Monday, March 26, 2012

SIKUMWAMBIA KUWA NINA MTOTO.. ANATAKA KUNIOA NA YUKO SERIOUS ,NIFANYAJE????


Habari yako dada violet, mimi ni dada wa miaka 25, nina mtoto wa miaka 4 yuko kwa mama Mtwara, hapa dar naishi peke yangu, sasa niilpata boyfriend .. tulipenda sana, lakini siku moja tukiwa katika maongezi yetu aliwahi kugusia kuwa akitaka kuoa anataka kuoa mtu asie na mtoto wakaanzishe familia yao  peke yao,,,
 niliogopa na kupata hofu ya kumwambia kuwa nina mtoto, mapenzi yaka grow sana na sasa anataka kwenda kujitambulisha nyumbani.. sasa nikimwambia nina mtoto si ataniacha??? Nifanyaje ili anielewe, uhusiano wetu una miaka 2 sasa, na always huwa anapenda kuinsist hicho kitu... najilaumu nafsi yangu kwa kutokuwa wazi from the begining... ushauri wenu please
7 comments:

 1. hata huyo jamaa inaelekea ni mgeni sana katika masuala ya wanawake kwani hata maziwa yako tu kama mimi ningejua tu kuwa umewahi kuzaa na kunyonyesha.Kama ndo ulikuwa mwanamke wa kwanza bila shaka hana uelewa wowote wa wanawake walizaa na ambao hawajazaa utajua tu.

  Kwa ushauri wangu tu bibie mwambie ukweli ili kama ni kukuacha akuache na kama ni kukukubali ulivyo akubali kwa sababu itakuwa mbaya mno iwapo ataambiwa na wengine au ikijatokea amebaini una mtoto.Hilo hutakuja ficha milele maana yule ni mtoto wako.Kama Mungu amekuandikia huyo bwana au mtu mwingine kukuoa basi utaolewa tu usiwe na hofu,bali ukweli daima ndo kitu muhimu.Usije ukagharimia arusi huku umeficha jambo halafu ndani ya siku mbili umeolewa siri inafichuka na kuzaa kizaazaa kingine.Muombe samahani kwamba hukuliweka hilo wazi mapema na ulikuwa na sababu ya kutosha tu kukaa kimya.

  ReplyDelete
 2. hahaha, sister, mie najua dawa ya mwanaume wa namna hiyo. mwambie kwa upole na uzuni unazani haumfai, Akikuliza kwanini nk.....? mwambie sababu wewe tayari unamtoto.

  vizuri atafute hasie na mtoto. Na muombe samahani kwa kuto mwambia, na muambie true uliogopa atakuacha, ndio maana haukusema, sababu ulijua yeye ataki mwenye mtoto.

  Alafu ondoka zako, kajitulize uko na mawazo. usimbembeleze akupende au awe na wewe.
  kuwa mstarabu, usigombane nae.

  Kama anakupenda atakutafuta, na hato kuacha, atakuelewa unavo jiskia.

  Na kama atakuacha basi hakukupenda kikweli. Na wewe wala haustairi kuwa na mwanamke kama huyo. pengine sio mpenzi wa watoto, hata watoto wake anaweza kuwakataa pia.  Ila jua kuna wanaume wengine wanasema tu kama wanataka kuoa hasie na mtoto. Ni maneno tu, ila akipata anae mpenda kweli haijarishi, kama ana mtoto au la.

  ReplyDelete
 3. Pole sana ndugu ila tambua hakuna kitu muhimu kama utulivu wa nafsi and ukweli unaokoa mwambie ukweli ajue moja kwani ni bora akuache hajakuoa kuliko kukuacha baada ya ndoa utakuwa umeiweka maisha yako dosari we mwambie dear NEXT TO ALLAH. kama ni Riski itakuwa tu ishallah na ALLAH akufanyie wepesi

  ReplyDelete
 4. Bibie safisha njia mapema ili uende kwa usalama na kwa uhakika zaidi kuliko mambo ya kubabaisha.Mpe ukweli huyo mtu wako aelewe.Usipomwambia ukweli ina maana huyo mtoto unamkana kwamba si wako na utapata madhara makubwa sana kisaikolojia ma kisosiosolojia pale ambapo utahitaji ukaribu na mwanao na malezi yake halafu huku huwezi kuyafanya hayo wazi kwa kuogopa mumeo asigundue.Fanya jambo mapema ili kieleweke mapema.Heri kuziba ufa kuliko kuja kujenga nyumba nzima ikibomoka.

  ReplyDelete
 5. Naitwa Salim Athuman, umri wangu ni 27, kwa imani ni Muislamu na kwa sasa ninaishi DSM.
  Nahitafuta msichana mwenye umri kati ya 22 hadi 25 na sifa kubwa awe Muislam, mpole na mwenye kujiheshimu na kujistiri(Mwenye kuvaa mavazi ya heshima).
  Itakuwa vizuri awe mweupe/ maji ya kunde, mrefu kiasi na mnene kiasi na mwenye elimu at least diploma.

  Dhumuni kubwa ni kuwa mchumba wangu kwa sasa na hatimaye Mungu akipenda tuje kufunga ndoa na kuishi pamoja
  hapo baadae. Kiukweli nimevumilia sana kuwa mwenyewe kwa kipindi chote nilichokuwa nasoma, japokuwa kwa sasa bado naendelea na elimu zaidi ila nahitaji na mimi kuwa na mwenza wangu. Tafadhali kama upo tayari kuwa nami naomba
  tuwasiliane.

  email yangu: salimathuman78@yahoo.com

  Namba ya simu itafuata baada ya kujuana vizuri

  ReplyDelete
 6. Hі all, heгe eveгy one is shaгing these κinԁs of knοwledge, therefoгe
  it's fastidious to read this webpage, and I used to go to see this weblog every day.

  Feel free to surf to my website ... titanium engagement rings

  ReplyDelete
 7. I used to be suggеsted thіѕ blοg νia
  mу cоusin. I'm no longer certain whether this post is written via him as nobody else know such specific about my problem. You are incredible! Thanks!

  Here is my page ... titanium engagement rings

  ReplyDelete