Monday, July 4, 2011

NIMEPIMA NIMEAMBIWA NINA UKIMWI?? NDOTO ZANGU ZIMEPOTEA GAFLA NAHISI KAMA NIMESHAKUFA,

Habari yako dada Violet, tafadhali usinitaje jina langu, wala email yangu, nimepewa blog yako na mtu, nahisi naweza kusaidiwa shida yangu
Nilipitiliza siku zangu hivi karibuni nilipata ujauzito,  kwa bahati mbaya ulikuwa nje ya kizazi, kusema ukweli sijaolewa, ila kuna mtu nilikuwa na musiano nae, na ni mwanaume wangu wa kwanza, kwa sasa nina miaka 22,
Ninaishi na wazazi  wangu walezi, maana mama alifariki wakati ananizaa, baba amefariki mwaka jana, sasa nina wazazi wangu wa ubatizo ndio walinichukuwa ili kunisaidia,  basi baada ya mimba kuwa nje ya kizazi nilipelekwa hsptl nikahudumiwa, nilikuwa na maumivu makali sana, na nilikuwa sijielewi kabisa, baada ya hapo nilianza kuumwa sana, siku moja mama alinipeleka  hsptl, wakapima vipimo vyote, na aliwaambiwa wanipime hadi ukimwi bila mimi kujua,

Baada ya kurudi nyumbani mama akaniambia nimeathirika, dada violet, naandika huku nalia, maana ni wiki mbili sasa tangu nitambuwe hivyo, najiona nimeshakonda, nahisi nimeshakufa, ila ninahema,  nifanye nini? Mbona sina matumaini tena, au nijiuwe? Au niende nikakae wapi??  Ina maana ndoto zangu ndio basi tena?? Ina maana sitafanya mambo yangu ya msingi yote??? Au ndio nimeshakufa mimi?? mbona mimi bado mdogo sana, ndio kwanza naanza kuyajua maisha, kwanini nakufa mapema hivi??
 
Nilikutana na yule kaka kwenye harusi moja tulikuwa maids, akanitaka kimapenzi, nilimzungusha kama miezi hivi, badae nikasema namimi nijaribu, ndio tukawa wapenzi, sikujuwa kama naenda kufa, sikujua hata kidogo dada violet, nifanyaje sasa?  Nimelia hadi nimechoka na machozi hayatoki tena, nimeanza kuvimba miguu, nywele zangu zote nimekata , najihisi kama maiti inayotembea, nitafanyaje jamaani, 



20 comments:

  1. pole sana mdogo wangu kwa yaliyokukuta hauko peke yako mwenye huo ugonjwa mimi mwenyewe hapa nilipo ninao huo ugonjwa lakini hakuna mtu anaelewa maana nina afya yangu tu nzuri sasa nikuambie kitu kimoja tu jikubali ukweli unao hiv kuwa na h.I.V sio mwisho wa maisha alimradi tu ufuate masharti ya madaktari utumie dawa sasa ukianza kujikataa mwenyewe nani atakukubali usijinyanyapae mwenyewe jikubali unao anza maisha mapya kwani kuna maisha mengine baada ya kupata ukimwi kupata ukimwi sio mwisho wa maisha wewe tumia dawa kula vizuri mrudie muumba wako uache usherati fanya mazoezi kidogo hata ya kutembea kila siku nusu saa itakusaidia hakuna haja ya kusoneneka maana yameshatokea basi jikubali ukifuata masharti utaishi miaka mingi tu wangapi wanaishi na ukimwi miaka tele hauko peke yako wacha mawazo wacha kulia maana vyote hivyo ukiendelea navyo vitakupunguzia maisha pole sana najua kwa jinsi gani umepata mfadhaiko

    ReplyDelete
  2. pole sana binti,wengi ambao walioathirika ambao hawakutegemea{waaminifu kwa wapenzi wao}hupitia stage kama hyako.mwanzo huwa ni mgumu sana,ila huo ni mwanzo wa kuishi kwa matumaini.kuwa na ukimwi sio kifo,siku hizi unaishi miaka mingi tu,na unaweza ukaolewa na kuzaa.fata masharti ya daktari,muombe mungu wako,huyo ndio kila kitu.na hao unaoishi nao pia wakikupa support utaishi vizuri.

    ReplyDelete
  3. Pole sana mdogo wangu... usikate tamaa mapema hivyo, najua ni ngumu sana kwa upande wako muombe Mungu akupe moyo wa matumaini mapya na wazazi walezi pia unao ishi nayo omba Mungu awawezeshe kukupa support katika kila jambo, kupata maambukizi ya ukimwi si kana kwamba mwisho wa maisha yako umefika mbona wengi wapo na wameishi maisha marefu... cha kwanza unacho takiwa kufanya ni kujikubali wewe mwenyewe ukiweza hilo ni rahisi kupiga hatua, Mungu akuwezeshe akupe nguvu katika wakati huu mgumu ulio nao, usiache kumwomba kila kukicha akupe ujasiri!!

