Thursday, February 23, 2012


Wote twajua jinsi gani mama alivyo mtamu, hakuna kama mama jamani, ukiondokewa na mama yako, utalia na hutosahau ktk maisha yako, maana yeye ni kila kitu kwa mwana, kuna mdau mwenzetu aliondokewa na mama, na leo amemkumbuka san asana sana,
MIMI  VIOLET, NAKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AKUPE USHINDI, NGUVU, NA UJASIRI WA KUWEZA KULEA FAMILIA YENU THOUGH HUTOFIKIA KIWANGO CHAKE,
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE


KUMBU KUMBU

Ni miaka 23 sasa tangu umetutoka lakini sisi kama watoto wako pamoja na baba ulietuacha huku tunaona ni kama jana tu umeondoka maana umeenda kimwili lakini kiroho bado tupo nawe, na kamwe hatutaacha kukumbuka malezi yako bora!
Tukiwa kama familia (watoto wako pamoja na mumeo (baba)) daima hatuishi kukuombea DUA njema kila kukicha upate kupumzika kwa kwa amani huko uliko.
Ni matumaini yetu mungu anasikia dua zetu MAMA
Ni sis wanao wapendwa Mariam, Hussein, Salum, Mariam Hawa pamoja na Baba yetu (mumeo) Sheikh Suleiman haatuna la zaidi ila ni dua tunakuombea
INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAJIUN.


1 comment:

  1. poleni, mungu azidi kuwatunza, kama alivyosema violet, mama ni muhimu sana hapa duniani

    ReplyDelete