Saturday, July 16, 2011

NINA MIAKA 48 NATAKA NIISHI NA MTU MZIMA MWENZANGU, JE NITAWEZA KUSHIKA MIMBA??


Dada Beauty touch in Dar, napenda nikupongeze kwa blog yako nzuri sana, mungu akubariki maana inatusaidia sana,

Mimi ni mama mtu mzima tu! Nina watoto wakubwa, ila sikubahatika kupata elimu ya darasani, sasa hivi nina miaka 48 na nimeacha kuona siku zangu, huu ni mwaka wa sita na niliacha kuona nikiwa na miaka na 42, sasa nauliza hivi, je? Ninaweza kupata mimba?

Maana zamani nilitumia njia mbali mbali za kuzuia mimba, sasa nilipoachana na mzazi mwenzangu nikaamua kuachana  na hizo njia za kuzuia mimba, kwakuwa nilianza maisha ya kuishi peke yangu.

Lakini sasa nimepata mtu mzima mwenzangu na tunataka kuishi pamoja, je naweza kupata mimba wakati siku zangu sizioni? Mimi na mwenzangu wote hatutaki mtoto, maana kila mmoja ana watoto wake tena wakubwa ,
Naombeni ushauri wenu  jamani,10 comments:

 1. Mama miaka 48 kukoma si umeshakoma labda mungu ashushe muujiza, kwa kuwa mmeshakuwa na watoto kuleni maisha saa hizi mama ukenda klinic si utatukanwa hata na hao manesi na kwa nyonga ipi mama ya utu uzimani hebu ishi wote mle matunda ya utu uzima, tusidanganyane mama yangu.

  ReplyDelete
 2. mama, wala usijali, huwezi kushika mimba tena, huwezi kabisa, miaka 6 bila period ni wazi kuwa umeshafunga, huwezi kushika mimba, wala huna haja ya kuogopa,
  nakutakia maisha mema mama yangu,

  ReplyDelete
 3. Sikujua by the time mtu wafika 42 hiki dhama ya kila mwezi inastop. Ntashukuru kweli

  ReplyDelete
 4. mara nyingi ni 45 huyu sijui imekuaje mimi ilistop na miaka 37 sikukubali niligangamaa mpka ikaanza tena kwani nilikuwa nahitaji mtoto mwingine thanks imefunguka

  ReplyDelete
 5. mwone daktari kwa aushauri zaidi.

  ReplyDelete
 6. usijisumbuwe kunywa madawa, huwezi kushika mimba tena, kwani period zimeshakoma. enjoy maisha yako ya uzeeni kwa raha zako mama yangu,

  ReplyDelete
 7. Jamani naombeni elimu zaidi tafadhali japokuwa mimi nina approach 36 sijuhi mambo mengi sana. Ni kweli ufikapo 45 hii kitu inakoma kabisa? Au inategemea na homones za mtu? Mama yangu kwa mfano alizaa sana nadhani mpaka 45 alikuwa anazaa. Mimi mwenyewe nina watoto wawili lakini tofauti na wenzangu ambao wanapata siku for three days mimi yani mpaka nachoka inakwenda up to five days mpaka six ingawa mzunguko uko fixed. Nina mashaka kama itahacha mapema au ndio ntafika 50 bado tu nahangaika.

  ReplyDelete
 8. ni mimi niliyeuliza kuhusu kupata mimba maana nilikuwa nasikia kunawengine wanapata mimba hata zaidi ya miaka 40 nakuendelea asante sana dada beautytouchdar kwakuweka hii mada ktkt blog yako ili wachangiaji wawezekunichangia nanawashukuru woote walionipa ushahuri mungu awabariki wote asante kwa ushauri wenu

  ReplyDelete
 9. KWA MKASA WA HUYU MAMA MWENYE MIAKA 48 KUSHIKA MIMBA TENA HUWEZI, PERIOD ZAKO ZIMEKOMEA TOKA UKIWA NA 42 YEARS, ILA KWA USHAURI ZAIDI NJOO HOSPITALI MUHIMBILI KITENGO CHA UZAZI WA MPANGO, TUTAKUELEWESHA VIZURI, HII PIA INATEGEMEA NA HOMONS ZAKO THATS Y WENGINE HUTUMIKA SIKU TATU WENGINE 4, NA WENGINE WANAWEZA KAA HATA MIEZI 3 BILA KUONA NA HAWANA MIMBA, SASA KWA HISTORI YAKO WEWE, MZUNGUKO WAKO WEWE NI WAZI KUWA MZUNGUKO WAKO WA USICHANA ULIKUWA NI MFUPI NDIO MAANA ILIKOMA MAPEMA, MIMBA HUTASHIKA MAMA, ENJOY YOUR NDOA, ILA NJOO PALE TUKUFUNDISHE JINSI YA KUJIKINGA MAANA KINGA NI BORA KULIKO TIBA

  ReplyDelete
 10. Asante mchangiaji wa muhimbili. Mimi si muuliza swali ila ningefurahi ungefafanua kidogo maana mie niko nje ya nchi japo natarajia kuja huko miezi minne ijayo. Swali langu ni hivi sie tunaotumika mpaka siku sita saba tuna uwezekano wa kuendelea kupata period kwa muda mrefu kuliko wale wa siku tatu? Maana mimi nina watoto wawili na nina miaka 36 lakini bado natumika siku saba. Embu nielimishe ili nikae mkao wa kula baada ya kuufahamu mwili wangu dear.

  ReplyDelete