Sunday, January 9, 2011

NIMEZAA NAE WATOTO WAWILI, ANAWAKATAA ANASEMA SIO WATOTO WAKE-NIFANYAJE?

Halow dada, habari, mimi ni mama wa miaka 29, nina watoto wawili wamiaka 5 na mwaka mmoja, wote ni watoto wa mume wangu, ambae tulifunga nae ndoa ya kiislamu, mimi nilikuwa mke wa pili, nilizaa nae mtoto wa kwanza, badae tukapishana tabia, nikaamua kuondoka na mwanangu, akafanya uhuni wakee, alipochoka akanifata na kuniomba turudiane,

wazazi walitukutanisha na kutuweka sawa, tukasameheana, nikarudi kwake huko chuo kikukuu (dar es salaam) maana mume wangu ni muhusika wa hapo, basi tuliporudiana tu! nikapata ujauzito ambapo baada ya kujifungua mume wangu akaanza shida tena, akanifukuza, na kusema hanitaki, ila watoto wake atawatunza,
sasa tangu nitoke kwake, alileta matumizi kipindi cha mwanzo tu, baadae akaacha, nilipomfata na watoto wake (wote wa kiume) akasema eti yeye sio wanae, hawajui wote wawili, sasa mimi peke yangu kulea waotot wawili siwezi, maisha yangu yenyewe ya tabu, huyu mwingine anatakiwa kusoma, lakini hata pa kupata ada sipaoni,

naombeni ushauri wenu nifanyaje? nataka kwenda kule kwenye mashirika yakutetea haki za watoto na wanawake, lakini sijui hata pa kuanzia, nina hakika hawa ni watoto wake.sikuwa na mahusiano na mwanaume yeyoyote yule, na mimi na yeye tulikutana nae pale pale chuo kikuuu, kuna salon nilikuwa nafanya kazi ya salon ndipo tulipokutana. nishaurini mwenzenu nawahurumia wanangu

6 comments:

  1. Pole kwa yaliyokufika mpendwa. Nakushauri uonane na watu wa mashirika yanayoshughulikia haki za wanawake na watoto kwa mfano TAMWA au nenda ustawi wa jamii waelezee watakusaidia.Hata hivyo endelea kumtegemea Mungu atakushindia, muombe bila kuchoka kwani yeye ni mwingi wa huruma na fadhira.

    ReplyDelete
  2. Pole Sana Mdada! Kumbuka Mungu hamleti mtu Duniani kwa bahati mbaya. Hivyo basi hao watoto ndio faraja yako watakula unachokula.

    Kuhusu kusoma wapeleke shule za Msingi za kawaida walizosoma Maprofesor wote kumbuka hakuna Profesor aliyesoma International school, na shule hizo za kawaida hakuna ada ya shule wapeleke wakasome huko.......Kizito!!

    ReplyDelete
  3. Ikiidi mkapime DNA hapo ni mwisho wa yote

    ReplyDelete
  4. Pia jifunze kuishi maisha ya kumtegemea mungu
    na kama ulikuwa unashughuli ya kukuingizia kipato fanya tafutia watoto shule za kawaida shule hata za serikali wasome watafika tuu wengine tulipofika tumesoma shule za kawaida na maisha yetu yalikuwa ni mlezi mmoja yaani mama na tuliachwa saba na mmoja wa nje ya ndoa mshahara wa mama wa midewife umetusomehs secondary na course za hapa na pale leo hii tumesimama tunamaisha yetu tumeolewa na sio kama baba alikufa no aliamua tuu kutafuta binti leo anatuangalia kwa jicho la usuda, sasa dada najua maisha ni magumu lakini watoto wawili funga mkanda everything is possible under the sun.

    ReplyDelete
  5. Tafuta washenga nao pia kwani mlivyooana si kulikuwa na washenga wajaribu kumkalisha na kuongea naye usikie nao watasema nini na kushauri nini.

    ReplyDelete
  6. pole mpenzi wapeleke watoto wako shule za kawaida tu watakua na watasoma mungu yupo kwa ajili yetu

    ReplyDelete