Friday, December 31, 2010

I WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2011


Nawatakia wapenzi wangu wooote, heri ya mwaka mpya, Mungu  atulinde, atukumbatie, atubariki kila iitwapo leo, tukumbuke kumshukuru Mungu kwa yoote, hasa uzima tulionao, ukiangalia ni watu wengi sana walitamani na walipanga malengo meengi wayafanye mwaka 2010, lakini wamekufa, hawapo tena, 
tujiulize, sisi ni akina nani mbele za Mungu? tumempa nini Mungu hadi kutufikisha mwaka 2011??? hakuna tulichofanya isipokuwa ni kwa neema yake tu!

Tusianze mwaka tukiwa na vinyonyongo myoni mwetu juu ya maadui zetu, bali tuanze mwaka tukiwa na furaha na wooote, tusameheane tulipokosea na tulipokosewa pia,   tusihesabu makosa, tusiyaweke moyoni, tuachilie roho zetu ziwe nyepesi,  ili Mungu apate nafasi ya kutubariki, we are the Human being, kukosea/kukosewa ni kawaida kwa binadamu, haijalishi umeumzwa kiasi gani, haijalishi umeaibishwa kiasi gani, nafaham shida inakuja pale tunapojaribu kutafakari kile ulichokosewa, ambapo hata kama ni kidogo basi litakuwa kuuubwaaaaaa, NO. tusifanye hivyo, maana kisasi ni juu ya bwana.tusahau yooote yaliyotokea na tuanze mwaka mpya na MUNGU,

MUNGU AWABARIKI WOOOOTE, NA TUSHEREHEKEE MWAKA MPYA KWA FURAHA 
BYE 2010, & WELCOME 2011
NAWAPENDA SANA!!!!!!



Monday, December 27, 2010

MUME WANGU ANAKUNYWA POMBE HADI ANAJINYEA - NIMFANYAJE APUNGUZE AU AACHE KABISA???

Wadau nisaidieni, nimechoka maisha haya,
Mume wangu ni  ni mywaji mzuri sana wa pombe, nilimjua akiwa anakunywa hivyo kumbadilisha ilikuwa ngumu, lakini sasa hivi too much, anakunywa hadi anajinyea, wenzake wanamrudisha hoi, nimemsema mpaka nimekata tamaa, hivi atabadilika kweli?
Nimfanyaje aache pombe, maana hakuna siku anayolala bila kunywa pombe yani bora akose chai kuliko kukosa pombe, kwenye gari huwezi kukosa pombe, hadi jasho analotoa linanuka, akiingia chooni akitoka kila mtu hujua kaingia nani, siku zinavyokwenda anazidi kuchakaa,  namuonea hadi kinyaaa, kuna uwezekano wa kuacha pombe kweli?



Wednesday, December 22, 2010

MERY X MASS & HAPPY NEW YEAR TO ALL

 JALIA,  Says........
What a lovely x-mass  !!!!!!!!!!!!
love you all!!!!! mwaaaaaaaaaaaaaaaa




 JONENSIA Says,
I wish you mary x mass, and  wonderful new year,
Mungu ni mwaminifu kwao wamuombao, nami ni miongoni mwao, na nathibitisha kuwa amekuwa mwaminifu kwangu, nawapenda wooooote, tufurahie kwa furaha na ushindi tele


Jonensia & Eunice
WE LOVE YOUUUUUUUUUUUU

Monday, December 20, 2010

(NAKARIBISHA SALAMU ZA X-MASS NA MWAKA MPYA)


kama wapenda kutuma salamu za x-mass na mwaka mpya, tuma picha kupitia email yangu ambayo ni  violet.gerald@yahoo.com, nami bila hiyana nitakupaisha '' itanoga zaidi kama utatuma na ujumbe wako wa mwaka! ili ninapoipaisha picha yako naambatanisha na ujumbe wako,
 '' mshukuru Mungu kwa kukufikisha mwaka mwingine tena, muombe rehema zake, muombe akuwezeshe kukamilisha malengo yako mema yote uliyoshindwa kufanikisha 2010 ili 2011 yakamilike,
PEKE YETU HATUWEZI- TUNAHITATAJI  SANA MSAADA WA MUNGU!!
KARIBU


 
TYMON AND HIS FRIEND


&  TRACE WITH HER FRIEND


 ARE WISHING YOU A MARY X-MASS &
HAPPY NEW YEAR (2011)


2010  Umekuwa mwaka mwema sana kwa Familia yangu, (mume wangu, na watoto wangu), hadi tunapokaribia kuumaliza mwaka huu,  Namshukuru Mungu kwa kutupa uzima, na baraka zake tele alizoziachilia kwetu. na kutuweka pamoja hadi leo hii kama familia, Im feeling so proud with my  Lovely ''TWINS'', they make me happy always, may the blesses of the Lord be with them for the  all coming years.
WE  LOVE YOU ALL!!!





