huna?
  Kugombana kupo, walipendana ndio maana wakafikia hatua ya kuona, hebu pisha na ukahaba wako katafute bwana wa kwako!
  Alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.

  ReplyDelete
 8. Kabla sijakuhukumu nikuulize maswali yafuatayo:
  1. huyo bwana na mkewe wametengana kwa muda gani?
  2. je hii ndoa ni ya kanisani?
  3. kuna watoto? (umri wao?)
  4. umekutana nae kwa sababu mnakaa/ mnafanya kazi mazingira mamoja? sababu na kuuliza hili ni kwamba upweke/ boredom ndio inaweza ikawa imemleta kwako na kwakua wewe umejirahisisha ukawa easy pick kumliwaza
  5. je ana mawasiliano na mkewe au kumsaidia kwa lolote? (anakushirikisha kwa hili?)
  6. anamzungumziaje mkewe (mind you, huyu ndie alikua mpenzi wa ujana wake)?
  7. wewe je ungependa kuwa kwenye situation aliyokuwepo mwanamke mwenzio kwa sasa?
  Ukinijibu haya nitakupa ushauri.

  ReplyDelete
 9. jamani wewe muuliza swali,!!ngoja nikwambie ukweli,sasa hivi unaona utamu ,raha,on top of the world,blah blah blah,ila dada bora umejiwahi mapema,maana inawezekana umeonyeshwa kiana yake kwa kutuuliza tukusaidie,utakuja balaaa,na majuto makubwa,yaani niandikapo sasa hivi ,ukisoma hii message,mwambie tunachofanya sio sahii,kwahiyo ,akapatane na mkewe na waishi kama mwanzo,na wewe omba toba ,utakuja kuniambia,umepata wa kwako.

  ReplyDelete
  Replies
  1. tayari nimempa ujumbe wako,kuwa wapeane second chance,imekua tabu kidogo ye kuupokea ujumbe huu bt kwa msaada wa Mungu najua yote yanawezekana.

   Delete
 10. NIMESOMA SABABU ZA HUYO MWANAUME,YAANI NIMTAPELI SANA KWAKWELI,MBONA SABABU ZENYEWE SIO ZA KUDIVORCE BASI ATAKUWA ANAACHA MKE KILA SIKU...KWA SABABU KIDOGO

  ReplyDelete
 11. mbona huyu mwanaume mbona anatoa siri za ndani,kwakweli jamani ana utoto kiasi fulani,solution mwaache akasawazishe na mke wake na mtoto,acha malaana,ugomvi ni kawaida mbona mambo madogo sana hayo.

  ReplyDelete
  Replies
  1. sio kutoa siri za ndani,mtu yeyote ata kama ni wewe ukiwa na tatizo au jambo linalokuumiza lazima utafute mtu umweleze upate relief,ndio maana watu wanatafuta ushauri labda wewe hayajakukuta ya kukufanya umwambie mtu

   Delete
  2. mhh sipati picha kwamba ni sahii kutoa siri kwa HAWARA,HUO NI UJINGA KWAKWELI.

   Delete
 12. Ndoa chungu??na huo mwaka mmoja walioishi kwa furaha umefutika,du embu dada muuliza swali funguka kidogo ,huyo anataka akutumie tu hana jipya,achana naye.

  ReplyDelete
 13. Wee Vai, hayo maelezo aliokupa ni ya kitoto kabisa.Pia amekupa maelezo ambayo hayajatoka kinywani mwake mwenye.Huo wote ni udanganyifu sijaona chochote cha kuchotwa akili mwanamke mzima uridhike na hizo porojo.Labda kwa sababu huyo mdada anataka mwanaume ameamua kuziba masikio na macho ili achonge mzinga wa nyuki.Kama anampenda tu huyo bwana wake aendelee lakini uwazi uko hapo hamna hata haja ya kuumiza kichwa.Wanawake mtazidi kudanganywa kirahisi hivyo hadi lini jamani?mtu anakupa stori ambazo wala hazina chachu nyoyote yaani unagundua tu kwamba mtu anakughiribu.

  ReplyDelete
 14. Jamani..jamani,.. we mtoto umefanya vizuri kuomba ushauri. Mala nyingi wenye ndoa huwa hawaachani huwa wanapumzika tuuu. Kama huamini jaribu kuingilia mdogo wangu, atakuja kukutusi huyooo mpaka utajiona choo. Mala nyingi mapenzi mwanzo huwa matamu na kumbuka huyo mkewe alimpenda zaidi ya hata wewe unavyozani anakupenda ndo maana akaamua kumuoa. Kuhusu kutengana huenda amemchoka au huyo kaka ni malaya mkewe akaamua kuondoka ila vya nje huwa vinachosha na naamini atamrudia mkewe, pia hujue nawe pia atakukinai/kukuchoka atatafuta mwingine ndo mambo yalivyo shost. Omba mungu akupe mpenzi wako, mtakae vumiliana kwa shida na raha. huyo kaka sio mvumilivu ndo maana anahaha haha c mume mwema, angekuwa mwema angeshamrudia mkewe. Angalia usiendelee kuwa kipozeo.

  ReplyDelete
 15. Ndugu yangu mi yalinikuta hayo,niliolewa na mwanaume ambaye aliachana na mkewe na walikuwa na mtoto mmoja ila alikuwa ananiambia kwamba mkewe ndo mwenyematatizo,hakuna mwanaume atakuja kukwambia kwamba relationship yake ya kbla ww yeyendo aliemkwaza mwenzake wooote watakuambia kwamba mwanamke ndo alikosa chunguza sasa mama ,mi nilikuja kuachana naye baada ya mwaka mmoja na tulishafunga ndoa kabisa ila wanaume hawaaminiki chunguza vzuri tu.

  ReplyDelete