Thursday, November 17, 2011

ELIMU HAINA MWISHO - MAMA YANGU AMEGRADUATE

Hakika hakuna kama mama Duniani, mama ni kila kitu kwa mtoto, maisha bora, yenye heshima, furaha, na msimamo yanajengwa na mama zaidi,  na hata mtoto anapokuwa na tabia mbaya,  wa kwanza kulaumiwa ni mama.


Namshukuru Mungu sana sana, kwa kunipa mama Mzuri, mama mwenye hekima, mama alienilea katika maadili ya kumuheshimu na kumuogopa Mungu, mama alinifundisha mengi wakati natoka nyumbani kwenda kuanza familia yangu mwenyewe kwa mume wangu, mama ambaye ni zaidi ya rafiki na mshauri wa kweli katika maisha yangu hadi leo

Huyu ni dada yangu pekee aliyebakia, baada ya yeye kuachia ziwa, ndio nikaingia kunyonya mwenyewe,  anaitwa Joyce.


And this is my lovely Dad, Rev. Gerald Mhinga, wote kwa pamoja wametupa malezi mazuri, nawaombea maisha mema na marefu, ili hata watoto wetu waje kuwatunza watakapokuwa wazee

Amepata Bachelor ya Bible Theology mjini Dododoma, it was fun kwakweli tunamshukuru Mungu sana kwa hilo,wamesoma wanafunzi 17 lakini mwanamke alikuwa peke yake, (nimejifunza kitu kwa hilo)

Walikwenda kutembelea bungeni, wanafunzi, nae akaona sio mbaya akipata picha moja ya kumbukumbu, maana sie wengine pamoja nakukulia Dom, lakini bunge tunaliona kwa nje tu! Ndani tukatafute nini ah!
Kiufupi, mama ni kila kitu kwangu3 comments:

 1. mmependeza jamani, mama yenu ni mzuri kuliko hata nyie wenyewe, she is still young kabisa as if ni mdogo wako, nimependa kweli, hongera zake

  Suzy

  ReplyDelete
 2. Mama yenu ujana wake umerejezwa kama tai kumbe Violet mtoto wa mchungaji ubarikiwe sana

  ReplyDelete
 3. umefanana na mama yako, hongera kwa kuwa na wazazi vijana na wazuri hivyo, mie sina baba wala mama, walishatangulia mbele za haki, sijui hata nitadeka kwa nani, nikiona hivi naumia sana moyo wangu

  ReplyDelete