Wednesday, June 22, 2011

JE TABIA MBAYA ZA MUME ZINAWEZA KUBADILI MSIMAMO MZURI WA MKE?

Leo tuongee wapendwa wangu,
Inasemekana kuwa baadh ya tabia za wanawake walio wengi huwa ni nzuri sana, kipindi cha mwanzo na hasa katika upande wa mapenzi, lakin kadri siku zinavyozidi kwenda, mambo hubadilika na kuwa kinyume, wanaume wanabadili tabia kiasi cha mke kujuta kwanini aliolewa, 
Katika kupekua pekua kwangu, nimeikuta kitabu hiki, kimenivutia na nimeamini ni kweli kabisa, nimeileta kwenu tufundishane, kitabu kimeandikwa
75% of woman’s are in loveless and lifeless marriages


Wanaume wengi sana huficha makucha yapo wanapotaka kuoa, hujifanya wastaarab sana, lakini baada ya ndoa kufika miaka 2 au 3 mambo huenda ndivyo sivyo,  unakuta mwanaume amekosea kosa ambalo hata mtoto akiona anajua kweli baba kakosea, lakini wanaume wanjifanya MANUNDA, hawakubali makosa, wala nini

 
Mbaya zaidi atakapoanza mahusiano nje ya ndoa, uaminifu hakuna tena, gubu mara kwa mara, anaweza lala vizuri, akaamka amenuna, au anaweza fanya mambo kwa siri bila hata kukushirikisha mkewe, na hata ukimkamata kwa hicho cha siri alichokifanya, bado anaweza kuwa mbishi na kukugeuzia kibao, na unaweza kuthibitisha pia, lakini bado akajifanya mbishi, ah!~ tabia hii inakera sana jamani


tena bila hata haya wengine hudiriki kuongea na simu za wanawake zao hata mbele yako, ukiuliza unajibiwa, mfanyakazi mwenzangu, wakati unaona dalili zote kuwa ni simu ya mapenzi Mwingine anaweza kuanza hata kumdunda mkewe, kwa sababu za kipuuzi, au kama akiuziwa huko nje na wanawake zake basi hasira zake zoote zinakuja kuishia kwa watoto, sasa ndio maisha gani hayo jamani?

Yote tisa, kumi akichukia eti  hata matumiz ya familia haachi,
Sasa je, kwa haya yote na mengine unayoyajua wewe, ni kweli yanachangia 99% kubadili tabia nzuri au msimamo alionao mkewe?


Wanawake tunapenda sana kupendwa, kubembelezwa, kuelekezwa kwa utaratibu, kusifiwa, na kuheshimiwa sana na waume zetu, hali inayopelekea msimamo wa mwanamke kuwa imara zaidi, na vipi kama ukivikosa vyote hivyo kwa mumeo?

Always umekua mtu wa kujuta, kulia, na huna furaha, sasa hali hii inaweza kubadili tabia yako na kutamani kufanya yasiyostahili???

Na kama ndoa imefikia hatua hiyo tuambiane, tufanyaje ili turudishe hali nzuri na maisha ya furaha kama tuliyokuwanayo awali??????
Kuna wanandoa wenzetu wanaumizwa sana ndani ya ndoa zao, hawajui wafanye nini, wamekata tamaa, hawana hata mdaada wa mawazo, 

sasa hebu tusaidiane kueleweshana nini cha kufanya pindi ndoa zetu zianzofikia hali kama hii

sometimes huwa naona kama vile ,Mungu anayaachia yote hata kwakuwa tunajisahau mno kumuomba, wakati mwanzilishi wa ndoa ni Mungu mwenyewe, sasa kumuomba amani ndani ya familia zetu hakupo 

tena, tukishavua mashera tu! basi na maombi mwisho, 
wapendwa, tukumbuke kuomba, maana hakuna linaloshindikana kwa Mungu
tunaomba busara zako mpendwa, na naamini kwa kupitia hili wamama wengi walio kwenye ndoa watapata msaada

  lakini

9 comments:

