Monday, June 27, 2011

SIJUI NJIA GANI YA UZAZI WA MPANGO HAINA MADHARA NAOMBA USHAURI

Hallow dada violet mimi ni mama wa mtoto mmoja namshukuru Mungu anaendelea vizuri, dada violet naomba ushauri ipi ni njia sahihi ya kuzuia mimba kwani

nilikuwa natumia sana mipira (condom) ila naona inanidhuru kwani inanisababishia kuwashwa mara kwa mara. naomba ushauri wako na wadau wengine nitumie kinga gani kuzuia ujauzito kwa sasa kwani mwanangu bado ni mdogo anaitaji ukaribu wa mama. asante sana




20 comments:

  1. du! maada hii imetugusa wengi, mimi ndio hata sijui yani, naona mungu tu ananisaidia, nachanganya changanya, tusaidieni wote jamani, maana hatujui hata tufanyaje, sivyo tutazaa watoto kama vipanya. mh!

    ReplyDelete
  2. Njia nzuri kuliko zote ni kalenda peke yake fuata tarehe zako nunua kalenda weka chumbani kila mwezi unafanya hivi ukianza tuu siku zako unaanza kuhesabia baada ya kumaliza period, unakutanna na mumeo siku nne mfulilizo baada ya hapo unastop siku nane ambazo ni siku hatari ukimaliza hapo unaendelea unakutana na mumeo mpaka unaanza period tena hata unakutana naye leo unaanza perio baada ya masaa mawili maadamu uliepuka siku nne za hatari hiyo ni njia ambayo mimi imenisaidia sana sana ila mumeo inabid awe muelewa hizo siku nane usijepata mimba maana hapo ndio siku za za kupata mimba, njia zote za kinga ni nzuri kuzuia mimba lakini zinamadhara kila njia ina madhalanjia nzuri ni hiyo ya kalenda tuu.

    ReplyDelete
  3. Mumeo akikaribia kukojoa atoe nje then akojolee nje! hiyo mi ndo ninayo itumia naweza piga hata 3 zote namwagia nje na mke wangu hapati mimba nami nakuwa hamu imeisha! kama hawezi tumieni kalenda

    ReplyDelete
  4. jamani mimi pia nina ilo tatizo anony ulieelezea kuhusu tarehe basi sijaelewa vizuri samahani naomba mtufafanulie kwani tuko wengi asante sana

    ReplyDelete
  5. mmejaribu kuweka vipandikizi??? nafikiri ukiweka vipandikizi inaweza kusaidia kama kikikupenda, mimi niliweka mwanangu alipokua na mwaka mmoja, sasa hivi ana miaka 3 naenda kutoa, naweka kingine tena]
    na wala hakinisumbui, napata siku znagu kama kawaida,
    MAMA IRENE

    ReplyDelete
  6. Ni mada nzuri sana kwakweli, binafsi ili kuepuka migongano huwa natenga siku kumi kumi, yaani tufanye nimeanza bleed tarehe 1 basi huwa nahesabu hiyo tarehe 1 hadi 10 hapo nipo huru (nimeinclude na period) nikimaliza hizo nahesabu tena tarehe 11 hadi tar 20 kuwa si salama thn kuanzia hapo naendeleza libeneke hadi tarehe nyingine ya kuanza siku za kubleed.
    NB: Ninapokuwa kwenye danger days hubby huwa anakojoa nje, njia hii ni nzuri na rahisi, kondom huwa zinaleta muwasho as una fungus.

    ReplyDelete
  7. jamani njia ya kalenda ni nzuri sana na mimi ndo naitumia na niko kama zamani sijabadilika maana nasikia hizi njia za kizungu zinaharibusana maimbile na maumbo ya wadada.
    sasa hii njia ya kalenda inabidi uwe makini kidogo na mkubaliane na mume wako kwa kifupi najitolea mfano mimi hapa Mzunguko wangu ni siku 28 ila kuna siku inaweza kwenda hata siku 30 ila cha msingi ninachokifanya ninahesabu siku 9 toka nilivyoona periodi yaani kama nimeona tarehe moja nikamaliza tarehe tano so kianzia tarehe 6 hadi tarehe 9 nafanya bila kinga yeyote kuanzia tarehe 10 mpaka tarehe 17 ni hatari so huwa natumia kinga na mume wangu anakuwa makini sana na inabidi msaidiane maana hapo ukifanya mchezo utapata mimba kuanzia tarehe 18 mpaka siku yakuona tena periodi huwa nafanya bila kinga so huwa haina kazi kama wote mmekubaliana kutumia njia hiyo

