Monday, February 20, 2012

NAWASHWA SEHEMU ZA SIRI, NA KUTOA MAJI MAJI YASIYOTOA HARUFU, NIFANYAJE?

Habari yako Vio, mimi nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri na ninavimba hii sehemu ya kukojolea  na nashindwa kuelewa nifanye nini dada yangu,,kwani ninawashwa mpaka natoa majimaji na ute visivyokuwa na harufu na nilishaenda kwa dr akaniambia ni ugonjwa unaotibika akanipa dawa nikazitumia bikaa muda ila tatizo limejirudia tena na nakosa amani sijui nifanyaje mwenzako nisaidie

13 comments:

 1. huyo dada namshauri arudi hospitali ili apate tiba
  Milka Mjungu

  ReplyDelete
 2. sina utaalamu sana ila pia aangalie aina ya chupi anazozivaa wengine ngozi yao ni sensitive avae cotton na aachane na thong
  Anneth Kyejo

  ReplyDelete
 3. Namshauri arudi kwa wataalamu hosp.ila pia aangalie na aina ya chupi na usafi wake pia ni muhimu sana.
  Goldermier Kapya

  ReplyDelete
 4. aende kwa gynocologist akapate ushauri zaidi, yawezekana UTI coz uti nayo huwa inasumbua sana
  Ritha Nancy

  ReplyDelete
 5. akanunue ketroconazole inasaidia sana pole mwaya
  Habiba Mlawa

  ReplyDelete
 6. tatizo kujirudia yawezekana ni infection ambayo pia mwenza wake anayo kwa ushauri arudi hosp na partner wake wachekiwe na kutibiwa wote, yawezekana anapata matibabu vizuri tu but akifanya yale mambo yetu analetewa tena infection, wenzetui males wanaweza kua na infection na asiwe na symptom yoyote. kingn anachoweza kufanya ni kufua nguo zake zote za ndani kwa kaji ya moto au detol kuhakikisha vimelea vimeisha au aloweke na detol baada ya kufua cause inawezekana anatibiwa huku anatumia chupi yenye hivo vidudu tena na tena vinarotate tu
  Sara Phyn

  ReplyDelete
 7. Yawezekana itakuwa fungus,aende kwa dr ajieleze bila woga na pia apime mkojo waangalie infection iko kiasi gani maana kuna sindano huwa zinachomwa kulingana na hali ya ugonjwa pia kuna dawa ya kuongiza kwa bibi. Pia km Sara phyn alivyosema mwenzi wake pia akapime yawezekana yeye ndo source. Mpe pole mwambie inatibika hiyo.
  Jane Peter

  ReplyDelete
 8. Aangalie aina ya chupi anayovaa, na cku zake katika uvaaj wa PEDI namaansha anakaa mda gani mpaka kubadilisha PEDI. In short usafi wake wa huko kwa bibi.
  Clarita Teresia

  ReplyDelete
 9. namshauri aende hosp tena dalili alizonazo pia yawezekana ni fungus au veneral desease kwasababu ya hayo maji maji yanayotoka hko ili apate treatment vzr anatakiwa aende na mwenzie
  Assynath Thompson

  ReplyDelete
 10. but kiukweli ni vizuri aende kwa dr bingwa wa magonjwa ya wanawake akapimwe zaidi na kama ikiwezekana yeye na mwenzi wake wakapimwe wote coz na yeye anaweza kuwa source ya hilo tatizo kujirudia mf UTI ukitibiwa ukapona then ukaenda ku duu wakati mwenzio hajatibiwa ni lazima itakurudia tu so ni vyema wakachekiwe wote,mpe pole sana asijali atapona awahi mapema kabla tatizo halijawa kubwa.
  Rose David

  ReplyDelete
 11. pia chupi zake awe anazipiga pasi kama anazianika ndani au awe anazianika nje zipigwe na mwanga wa jua, na pia kama anatumia sabuni za kuosha huko chini zenye chemicals nyingi aache
  Ntukano Mtingele

  ReplyDelete
 12. Pia angalie anaweza akaanika chup ndan halafu haijakauka vzr yeye akavaa hyo pia c nzr kwa afya ya bibi huko.
  Clarita Teresia

  ReplyDelete
 13. awe anavaa chupi za cotton na kabla ya kuvaa awe anazipiga pasi, pia awe anazianika nje chupi zake. Ila pia nu vizuri ajarudi kwa dr,

  ReplyDelete