 1. wanaume wanakera sana bwana, dawa yao ni kuwatafutia wanaume wenzao, shenzi taip

  ReplyDelete
 2. hata kama wanakera sasa tunarisotije na sio kuwatafutia wanaume wenzao sio solution ndugu yangu.ni kweli ulivyoandika dada V hii mada imenigusa sana mf mimi mume wangu sio mkali ila Da hakuna kitu kinaniudhi ukimuliza kitu umahitaji msaada wa haraka ufanyeje, anakwambia subiri na anaweza kukupa jibu hata baada ya miezi mitatu wakati mimi nimshakuwa na maamuzi mengine, auna umeshasahau, au kachoka hataki kuongea ukimuliza kitu anakuangalia tuu yaani ignore kwa sana, lakini vitu kama hivi ukishajua wala hupati shida navyo vilele unaendelea mbele na maisha yako na kila kitu kinaendelea kama kawaida ila kweli wanawake tunahitaji kkumbelzwa, kupendwa na mambo mengine
  unajua ni rahisi mwanamke kujitoa kwa mwanamme kuliko mwanamme kujitoa kwa mwanamke ni wachache sana sana

  ReplyDelete
 3. Umesema ukweli dada v, yani kuna dada yangu mimi, mumewe anamnya nyasa sana, kuna siku alitaka kunywa vidonge afe, ndio familia ikamsihi sana, yani umeongea ukweli mtupu dada, huyo dadayangu akikusimulia story yake unaweza kulia sana, inasikitisha, ngoja nipate ushauri hapa halafu nitambwambia dada yangu labda utamsaidia,
  ANITA

  ReplyDelete
 4. cha msingi ukipata pa kukupoza, wewe pozeka, wanaume wanatabia za kukera na kudharirisha sana, utakaa unamlilia mtu mmoja tu wa kazi gani, ndoa hizi! jamani mh! natamani kuwaambia ambao hawajolewa wasiolewe, ila sidhani kama watanielewa, acheni tu! waolewe wajionee wenyewe,
  ushauri wangu, mmeo akikuzingua, nawewe mzingue
  NO NAME

  ReplyDelete
 5. Wanaume bwana ni mizigo tuu pale anapokuhitaji ndipo anapojua kubembembeleza. So la muhim sisi wanawake, ni kuwachukulia kama walivyo na kikubwa tunang'ang'ana kwenye ndoa zetu kwa ajili ya watoto na si vinginevyo. KWA UJUMLA WANAKERO MNOOOOOOOO

  ReplyDelete
 6. Jingine kwa wananume jamani ni gumu sana na linauma mno mno wanaume jamani jamani jamani jamani jamani ni wagonjwa wa HIV wanakunywa dawa na wanajua jinsi ya kuishi wake zao wanaangamia wanaongelea virus inanisikitisha sana sana. Tatizo limeshaingia ndani ya nyumba mshirikishe mwenzio jamani, na sisi wanawake tukiona mapungufu ndani ya nyumba huko chumbani ni bora kuwa wazi kuliko kuwa kimya na zaidi ya yote kuwa na uwelewa na ufahamu jamani inaumiza sana sana sana na inasikitisha jamani wanawake tuwe makini ikibidi kupima wewe mwenyewe binafsi kapime tusiogope. watu jhawafi kwa HIv ukijua jinsi ya kuisha ili ulee wanao,asante kwa mada hii dada V