    ReplyDelete
  8. Dada ulotoa mada hapo juu ya Kalenda kidogo itawachanganya wengi. kalenda kwa kweli ni nzuri mno ila inategemea na mzunguko wako wa mwezi. Nijuavyo mie, unapoingia kwenye cku zako unahesabu siku saba (7) za period, then next seven ni siku nzuri kabisaaaa za kukutana na mmeo halafu saba ya tatu (i mean kuanzia siku ya 15 hadi 21 HAPO NDIPO KWENYE HATARI ZOTE)unacheza lakini unakuwa makini kwa kumuasa mwenzi wako atolee nje, na saba ya mwisho yaani kuanzia siku ya 22 mpaka 28 ni BURUDANI KWENDA MBELE hata ufanye usiku na mchana hakuna tatizo lolote. HII NI KWA WALE WANAOKWENDA SIKU 28 ila kama tarehe zako ziko vice versa kwa kweli ni ngumu sana kutumia Kalenda. KWA HIYO SIKU ZA HATARI NI SABA TUU KATIKA MWEZI. TUONE MAONI YA WADAU WENGINE TENA.

    ReplyDelete
  9. asante dada Violet kwa mada nzuri, pia niwashukuru wadau kwa kutuelekeza juu yahili, nami naomba niwape ujuzi wangu,
    MIMI HUWA NATUMIA VIDONGE, Ila navitumia pale ninapocheza vibaya tu! nafanya hivi, SIKU 10 (included period days) huwa nafanya bila kinga, ila from there to tarehe 20 hapo kati nikifanya tu! HUWA NAMEZA MAJIRA ILE NYEKUNDU, KIDONGE KIMOJA, MAANA KINAENDA KUHARIBU YI KABISA,
    kile kitendo msikipimie jamani, jamaa akishazidiwa unadhani ataweza kupiz nje??? hawezi kabisa, so kma ikitokea amepiz ndani na huna hakika na hizo siku, bora ujimezee majira yako kidonge kimoja tu ndani ya masaa 12 kazi kwisha
    Mday A-Town

    ReplyDelete
  10. Mdau wa kuanzia siku ya 15 hebu angalia vzr coz hii hata kwenye biology tulifundishwa, mwanamke yoyote mwenye mzunguko wa siku 28 siku ya 14 kuanzia siku ya kupata kwake period ni siku ya hatari sana coz ndo siku ambayo yai hupevuka so utake usitake lazima upate mimba tht day.

    NB: Mimi binafsti siku zinabadilika sana mara siku 28 mara nyingine hadi thirt something lakini huwa natumia ile ile ya kutenga kumi kumi. Sijui lakini kwa wengine.

    ReplyDelete
  11. Mama KWC tupo pamoja kabisa mimi ni mdau niliyetoa hiyo ya nine days toka siku ulivyoona japo mara nyingine natenga kumi ila nakuwaga na wasiwasi kidogo kama nikipiga na ile ya kumi. huyo aliyesema 15 days mmhhh hapo kidogo umeingia msituni maana ukifanya tu ile siku ya 14 au masaa machahe kabla ya hiyo siku ya 14 ujue lazima utapata mimba cos sparm zinauwezo wakukaa ndai kwa 24hrs zikiwa bado hai. so kama mzunguko wako ni wasiku 28 au 30 na bado unafanya mpaka ile siku ya 15 kuna tatizo hapo. mimi nimetumia kalenda more tha 3yrs now na huwa najitengea siku zangu 9 au 10 kuanzia nilivyoona perion from there natenga nyingine 7 au 8 wala sijawahi kupata ujauzito na niko vizuri kabisa na watoto wangu 2. NYIA YA KALENDA NZURI SANA HASA WOTE 2 MKIKUBALIANA.

