Monday, June 13, 2011

NI MUME WANGU WA NDOA, ANANILAZIMISHA KUTOA MIMBA, HATAKI NIZAE, NIFANYAJE


Habari yako dada violet,

Pole kwa kazi mama, mimi naomba ushauri maana sielewi nifanyaje? Nimeolewa huu mwaka wa saba sasa, tuna watoto wawili, wote wa kiume, baada ya kujifungua mtoto wangu wa mwisho aliniambia nifunge kizazi kabisa, nisizae tena, nilipomwambia mama yangu alinikemea na kuniambia bora nijikinge kuliko kufunga kizazi nikiwa bint mdogo,

Sasa nimeshika mimba, na ina miezi mitatu, mume wangu hataki hata kusikia, ananilazimisha kuitoa, nimejaribu kumueleza madhara nitakayopata, lakini haelewi, ananifokea tu! Kwanini sikujikinga, na alichosisitia ni kwamba nitoe mimba hii,  mimi roho inaniuma sana kwenda kuua mwanangu, naumia sana na mume nampenda, naombeni ushauri wanawake wenznangu nifanyaje?



10 comments:

  1. Wewe usiwe mjinga! ukitoa hiyo mimba na ni miezi mitatu rafiki utaja poteza maisha bure!! Unafanya kazi au ni mama wa nyumbani? Kama unafanya kazi nini kitakachokushinda? Ushauri wangu kwako acha hiyo mimba uzae ndugu yangu, hata kama atakukasirikia achana naye, lea mimba yako nami nakuombea kwa mwenyezi Mungu upate mtoto huyo Bwana mwenyewe atakavyokuwa anampenda. Usitoe tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Raha ya kutoa mimba mkubaliane wote, labda hamkua na mpango wa kupata mimba sasa imeingia kwa bahati mbaya, na kutoa labda wiki mbili, tatu au mwezi tu lakini miezi 3 kwa kweli sikushauri.

    ReplyDelete
  3. Usitoe dada1 kuna mdada namfahamu alipata mimba tena bila kujua, kwani alikuwa akinyonyesha bado. Basi alipokuja gundua kuwa ni mimba akataka kuitoa mimba ya miezi 4, lakini alipoambiwa asitoe akaacha, na Mungu akamjalia akapata mtoto wa jinsia ambayo hakuwa naye. So muombe Mungu akusaidie. Utajifungua salama na mwisho wa siku huyo bwana ataona aibu. Mwanaume hana hayaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Hata kama maisha magumu imeshatokea hakuna jinsi.

    ReplyDelete
  4. usitoe hiyo mimba acha akasirike acha akufokee miezi mitatu ni kiumbe tayari, na pili kumbuka unariski maisha yako ndugu ukifa saa hizi watoto wako unamuachia nani, na kwani umepewa na mtu baki, achana naye huyo zaa mtoto wako unaweza hata badilisha uzazi ukapata wa jinsia tofauti na hao wa kiume usimjibu wala nini wala usimsilize hata kidogo kaa kimya atasema atanyamaza na atachoka.

    ReplyDelete
  5. usimsikilize mumeo, hata akakupiga, husitoe. Na kaa hapo hapo home husitoke.Kama hataki mtoto basi haondoke yeye na akuachie nyumba, mpaka siku atakayo itaji watoto basi arudi. Na kamshitaki kwa wazee. Shika mimba hata mara 4 ilimladi nawe upate mtoto wa kike, atakae kuwa rafiki yako na atakae kukuosha uzeeni na utakapo kuwa hoi mgonjwa. Yeye karidhika kwa vile kaona kapata midume itakayo msafisha uzeeni. Watoto mali bwana, mtoto wako atakutunza kwa upendo uzeeni ila mtoto wa dada ako sizani kama atakuwa na mapenzi nawe kama ulie mtoa wewe mwenyewe tumboni

    ReplyDelete
  6. Jamani huyo mwanaume hana hata haya anakuambia eti mbona hukujikinga kwani si niwajibu wake pia kujua siku zako za hatari. wanaume wengine bwana hewa kabisa. USITOE MWAYA TENA MUNGU ATAKUJALIA UJIFUNGUE MTOTO WA KIKE

    ReplyDelete
  7. Tunamlaumu huyu baba bureeee... huyu mama ana watoto wangapi? je wanashirikiana ktk kushomesha/kulea watoto? unaweza kuta huyu baba ndo anahudumia watoto mwanzo mwisho, ss asimnyime kuzaa wengi???? coz akina cc mambo ya ada na nini ni jukumu la baba.. ss mwenzangu una watt 3 au 4 bado unaendelea kuzaa huoni km ni ukosefu wa akili? watoto ni mali ndio lkn mpk wafikie kuwa mali ni another isue... ukishajifungua huyu mtoto naomba ukafunge kizazi au tumia njia yeyote ya uzazi wa mpango usikoseshe raha mtoto wa mwanamke mwenzio alaaa!!!!!.. kila mtu anapenda kuwa na watoto wengi lkn hali ya maisha ndo inawabana.

    ReplyDelete
  8. wewe hapo juu unayemshutumu mwenzio sasa mimba imeshaingie aifanyeje, na kwani kajipa mwenyewe, kama uzazi wa mpango wapange wate.usimlaumu mama wa watu bure.
    sasa ishakuwa hivyo aifanyeje zaidi ya kuzaa

    ReplyDelete
  9. wote wamekushauri vizuri sana.

    ReplyDelete
  10. Nendeni kwa washauri wema, wakuu wa dini au hospitalini, mkapate ushauri...
    SWALI LAKUJIULIZA : Mfano yeye ndiye angekuwepo humo tumboni,akatolewa angkuwepo kwenye hii dunia? Muogopeni mungu!

    ReplyDelete