  ReplyDelete
 7. Dada V mi ushauri wangu unatokana na imani yangu ya dini ya kiislam amabapo kuna aya ktk Quran inasema hata mume akiwa na matendo mabaya mwanamke akijitahidi kuwa mwema basi mume atabadilika. Na hili nimethibitisha mimi mwenyewe binafsi, maana mume wangu ni mtu mwenye gubu, mbinaafsi,contoling freak,wivu wa hli ya juu analotaka ndio hilo hilo.mwanzoni nilikua nami sikubali napambana nae akinitusi namtusi akinuna nanuna basi mambo yalikua mabaya ndani kulikua hakuna furaha wala amani mpaka siku moja nikamsikia kiongozi wa dini ktk TV akizungumzia matatizo ya ndoa na kwamba wanawake ndio wenye kusafer at the end of the day na akatoa aya na ushauri nikaufata. Nikaamua kuwa mpole mwenyewe akianz kupandisha mi namjibu kwa upole na kuomba samahani na kuongea kwa adabu basi huwezi amini anabadilika na anona aibu kuanzisha maugomvi yasiyo na maana.Hivyo wanawake wenzangu tusishindane nao hawa cha muhim ni kuignore wanapokua na mahasira ngojea katulia muingize mungu ktk maongezi yenu na siku ya kufa na siku ya kiama basi hapo utmuona mwenyewe anarudi chini maana hakuna mwenye jeuri ya kumpinga mungu na mambo yakua fresh na utakua na furaha na amani.Tatizo letu sisi wanawake ni jeuri na midomo ndio inayotuponza.mtii mume wako akikwambia usifanyi jambo achana nalo ankupenda ndio maana akakuoa wewe na kama anatimiza majukumu yake nini unataka. maisha ya hapa duniani ni mafupi unaweza ishia mateso hapa na ukaenda motoni ukifa.pigania yaliyo muhimu kwako hapa duniani na yatakayo kupa nafasi nzuri kesho ukifa. ni hayo tu.

  ReplyDelete
 8. Hi

  Jamani mada ni nzuri na imenigusa hasa ila tutaendelea kuwa wapole mpaka lini?kila siku sie tu wanawake na wao wanaume watabadilika lini au sie ndio wakuomba msamaha siku zote ili hali wakati mwingine makosa wanaanza wao?

  Mie nina mfano ulio hai kabisa yamenitokea nilioloewa miaka miwili ilyopita lkn kabla ya ndoa nilizaa na huyu mume wangu na mpaka ss tupo wote ila tabia zake kwa kweli sipendi kabisa na kila anikoseapo namwambia mie sipendi hivi na hivi lakini mwisho wa siku ananuna tunaweza kaa hata wk atuongei na kula twala wote na kitanda kimoja tunalala sasa infika stage mtu na ww unachoka kuomba samahani kwani wao wanaume wakianza sema sorry watakatika mikono?

  Sawa kila kitu ni kuomba kwa mungu ila kwa hawa wanaume zetu wa sikku hizi wamezidi jamani ni tofauti na baba zetu so na wao wabadilike wajue nn maana ya maisha ya ndoa na hatuwezi ishi siku zote bila kukwaruzana na kitu kingine hakuna swala linalokuwa gumu kwao kama kwenye simu mume wangu mie uwa tunagombana sana kwenye suala ilo simu yake dada vai ina password ukiwasha tu inadai uweke password so anaficha nini kama sio masuala hayo hayo ya wanawake ila yangu mie haaaaaaaaaa angaalie nani kapiga na nani katuma msg so hapo ni ugomvi usioisha ndani ya nyumba kila leo.na hata siku akiiacha tu nikipekua nakuta msg za msichana anasema kamiss period so hapo mtu unachukua hatua gani km sio kuchukua namba ya huyo msichana na kumpa ukweli wake then mwisho wa siku huyo msichana anakutakana na mumeo nae ndani ugomvi amuelewani na anakujibu simu yangu haikuhusuuuuuuuu so mtu km huyo unamfanya nn nami nakaa namuangalia macho coz nimemsemea kwao naona hali ndio hiyo hiyo tu so nina kitu ndani ya moyo ambacho hakiwezi isha leo wala kesho so kumpenda nampenda ila tabia zake hapana na nimekaa nae na kuongea nae mwanzo mnaanza vizuri mwisho anakujib kunyaa.

  Na wao wabadilike sanaaaaaaaaa tu waache vimada vyao vya nje.

  ReplyDelete
 9. kwa kweli nami sina la kuongeza ila cha msingi nanyie wanaume mbadilike na nyinyi pia mjifunze kuomba samahani na mue wepesi kukiri makosa yenu.

  ReplyDelete