Monday, November 21, 2011

MUME WANGU AMEZAA NJE YA NDOA, AMEOMBA MSAMAHA NISIONDOKE NIENDELEE KUWA NAE, NIFANYAJE


Habari dada Violet, naomba unipe ushauri, mimi ni mama wa mtoto mmoja mwenye miaka 5 sasa hivi, nilibadilisha dini toka kwenye ukristo na niliolewa kwa ndoa ya kiislamu, ndani ya maisha ya ndoa, kuna mikwaruzano mikubwa sana baina yangu mimi na mume wangu ikiwemo kupigwa sana,  kudharirishwa mbele za watu, maana wakat mwingine huwa ananipiga mbele za watu, yani mikwaruzano tu!  Na nikitaka kuondoka huniomba msamaha, kwakuwa naona nitashindwa kulea mtoto peke yangu
Juzi kati hapa nimepata taarifa kuwa amezaa nje, nilipomuuliza alikataaa, lakini baada ya kutishia nakwenda kufanya fujo kwa Yule mwanamke ndio akakiri kuwa ni kweli,  nimeamua kuondoka, lakini yeye anasema nimsamehe ilikuwa bahat mbaya, nishaurini nifanyaje jamani, mbona sijielewi mwenzenu , sasa hivi hayupo amesafiri, ila nataka akirudi akute nimeshafikia maamuzi, 




 

2 comments:

  1. Hukujua kuwa waislamu wanaruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja??

    Kaa naye huyo ndo mumeo uliyembadilishia hata dini ili uolewe naye.Kuzaa nje si tatizo, labda tatizo ulilosema unapigwa sana naye.Uliyataka mwenyewe kuolewa katika dini inayoruhusu wake zaidi ya mmoja hivyo vumilia bibie.

    ReplyDelete
  2. duh! pole sana, kama hadi ulikubali kubadili dini inamaana ulimpenda. Na uvumilie maana inaonekana hata ukipigwa upo tu, so kuzaa nje kwa mwislamu ni kawaida na hata kuoa wake wanne. Tegemea harusi ya huyo aliezaa nae nae ajue baada ya muda ataletewa mwingine maana hilo ni kawaida kabisa kwa wenzetu hawa. Ila kama unaweza ingia kanisani mlilie mungu kwa kwel na haki hakika huwa hachelewi kujibu.
    Ubarikiwe dada yangu.

    ReplyDelete