Wednesday, December 21, 2011

HATUJAFUNGA NDOA, AMESHAPUNGUZA MAPENZI KWANGU, TUKIFUNGA NDOA TUTAISHI KWA AMANI KWELI???


mimi ni msichana ambaye ninaishi na mwanaume japo hatujafunga ndoa ila tulilazimika kukaa wote baada ya mimi kushika mimba na sasa tuna mtoto.
tatizo langu ni kwamba huyu kaka hana tena mapenzi na mimi kama ilivyokuwa hapo mwanzo kwani hanijali, hanithamini, japo hela ya matumizi nyumbani anatoa kama kawaida ila yale mapenzi ya mtu na mkewe hana kabisa





Anajibu majibu ya kimkato tu! Kuongozana na mimi ni kama hajisikii, unakuta hata kwenda kanisani anatangulia, mimi ananiacha, yani kifupi amekuwa na tabia ambazo wala sizielewi 

mfano katika swala la mapenzi mimi nisipoanza kumuomba tufanye tendo la ndoa hata mwezi unaweza kupita bila yeye kuniambai chochote na mbaya zaidi ameshatoa mahari kwetu na mwakani tulikuwa tunatarajia tufunge ndoa.


 

sasa jamani kuna tutaishi kweli kwa staili hiii  kweli hapo au najindanganya tu mwenzenuuuuuuuuu. naombeni ushauri wenu wadau kabla sijaingia kwenye kifungo cha ndoa cha milele

.

7 comments:

  1. atakuwa keshapata mwanamke, anamzinguwa huyo, unafikiri wanaume wana maana?? mimi nakushauri, achana nae pamema, kabla hajakusumbua,

    ReplyDelete
  2. inawezekana kabisa wewe ni chanzo cha haya, coz kina mama wengi huwa wanajisahau sana wanapopata watoto, mapenzi yote huhamia kwa watoto wao, ndio maana waume wanafanya vitu vya aajbu

    ReplyDelete
  3. muombe mungu awe mshauri wako wa mwisho, kabla ya kuingia kwenye ndoa, maana maisha ya ndoa si ya kuchezea kabisa,pole dear, ni mbaya sana ukijuwa kuwa hupendwi, inaumiza mno, lakini pole, mungu akutie nguvu mpendwa

    ReplyDelete
  4. jamani wachangiaji tuwe tunafikiria kabla ya kukurupuka tu! na kumwambia aondoke, naugana na huyo aliesema kuwa ujichunguze wewe umekosea wapi, jichunguze kwanza wewe binafs, yawezekana umemkosea ndio maana ameamua kupunguza mapenziyake kwako, jirekebishe kwanza, au kama unaweza jaribu kukaa nae, muulize tatizo nini, muweke wazi akwambie tatizo ni nini, mbembeleze kwa upole na upendo hadi aseme unaweza jikuta ni kweli wewe ndiwe mwenye kosa
    anita

    ReplyDelete
  5. ongea nae, ujuwe tatizo ni nini, na kama mtaweza kulisolve, basi limalizeni yaishe, msipende kucomplain kwanza, malizeni matatizo mfunge ndoa, ila kama ni makubwa, basi amua moja tu! mwambie kama hawezi kubadilisha tabia yake, basi akuache, kila mtu afate hamsini zake

    ReplyDelete