Tuesday, August 28, 2012

MPENZI WANGU AMENICHUKIA KISA.. NIMENUNUA KIWANJA NA KUFUNGUA DUKA LA COSMETICS, KWA JINA LANGU-- JE NILIKOSEA????

( MNAIKUMBUKA STORY HII?) Huyu dada aliwahi kuomba ushauri kwamba mchumba wake anamuignore sana, sometimes anamzimia hata simu akimuuliza why, anasema some times yuko buzy hataki usumbufu........ tukamshauri jinsi ya kufanya,,, amenijibu hivi,,,,

Aunt nashukuru kwa ushauri wako kweli mpenzi wangu alibadilika nakunipenda na iyo tabia yakuzima cm kaacha
 ila saivi lime jitokeza tatizo lingine ananipenda ila nahisi km yuko na mwanamke mwingine na saivi anasema kuwa nimemkera kisa nilifungua cosmetcs na nilinunua kiwanja na vyote hivyo nimeandika jina langu na lake hivyo kakasirika eti ckumshirikisha ila mimi niliona nisawa kuandika hivyo kwani nampenda km mchumba wangu ila kanibadilikia hataki kuongea na mimi nimejaribu kumuuliza km umefika mwisho wa penzi letu aniambie ila hataki kuwa muwazi nimeongea na dada yake amuulize km tatizo nini hataki kuongelea hayo mambo akiulizwa anae mwanamke mwingine anadai hana hebu nisaidie kuwa ananipenda kweli kwasababu nampenda sana isitoshe nimtu tumekaa nae myaka mingi na hatujawahi kugombana 
NISAIDIENI USHAURI  MWENZENU


 

2 comments:

  1. Hapo tu ndipo wanawake mnaniacha hoi eti "Nampenda sana na ni mtu tumekaa miaka hatujawahi kugmbana" sijui unazungumzia ugomvi wa namna gani wakati tumeambiwa sasa ni mara ya pili kuleta maada hapa ili usaidiwe.Mwanzoni ulikuwa humpati kwa simu alikuwa anakuzimia.Sasa anakuzimia mawasiliano kwa sababu umenunua kiwanja na kuanzisha duka kwa kuandikisha jina lako.sasa utawezaje kuishi na mtu wa nmna hiyo?Kwanza sasa hivi ni uchumba tu je ukishaolewa naye itakuwaje?Na imekuwaje unaishi na mwanaume miaka mingi bila ndoa ya kueleweka?unategemea nini?utazidi kuumizwa katika hali ya uchumba?Sina la kukushauri zaidi ya kusikitika kwa kuzeeshwa pasipo sababu.

    ReplyDelete
  2. mimi naona wewe dada una mpango wa kulia tu!!! kwanini uteseke hivyo na wakati huyo mtu hajakuoa??ww ushamuona mtu mwenyewe ana mapozi, leo hii unataka kumsujudia, CHAGUA KITU KIMOJA TU! ENDELEA NAE, UMNYENYEKEE AU ACHANA NAE UWE HURU,,, THE CHOICE IS YOURS

    ReplyDelete