    ReplyDelete
  12. Mimi mume wangu amekuwa anamwaga nje na tumeishi hivo huu ni mwaka wa tisa na tuna watoto wawili tu ndio tuliokuwa tunawahitaji. Ila kwa sasa nafikiria kwenda kuweka vijiti kwani hapo awali sikuwa najali nilikuwa na mtoto mmoja kwa hiyo ningepata ujauzito wa bahati mbaya ingekuwa poa tu. Kwa kweli nina wasiwasi wanaume wanapata tabu sana kumwaga nje ndio maana nataka kuweka vijiti. Ndugu zangu wanantumia vijiti na havijawaharibu shape inategemea mwili na mwili. Nataka mume wangu na mimi tu enjoy siyo unafanya huku full wasi wasi hata raha haipo. Huyo mdau anaesema anakunywa no mistake pills (kama nimepatia jina) namwomba awasiliane na madaktari kuna rafiki yangu alikuwa na huo mchezo akaja ku learn kuwa ni njia hatari sana kiafya amehacha.

    ReplyDelete
  13. mada nzuri sana sante. Njia zote za kizungu ni hatari. wataalam wanashauri kalenda au njia za asili. kuna Dr Mwaka Ilala 0715331144 NA 0755720720 kalibu na TAWLA anatoa njia ya asili ni mbegu fulani unapewa maelekezo na pia yupo Dr Alice Mgasa yupo Makumbusho sokoni chumba namba 035 kalibu na wauza ndizi Bukoba wa jumla na lejaleja utapata ufumbuzi bora.hawa wote wanatoa elimu kwenye TV na radio (ITV, Wapo radio na Magic FM)

    ReplyDelete
  14. Naomba nisaidie dada njia gani ni nzuri ya kuzuia mimba?

    ReplyDelete
  15. navyo ona mimi nyia nzuri ya kuzuia mimba ni ya kuweka vijiti au kwenda kwenye hospital za uzazi wa mpango wakupatie ushauri zaidi kusema ukweli wa mungu mimi nilikuwa napenda kutumia calenda ila sasa mwisho wa siku uwezi kuzuia hisia ua kuzuia hisia za mwenzi wako anapokuitaji kimwili utapaswa utoe ushilikiano kama yeye anapooneshaga kwako,sasa ikafikia hatua napata mimba mara nne mfululizo kwakuwa sikuwa tayali kuzaa niliabortion lafiki yangu mmoja akanishauri kama alivyosema mdau mmoja nimeze vidonge pindi nimalizapo sex ilikuwa inasaidia kiasi fulani ila sasa ikafkia muda ilibidi niache maana tumbo lilikuwa linanisumbua kutokana na vile vidonge ila kwa sasa tumeshauriana na mpenzi wangu na mama yake ametushauri ni bora tutumia njia ya vipandikizi yani vijiti,niseme neno moja kalenda au vidonge umalizapo sex ni bure kabisa ni kheri utumia njia nyingine

    ReplyDelete
  16. Mi nadhani mtuasimkosoe sana mwingine maana kila mmoja wenu ameeleza usoefu kulingana na mwili wake ulivyo. kwahiyo mi naona, huyo anayeshauriwa kutumia kalenda, ni njia nzuri ila inabidi km hajui namna ya kifuatilia, amtafute mtu aliye hodari wa kufuatilia ili aweze kujisoma mwili wake vema b4 hajaanza. akiufahamu mwili wake vema, hapo anaweza kuanza, na itakua salama kwake.

    ReplyDelete
  17. UKWELI NI HUU,
    SIKU 12 ZA KWANZA BILAKUJALI UMETUMIE SIKU NGAPI NI SALAMA, SIKU YA 13 HADI 17 SI SALAMA, BAADA YA HAPO SIKU ZOTE NI SALAMA

    ReplyDelete
  18. Nimeipenda mada hii. Mimi nina mtoto mwenye umri wa miei miwili na tangu nimejifungua sijaona siku zangunsasa hiyonkalenda ntaitumiaje?

    ReplyDelete
  19. Hii njia ya kumwaga nje mwanaume wakati mwanamke akiwa kwenye hatari,cku zaka je mwanamke anapata raha kweli?maana huwa inatokea mwamke anataka kumwaga at the same time mwanaume naye anataka kumwaga,sasa ukitoa nje huoni ya kuwa utamkatili mwanamke.

    ReplyDelete
  20. kwakweli njia ya kumwaga nje unapoteza nguvu nyingi bila kujua mwanaume anajiumiza

    ReplyDelete