Wednesday, August 29, 2012

NIMEMPATA NINAE MPENDA SANA- TATIZO DINI ZETU ZINATOFAUTIANA, NA NDUGU HAWATAKI HILO,, NIFANYAJE???
Hello miss violet
Nimekua nikifuatilia sana matukio yenu na jinsi watu wanavyotoa uashauri nimeguswaa maana na me nina langu lanitatiza na sijui nifanyaje yaaani sina jinsi ya kufikiria tena.
Nilikua na bwana ambae alikua ananipenda sana ila mimi sikuampenda kiiivyo nkaamua kuachana nae maana ntamuumiza tu maana sikua muaminifu kwake na nkawa najisikia vibaya, kwa ilo nkaamua kumuacha aendelee na maisha yake.


 


Nilipoachana nae nkapata mkaka mwingine ambae kanionesha maisha ambayo sijawai kua nayo ninampenda sana uyu kaka na yeye ananipenda saaana ila ni anawivu na hasira mbayaa ila sababu namuelewa namchukulia kama alivyo najua jinsi ya kumuhandle kama anahasira ilaaa tatizo kubwa ni lililopo ni DINI,
Yeye ni muislam na mimi ni mkristo, ndugu zangu  washaanza kunijia juu kua hawataki niolewe na muislam, kifupi hawataki mausiano yangu nae na me nampenda sana jamani nina furaha  kuwa nae, tuna amani na niko huru saaana kwake!  Mbaya zaidi mama yangu anasema anatambua ndoa moja tu ya kikristo nyingine hazitambui  nisaidieni jamani nifanyaje?? Na hatuko tayari kuachana!!!


6 comments:

 1. Pole sana, nakushauri kwakuwa nimeguswa na hili, kama kweli mnapendana stick kwenye upendo wenu ndugu na wazazi watakuja kuwaelewa tu, jaribuni kuwaelewesha ili mfunge ndoa muitakayo, kwako wewe kama mkristo sifahamu dhehebu gani, kama ni mkatoliki mnaruhusiwa kufunga ndoa ya mseto na hivyo ukimuelewesha mpenzi wako anaweza kuelewa mkafunga kwani yeye hatobadili dini ila mtafunga kanisani na kwa mantiki hiyo mama yako na ndugu zako wataridhia, ama laa bwana anataka ubadili dini sikushauri kubadilisha dini sababu ya mwanaume, ni bora uifahamu dini kwa ndani na kama ukiona dini muafaka ni hii basi go for it, kwani ukibadili dini kwa kufuata mtu sidhani kama hata Mungu anapenda! Mimi ni mfano hai wa hili suala lililokutokea wewe, mimi ni Muislam mume wangu Mkristo! Yaliyotokea kati yetu naweza kuandika mpaka kitabu au kama ni movie basi babkubwa! Ila kwa ufupi tulistick kwenye msimamo wa kupendana tulifunga ndoa ya mseto kanisani, tuna watoto wawili na tunaishi kwa furaha na amani na tunamtegemea Mungu huyohuyo mmoja atusaidie katika maisha yetu! Ukitaka maelezo zaidi nipo tayari kusaidia!

  ReplyDelete
 2. FATA MSIMAMO WAKO TU! ILA KWA USHAURI WANGU USIBADILI DINI, FUNGENI KILA MTU NA DINI YAKE,,, UKIABADILI DINI SIKU YA SIKU UTAKUJA KUPATA TATIZO UTAKIMBILIA WAPI NA NDUGU ZAKO WAKIKUTENGA?

  ReplyDelete
 3. Kwa ushauri wa haraka tu bibie ni kwamba ndoa utaoa ndugu bali ni wewe na umpendae kwa kuwa kusema wanataka awe mkristu au muislamu au vyovyote vile si juu yao bali ni wewe na yule umpendae kama mmekubaliana basi Mwenyezi Muumba atawabariki.

  ReplyDelete
 4. Pole sana, huo ni mtihani...ila fungeni ndoa kila huyo na dini yake, siku hizi kuna ndoa za mseto jamani...hao ndugu wanakubana kama vile wao ndo wanakuoa, duh...pole sana...pia Sali sana Mungu akuongoze maana yeye ndo atakunusuru na mtihani huo

  ReplyDelete
 5. Wewe mwenyewe unasema ni mkali, ana wivu, na ana hasira sana.Kwa nyongeza zaidi ni dini tofauti na yako.Kwa mantiki ya maelezo hayo mimi naona tayari huyo hakufai kuolewa naye.Nyongeza nyingine ni ndugu zako wasiokuwa tayari uiongie katika ndoa hiyo. Kiujumla hata kama watu wanasema mwamuzi ni wewe na kwamba ndoa ni yako wewe na huyo unayeolewa naye, nisingekushauri uzingatie sana maelezo hayo kutokana na kasoro lukuki zilizoanishwa hapo juu kutoka kwako mwenyewe. Ndoa inahusika sana na familia unayotoka kila mtu.Unaolewa si kwa kuwa unataka kuishi maisha yako na mumewe,ila kwa sababu unatoka kwenye familia na familia hiyo inakutakia heri wewe uwe kwenye familia inayokyfaa na inayowafaa wao.Kumbuka uko hivyo na unapendwa hivyo kwa sababu ya kulelewa na familia yako.Hujatokea msituni ukaibukia hapo ulipo.Ndio maana siku ya siku mambo yakitibuka utakimbilia kueleza mama yako au baba yako au ndugu yako.Sasa kama utatibuana na familia yako mambo yakikulemea utaenda kusema na kupata faraja kwa nani?Kasoro ulizoeleza zinatosha kabisa kukaa chini uhesabu moja,mbili tatu nne, siolewi naye.

  ReplyDelete
 6. Zingatia sana maelezo ya mdau hapo juu.Umekuwa mtu kwa sababu kuna watu (familia) na kuna watu kwa sababu kuna mtu(familia yako).Ndio maana watu wana usemi kwamba "usiyefunzwa na mama yako utafunzwa na ulimwengu. Familia yako ndio msingi na nguzo ya maisha yako hata kama utaolewa na kupata mume malkia.Mtoto hakui kwa mzazi.mwanafunzi hamshindi mwalimu wake hata akimzidi digrii nyingi.Kasoro hzo ambazo wewe umezikiri wazi zaweza kuwa mwiba huko baadaye,ingawa unaweza kuchukuliana nazo kama ulivyosema kwa sababu unasema hivyo uko nje yake,ngoja uingie uwe ndani. Pia Utofauti wa dini zenu hilo ndo balaa na ndilo familia yako haitaki kusikia chochote.Bibie, ndoa ni pamoja na dini.Msingi mkubwa sana wa kuhimili ndoa yako ni dini.Mtu asikudanganye kuwa uamuzi ni wako, ni sawa,lakini siyo kweli kwamba wazazi wako hawana sehemu ya kukusaidia maamuzi sahihi.Familia yako inataka mafanikio ya ndoa yako,na ndio maana wanahusika.Ukipuuza utalia baadaye na hutakuwa na msaada.faraja ya kwanza unapata kutoka kwa wazaqzi mambo yanapokukuta mabaya.Kaa chini wasikilize wazazi wanachoongea, zungumza nao weka nao ushirikiano katika jambo hilo ili kama una cha kuwaeleimisha juu ya huyo mwanaume iwe rahisi usije ukaweka hasira.Bahati mbaya tena umemkimbia aliyekupenda japo wewe hukumpenda.Mruka matope hukanyaga mavi!!

  ReplyDelete