Friday, July 29, 2011

VINYWELEO VIMEJAA MIGUUNI – NIVITOE NA NINI? VINAHARIBU MIGUU YANGU


Wapenzi, mnisamehe kwa kuwatupa kwa muda mrefu kidogo, jamani niko busy kupita kiasi, nimebanwa sana kazini, chuoni , na kuna issue nyingine nafanya inanikeep busy sana, ikikamilika hiyo issue ya tatu nitawajulisha wadau wangu, but tupo pamoja sana, 

Kuna mtu ameniomba ushauri jinsi ya kuondoa vinyweleo katika miguu yake, sasa je kwa wale ambao mnafahamu  njia za kutoa hivyo vinyweleo ni nini? 
atumie wembe, uzi, veet , au hairuhusiwi kuvitoa au kuna njia zingine tena za kutumia??


Jamani vinyweleo vinakera, vinaharibu uzuri wa miguu yetu kabisa yani, unakuta mguu mweupe halafu vinyweleo vimejazanaaaaaa vyeusi,  wala hainogi,  naamini kwa kumsaidia alieuliza, na wengine watapata msaada pia6 comments:

 1. ni kweli jamani, hata mie hii mada inanihusu, nasubiri hizo tips ili nipate kujua.

  ReplyDelete
 2. Tumieni VEET Wapendwa wangu, veet ni nzuri sana na inaleta usoft kabisa,kwanza kabisa chukuwa veet halafu paka miguuni kwenye vinyweleo, kisha acha kwa dakika kumi, kisha unachukuwa kitambaa laini au kitauro kidogodogo, unachovya kwenye maji ya vuguvugu, ila sio vuguvugu sana yanatakiwa yawe na umoto kiasi, halafu unajivuta taratibu kwenye miguu yako kutoka chini ya
  goti hadi miguuni, utaona vinatoka taratibu,
  ukimaliza osha miguu vizuri, kisha paka lotion, ni nzuri sana

  ReplyDelete
 3. asante dear, sasa wengine wageni kwa mambo hayo, veet inapatikana wapi au duka lolote la urembo tutaikuta??? pia ukitoa huwa haviji kwa wingi maana wengine huwa wanatwambia kuwa ukitoa ndo vinaota vingi kuliko mwanzo, msaada plz

  ReplyDelete
 4. veet inapatikana hata maduka ya dawa, tena zipo kubwa na ndogo, ukitoa miguu inakuwa nyororo sana, jaribu kutumia uone, mimi huwa natumia hiyo, sijapata madhara yeyote, sijui labda huko badae, lakini kwa sasa, mmmmm, niko kama mtoto, miguu nyororo, inapatikana sna kwenye maduka ya madawa na na cosmetics,

  ReplyDelete
 5. Kamuone Diana pale DI's Health & Beauty Parlour, tel. no. +255 754 563753 atamaliza tatizo lako na miguu yako itameremeta!

  ReplyDelete
 6. WAX WAX WAX ACHANA NA VEET, CALL NAMBA YA HUYO DIANA, AU NENDA SALUN ZA WAHINDI

  ReplyDelete