Friday, April 27, 2012


Hallo
dada violeth pole na kaz ya kutushauri wanajamii.
Dada violeth mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28, nina boyfriend ambae ana mtoto mwenye mwaka mmoja na miezi nane.ila washaachana na huyo dada alozaa nae, mototo aliendelea kuishi na mama yakekwakuwa ni mdogo.

Sasa juz kati huyo dada kanipigia simu kupitia namba ya boyfriend wangu na kunieleza kuwa wapo wote moro, later nikancal huyo boyfriend na kuhoj kulikon akanambia mtoto anaumwa dats why yule mama mtoto kaenda huko moro .
nlimpigia tena kwa boyfiend wangu akapokea yule dada na kuniambai yupo kwa boyfriend wangu, nikamwomba niongee na mhusika akakata na kuniambia nisimsumbue mume wake. Basi later on nikampigia ma boyfriend na kumwambia yalojiri akanambia yule mwanamke kamfuata ofisini na mtoto kwa hiyo hakuona busara kumfukuza wakati ana mtoto wake. bac usiku alipofika bma boyfriend akanipigia simu na tukaongea wote watatu na boyfriend wangu akaprove mbele yetu wote kwamba hatoweza kuwa na yule dada na huyo dada akakubaliana na hali halisi na kwa mdomo wake akanambia kweli huyo kaka ananipenda sana mimi.
Mbaya zaidi Yule dada kaenda kwa wazazi wa boyfriend wangu Sasa bac Yule dada kapandikiza kule kijijini na kapandikiza maneno ya uongo kwa mama mkwe kiasi kwamba mama mkwe leo asubuhi kanipigia kupitia simu ya yule dada kanitukana matusi ya nguoni na kuniambia hataki kuniona wala kunisikia na huyo dada ananambia angekuwa hapendwi asingeenda kule kijijini.Ma boyfriend nimemcal ananambia hata yeye kishagombana na mama yake coz anataka kumchagulia mtu wa kumuoa. Huyo boyfriend wangu huwa anasema hata asiponioa mimi hataweza kumuoa yule dada coz hawatowezana.
sasa nifanyaje8 comments:

 1. Sasa bibie unataka sisi tukusaidie nini wakati mwenyewe unayaona kwa macho yako na kuyasikia yote kwa masikio yako? Ukiolewa na huyo jamaa hutakuwa na mama mkwe?Mimi nadhani unajiingiza mahali pagumu ambapo patakuuliza sana usipokuwa makini.Kama jamaa amezaa na huyo jamaa wewe unatafuta nini hapo?Kila siku ustasikia mtoto anumwa anaenda kukutana naye,si utaugua pressure bure? Wewe achana naye mapema,yani pamoja na sokomoko lote hilo uko gizani bado?Jamani kwani wanaume wameisha a ndo kukata tamaa ya maisha?

  ReplyDelete
 2. Deal na bwana ako..achana na hzo habari za huyo mwanamke, huyo mama mkwe mpe heshima yake,mpende kama mwanzo...siku mwanaume akitamka hakutaki au akifanya vitendo vizito vya kukuonyesha hakutaki then achana nae...hayo yote kwasasa ni majaribu tu..kama unampenda mpenzi wako then don let go so easly

  ReplyDelete
 3. dada we komaa tu,kwani we utaolewa na huyo mama mkwe.as long as jamaa anakupenda.hata huyo dada anafahamu kwamba jamaa anakupenda ndo maana anahangaika huku na huku mara apige simu mara mama mkwe.mara nyingi wamama huwa wana tabia za kuchagulia vijana wao wakwe ila mkionyesha msimamo mnapendana huyo dada atagive up,na mama mkwe akiona miaka inasogea na mtoto wake amengangania hapo,basi atajifunza kukupenda.kuwa mvumilivu mamii mapenzi yanahitaji uvumilivu.ningeshauri umwache jamaa kama tu angekuwa hajaonyesha msimamo.

  ReplyDelete
 4. mwambie huyo kaka akupe msimamo wake, usije ingia kwenye ndoa ukawa umepotea. Akuambie msimamo wakr kuhusu huyo mzazi mwenzie na kuhusu mama mkwe. Yeye kugombana na mama yake hakutombadilishia mzazi sababu akikuoa utaweza kudeal na mama mkwe

  ReplyDelete
 5. Afu kumwambia kuwa hata nisipokuoa wewe sitamuoa huyu dada ni utata. Inaonyesha hata wewe hajakufikilia kuwa my wife wake. Kwa nini asingesema nitakuoa wewe si yeye badala yake anasema (impliedly) kuna uwezekano sitawaoa wote.

  Pole bidada. Hata kama hujui kusoma picha je? Inaonyesha hata wewe si chaguo la huyo kijana, na ogopa sana wanaume wanaozalisha wanawake na kuwaacha unajuaje kama na wewe hutaachwa. Nina shemeji yangu ana watoto kila kona wadada wote wanazaa nae kwa kudhania atawaoa.

  Mnisamehe lakini mimi nilijiwekea principle, sitaki mwanaume mwenye mtoto maana najua sina moyo wa uvumilivu na nina wivu mbaya. Na kweli imekuwa. Sasa huna right ya kumkoromea mzazi wa mpenzi wako kwani wewe una nini nae; hata ukisema uolewe mtoto umemkuta hivyo yakubidi ufyate mkia; tofauti na wale ambao waume zao wanazaa nje, mtoto kawakuta.

  ReplyDelete
 6. Mhhhh achana nae kabisa najua itakuuma sana lakin msahahu ni mambo ya kawaida yanatokea personel siwez kabisa kuwa na mtu wa aina hiyo... Mbeleni utaumbuka bure......Mama Adidi

  ReplyDelete
 7. Achana nae. Huo ni mwanzo tu wa matatizo. Unaweza kuishi na ugomvi wa mama mkwe? Huyo mdada aliezaa na boyfriend wako hatakaa atulie awaone mnaendelea vizuri mkipendana, hata mkiwa mmeoana. Kila siku atakugombanisha wewe na mumeo na pia wewe na mama mkwe, na ghafla utajikuta unagombana na ukoo mzima. Utaweza?
  Life is too short, usijiingize kwenye matatizo. You dont need stress in your life. Sidhani kama hayo ndo maisha unayoyataka. Your husband kashindwa kuwa control both mama ake na huyo mwanamke, na ita affect sana relationship yenu. Run for your life and Get another man! Tena utoke ASAP, kuna mdada namfaham she was almost in a similar situation, now keshaachika!

  ReplyDelete
 8. Nyie wasichana wengine bwana mtabakia hivyo hivyo ma baby, ma sweety, ma honey, ma love, na wewe unasema ma boyfriend, soma alama za nyakati utapoteza muda wako bure na una 28yrs! utajistukia una 40yrs bado unasema ma boyfriend lol! NISIPO KUOA WEWE SIWEZI KUMUOA HUYU! jibu tosha tafuta hata msukuma mkokoteni kikubwa awe na mapenzi ya dhati

  ReplyDelete