    ReplyDelete
  4. pole sana mdogo tulia fanya maendeleo yako kama ulivyopanga mimi niliolewa nikiwa na virusi vya ukimwi, na mume wangu hakuwa navyo tuliishi uchumba kwa miaka minne kumbe wakati tunakutana mimi tayari nilikuwa na virusi vya ukimwi kwa sababu alinipenda akaamua kunioa hivyo hivyo mwaka 2005 mpaka sasa tuna watoto wanne nimezaa mapacha mara mbili na ni wazima, na mimi naendelea na dawa mume wangu hajaathirika tunatumia condom, ila pale tu tunapotaka kupata mtoto tunafanya mapenzi salama kwa kuchezeana muda mrefu na utelezi kwa sana. Muombe Mungu usikate tamaa Mungu yu pamoja nawe nasi wote tunaishi katika mazingira hayo

    ReplyDelete
  5. pole sana mdogo wangu, ila mimi nakushauri kitu kimoja naomba nenda tena hospitali nyingine ukapime ili upate uhakika maana kuna tatizo kama lako liliwahi kumtokea mdogo wangu akaenda hospitali akiwa anasumbuliwa na maradhi akapimwa hadi HIV daktari akasema ameadhirika, akaja kwenda hospitali kubwa ya bugando mwanza tukampima tena ukimwi vipimo vikaonyesha hajahadhirika akarudia tena hospitali nyingine vipimo vikaonyesha yuko safi. kwa hiyo mdogo wangu nakushauri kapime tena hata hospitali 2 tofauti, mara nyingine inatokea madaktari wetu wanakua hawako makini wanatoa vipimo ambavyo si sahihi. usikate tamaa

    ReplyDelete
  6. lipo tumaini mpenzi wangu kama walivyokushauri hao hapo juu fuata hivyo hivyo kikubwa tuu ujue jinsi ya kuishi la kwanza la pili kubali tatizo usijiulize why, how, where. ishi maisha ya kumushia mungu usikate tamaa, kunywa dawa na dawa inaenda sambamba na maombi.hujachelewa mpenzi wangu, ukijiuwa saa hizi utaingia mbingu ya nani. watu wanaishi wanazaa,weka malengo ya maisha yako kama kawaida. na ukisimama ktk bwana unapona

    ReplyDelete
  7. Sina la kusema kwa kweli ila naelewa kabisa kuwa kuna watu wengi sana wenye tabia nzuri na wasiostaili kupata huu ugonjwa lakini bado wanapata. Kama walivyoshauri wengine hapo juu mdogo wangu mtumanini Bwana utaishi muda mrefu sana. Nami pia nakuombea.

    ReplyDelete
  8. kama hatomaind huyo bint naomba mpe mail yangu ni kadinari4@yahoo.co.uk aniandikie no yake ya simu mimi nitampigia ningependa niongee naye kwa kirefu sana, na utulivu mimi dada

    ReplyDelete
  9. Da Vai... naomba km inawezekana niongee na huyo binti. Ni mdogo sana kufikiria hayo anayoyafikiria sasa. E-mail yangu ni jj_temu@yahoo.com. Naitwa Mama Vanessa. Mpe e-mail yangu..km hatajali awasiliane na mimi. Mwambie NAMPENDA SANA..!

    ReplyDelete
  10. pole sana, ila ukimwi sio mwisho wa maisha na ukimwi sio kifo, wangapi wanakufa kwa ajali? ikubali hali halisi, hudhuria vituo vya ushauri nasaha, kula proper diet, ishi maisha kama kawaida na epuka maambukizi mapya, maisha yanasonga kuna w...atu wanaishi na virusi for 20 years na wanasurvive, ndoto hazijafa tena ndo uziendeleze kwa moyo wote. kumbuka maisha ni vile utakavyoyachukulia ukichukulia kuwa umekufa utakufa kweli mbona kuna watu wanaishi na magonjwa makali hatarishi kuliko ukimwi? wangapi wanaishi na kansa, wangapi wanaishi na athma? leukemia na magonjwa hatari, usikate tamaa

    ReplyDelete
  11. Usikate tamaa kama unamwamini Mungu utapona mwombe mungu sana tubu na damu ya yesu itakuponya badilisha damu yako kuwa damu ya yesu na kila saa ukiri uzima katika damu yake naimani mungu atafanya jambo, mana katika damu ya Yesu kuna uzima.

