Monday, December 12, 2011

HAKUNIAMBIA KAMA ANA MTOTO WAKATI TUKO WACHUMBA- AMESHANIOA NDIO ANASEMA ANA MTOTO NJE YA NDOA, NIFANYAJE??


Habari dada violet natumaini mzima , nina miaka 26, naomba ushauri nimeolewa miezi mitatu iliyopita, nimekuwa kwenye uhusiano na mume wangu mwaka mmoja na nusu kabla ya kufunga ndoa,

kinachonisababisha niombe ushuri ni hivi karibuni mume wangu kaniambia ana mtoto wa miaka saba jambo lililonifanya nishtuke sana, anaomba msamaha kwa kutokuniambia muda wote huo, nilimuamini sana,

sasa hili limenifanya nianze kutomuamini na roho inaniuma kwani sikutaka kuolewa na mtu mwenye mtoto, coz sitaki kuwa na mtoto wa kambo, ndoa yangu ni ya kikristo, sihitaji kumchukua mtoto kwani c kosa lake, lakini hili limeweka jeraha moyoni kiasi

mdau wako from
arusha




11 comments:

  1. Kwanza ,kabisa usi jilaumu kwa kuto kuambiwa.wewe tayari umesha anza kumjuwa mwenzi wako kwa upande mwingine, hasa kutokukuambia kuwa ana mtoto.hivyo juwa mmeo ni msiri. je kiukweli kabisa ina kusumbuwa yeye kuwa na mtoto mkubwa wa miaka saba,ninini hasa kinacho kusumbua hapo,ni mtoto au kutokuambiwa juu ya huyo mtoto?. mwisho hebu jifanye wewe unge kuwa yeye mumeo ungelichukuliaje swala hilo. ukiwa mkweli kwa nafsi yako ju ya swala hili halita kupa shida.atakuwa anasababu kuto kukuambia,ila tu kama imetokea basi mimi navyo ona kwa upande wako itakusaidia kumjuwa zaidi mumeo na kujiandaa kwa lolote baada ya hili la mtoto. pia kaeni chini mzungumze/mawasiliano ni muhimu, heri kakuambia sasa,kuliko inge chukua muda,hakuna wa kumaliza hoja yenu ni ninyi wawili kuelewana. pole sana .kaka s.

    ReplyDelete
  2. wala huna haja ya kuchukia au kujiskia vibaya, japo inauma, lakini ndio imeshatokea hivyo, jaribu kuukubali ukweli, kwamba mume wangu ana mtoto, basi, maana huna jinsi, kama unampenda huwezi kumwacha, na hata tukisema umwache, hutomwacha, maana ndoa za kikristo unazijua zilivyo committed, so cha kukushauri, kaa na mumeo, mueleze ulivyojisikia, then basi, no way out, but mh! wanaume jamani?? ah!

    ReplyDelete
  3. pole dada, usiachane nae, wewe mshukuru Mungu umejua mapema, usiwaze sana na istoshe ndoa yako bado changa sana, wewe mpende, muheshimu, naungana na huyo wa hapo juu, kwamba KUBALI UKWELI, itakusaidia
    pole mpenz wangu, nakuombe mungu akupe nguvu

    ReplyDelete
  4. hizo ndio ndoa za kibongo!! pole mwaya. ndoa bado changa tayari machungu yameshaanza.

    ReplyDelete
  5. mdau acha kunishangaza jambo dogo ivyo ushaweka jeraha moyoni ndoa ni kuvumiliana na kukubaliana kwa mapungufu yenu na pia mwanaume kukwambia baada ya ndoa inaonekana wewe ndo umesababisha iwe ivyo maybe ushawai ongea nae vibaya huhusu watoto wanje na kama jamaa alikupenda alijua akikwambia kakupoteza shukuru na omba sana MUNGU ingawa inauma na life liendelee mana mtoto mkubwa kuna wengine wameletewa watoto wa miezi after kuolewa.maisha ya sasa twaangalia uelewa wa mwanaume kwako perfect Gentlemen wamebakia kwenye tamthilia

    ReplyDelete
  6. usiachane nae, ila uwe makini nae, tena mdadisi sana, usikte ana mengine makubwa, au hata ana watoto wengine, anaogopa kusema, jua kabisa mumeo si mkweli, so ninachokushauri ni kwamba wala usimuache, wewe ishi nae ila uwe makini tu! na ndoa yenu bado changa sana, usikubali mtoto aje kwako, mwache akae huko huko, mradi unajua tu! na huduma mumeo aendelee kupeleka
    USHAURI
    WANAUME ZETU JAMANI, KUWENI WAKWELI KWA WENZI WENU, UONGO UNASAIDIA NINI??

    ReplyDelete
  7. inawezekana kabisa mumeo alijua utakataa akuoe ndio maana alikuficha, lakini maji yameshamwagika, huna budi kukubali ukweli, mi naona niungane na wadau, mtoto asivunje ndoa yenu, mpende mtoto na mume pia, mkiongozwa na mungu,
    ubarikiwe

    ReplyDelete
  8. Shukuru umedanganywa mtoto wenzio wanadanganywa na waume zao ni wazima kumbe wamesha kwa gonjwa la ukimwi siku nyingi wanakunywa dawa wake zao hawajui wakija kujua to late, mungu atusaidie kwa kweli

    ReplyDelete
  9. Yaoge maadamu uliyavulia nguo. Siyo mambo yote unaweza kuambiwa,mengine tunayakuta mbele ya safari.Kutakuwa na mengi mazito zaidi ya hilo.Mimi nadhani hilo ni jepesi wala usilishupalie mno.Mtoto huyo ana mama yake ya nini wewe kulalama?

    Ameishakuambia inatosha ni kuchuliana na kuendelea na maisha.Hata kama hutampenda huyo mtoto haitakusaidia.Utayaona mengi bibie.

    ReplyDelete
  10. Pole mdogo wangu, ila usikubali kukaa na huyo mtoto akae na mama yake kama yupo hai mwambie apeleke kila kitu ila usikae nae, watoto wa siku hizi akisha kusoma atakutesa mpaka ukome me yalinikuta ndio maana nakushauri hivyo hakikisha hukai na huyo mtoto ukikubali umechemka, MTOTO WA MWENZIO MKUBWA MWENZAKO!

    ReplyDelete
  11. Sioni sababu ya kupanic, huyo mwanaume umekuwa nae kwa mwaka mmoja na nusu na mtoto ana miaka 7 which means amempata huyo mtoto hata kabla hajakutana na wewe hapo hakuna tatizo kama alikuwa amempata ndani ya huu mwaka mmoja nusu uliokuwa nae kweli lingekuwa tatizo kubwa, pamoja na kwamba kosa lake ni kuto kukuambia toka awali japo pia inawezekana alihofia ungeweza kumuacha, take courage Mwombe Mungu mpokee mtoto wala usimnyanyase na maisha yataendelea tu.
    Kila la kheri

    ReplyDelete