    ReplyDelete
  12. MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU MTEGEMEE YEYE KATIKA KILA JAMBO USIKATE TAMAA. WEWE SI WA KWANZA NA HAKUNA MTU ANAYEPENDA KUISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI. MRUDIE MUNGU WAKO NAAMINI HUKO KUNA UKOMBOZI WA KWELI. AMENI

    ReplyDelete
  13. Pole sana mdogo wangu,ila nakutia moyo kwa Mungu wetu hakuna kinachoshindikana,chukua hilo kama ni jaribu,jipe moyo najua kwa nguvu zako ni ngumu sana na ndio maana unajisikia hivyo,ushauri wangu muombe sana Mungu na imani utaweza tu.Pole sana na Nakupenda sana wish ningepata mail yako

    ReplyDelete
  14. Me nashauri uende ukapime tena peke yako zaidi ya mara moja,baada ya hapo ndipo utajua ufanyeje.Huwa inatokea wapimaji kuchanganya majibu.

    ReplyDelete
  15. pole sana baby usikate tamaa huo sio mwisho wa dunia nenda kapime tena kama kweli pima cb4 zako anza kuishi kwa matumaini mana watu wanaishi 2o years kikubwa ni kujikubali mi mwenyewe niligundua nikiwa mjamzito wa mtomto wa 2 nimejifungua sikumnyonyesha mtoto yuko salama ana miaka 4 na niko poa huwezi nitambua na wala sijaanza kutumia dawa kikubwa ni kukubali matokeo nendA UKAPATE USHAURI NASAHA PIA UTSAIDIA

    ReplyDelete
  16. Mimi nawapongezeni woteeee mlio mpa binti ushauri kwa kweli mmeongea vizuri sana maneno yenu yanaleta matumaini,Namwomba binti asome na kufuatilia yale yote aliyoshauriwa, kweli ushauri wenu nimeupenda hongereni sana.

    ReplyDelete
  17. pole sana dada ulieipatwa na tatizo hilo, mi mambo mengi ya kusema ila ngoja ni weke kwa ufupi, ukweli ni kwamba Maambukizi ya HIV yanapunguza tu life expectancy ya mtu,ila unaweza timiza ndoto zako hata kama una maambukizi,kua na familia na kua na watoto pia inawezekana kabisa,
    hakuna atakaye ishi milele dunia hii, tumia dawa nawe utadumu bila kua na tatizo lolote hata zaidi ya miaka ishirini ijayo hasa kama umegundua mapema sana kabla vidudu havijakuharibia kinga yako,
    dunia pia inazidi gundua ARVs zenye uwezo mkubwa wa kupunguza kasi ya kuelekea kwenye full blown AIDS, baada ya miaka kumi ijayo inwezekana kukawa na dawa zenye nguvu kuliko tulizo nazo leo hii kuzuia kasi ya virus.
    ni mengi ya kusema ila kwa sasa tuishie hapo, soma sana web site za HIV/AIDS na kamaunahitaji msaada na comfort zaidi,waweza wasiliana nami mi ni MWANAFUNZI WA UDAKTARI, na hisi naweza saidi pia! kama mwenye blog anaweza toa email yako tunaweza wasiliana.or live a massage on emaridadi@yahoo.com thanxs

    ReplyDelete
  18. jamani nimesikitika pole mtoto mzuri, usikate tamaa wamekushauri vizuri wote waliopita jikubali usikasirike endelea na maisha mengine ya matumaini watu wengi wana matatizo hata mimi nilipata matatizo katika umri mdogo sana lakin namshukuru mungu naendelea vizur na maisha yanasonga mbele. Mungu akutie nguvu nakutakia kila la kheri love u sana

    ReplyDelete
  19. Pole sana dia, usikate tamaa sio mwisho wa dunia,bado unaweza kutimiza malengo yako,kuwa na Ukimwi sio kufa,nenda kawaone wataalamu kama umefikia muda wa kuanzishiwa dawa za kupunguza makali watakuanzishia,ila sasa ishi kwa uangalifu ili usiongeze maambukizi,hakikisha unakuwa na furaha,mweke Mungu karibu yako,sali sana ili upate faraja na utaishi maisha marefu. Mungu akutie nguvu,usikate tamaa dia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sama mdogo wangu, mbona hata mimi ninaishi na maambukizi ya ukimwi na maisha yanaendelea vizuri tu. Nakama ukiniona huwezi kuamini kama nina maambukizi kutokana na afya yangu ilivyo nzuri, kitu cha kwanza ni kujikubali wewe mwenyewe kwamza, kula vizuri, punguza mawazo kabisa,pata muda wa kupumzika na ufanye mazoezi japo madogo madogo na apende sana kufuatilia habari yahusuyo ukimwi. pia kama una pesa kunywa dawa inayoitwa OMEGA 48 inapatikana South Afrika lakini hapa dar wanayo blach sub blach yao. emagine mara ya kwanza wakati napima nilikuwana CD 324 lakini baada ya kunywa imepanda mpaka 620, na hapo sijaanza ARVs. hata nilipoenda hospital walishangaa kwann CD4 zangu zimepanda kwa haraka hivyo kwa kipindi cha mwenzi mmoja tu. lakini nashukuru mungu maisha yanaendelea na sina wasiwasi tena. kwahiyo nakuomba sana usikate tamaa.

      Delete