Wednesday, December 15, 2010

MKE WANGU HAPENDI NDUGU ZANGU HATA KIDOGO- NITAMFANYAJE AACHE TABIA HII


Wanawake wengine sijui wakoje jamani, inahusu nini kuchukia ndugu wa mumeo bila sababu ya msingi, au hata kama kuna hizo ''sababu  za msingi'' watu hukaa na kuongea mkayamaliza, sasa wewe unanuna hata kutembelewa hutembelewi lo! vibaya jamani, wanawake wa tabia hii mjirekebishe, raha kupendwa na ndugu wa pande zote, kupenda kuwa kivyakovyako ni dalili za uchoyo na ubinafsi wala haifai, kaka huyu amenisikitisha kweli,  soma hiyo!!!!!!!!
Nahitaji ushauri wenu sana,
Nilioa miaka miwili katika ndoa yangu, na sikugundua kama mke wangu anatabia hii, maana tulikuwa mbalimbali, tulipojuana tu! Yeye alikwenda South Africa kusoma, namimi nilikwenda UK, baada ya kumaliza, tulikutana Dar, (ambako ndio kwenye familia zetu) tukaanza maandalizi ya ndoa, na hatimae kuona, sikuweza kumchunguza tabia zake, nadhani nilifunikwa na upendo niliokuwa nao kwake.

Shida ni kwamba, mke huyu amechange  kiasi kwamba namuogopa hata mimi, ni mtu wa hasira sana, mtu wa kususa, some times anasusa hata kupanda gari yangu mimi, yuko radhi akapande daladala, sasa mimi maisha haya sijayazowea.

 Ndugu zangu wakija ni mkorofi, anaona kama anabanwa vile, wakati nina nyumba kubwa tu! Na ina nafasi, tena asilimia ya ndugu zangu wako busy na shughuri na familia zao, ila ikifika kipindi cha December wengi hupenda kuja kwangu, kubadilisha mazingira, yani wakifika mke wangu, anachelewa kurudi kwa makusudi tu! Na anaweza kuamka na kutoka bila hata kumsalimia mama yangu na ndugu zangu, yaweza pita hata siku tatu hajawaona.

Mama ni mtu mzima, aligundua hali hii, na akasema kuwa yeye atakuwa haji, ila akinimiss itabidi niwe naenda hata weekend kumsalimia, mama ananipenda sana, maana mimi ni mtoto wa kiume pekee kwa mama yangu,  nikisaidia kwetu nikimwambia tu kwamba nimetuma hela nyumbani, anaweza nuna hata siku nne, bila kusema na mimi, sometimes huwa natuma bila yeye kujuwa.
Nashangaa ndugu zake yeye hawaishi pale kwangu, leo atakuja huyu atakwambia ni mtoto  wa uncle yuko uingereza, kesho atakuja huyu atakwambia ni mtoto wa binamu, mimi huwa sijali 
 maana huwa naamini  wageni  wanaongeza riziki katika familia.

Sasa ndugu zangu wamesusa kuja kwangu, nami nilishazowea wageni, tuna mtoto mmoja tu, ana mwaka na miezi minne, cha ajabu hata ndugu zangu walioko Dar, wakitaka kuja kumchukuwa wakashinde nao kwao mke wangu huwakatalia na husingizia anaumwa.

Naumia sana, naombeni ushauri wenu, naogopa hata kuwaambia wazazi wake maana najuwa baada ya kumsema, nitanyamaziwa hata miezi, na mimi hali hii siipendi na wala sijaizowea, maana hadi huwa naogopa kuwahi kurudi nyumbani siku ambazo amekasirika, mtoto atapigwa na kufokewa kama mtu mzima, naweza kumtandika makofi, lakini nampenda ila nachukiwa tu! tabia zake? je anaweza kubadilika kweli???




Sunday, December 5, 2010

TULIACHANA NA MUME WANGU, AMENINYANG'ANYA WATOTO NA HATAKI HATA NIONGEE NAO-NISAIDIENI


Hello dada yangu violet,
nahitahiji ushauri wako na wadau pia, mimi niliolewa na mume ambae sikumpenda in 2001 and I was 17 years old, ila nililazimishwa na wazazi. Tukafunga ndoa, ndugu zake hawakufika sababu walikuwa hawanipendi, sikujali sana sababu yeye aliiahidi familia yangu ya kwamba atanilinda

tuzaa watoto 3, ila mda ulivyokwenda nae alianza kubadilika, akaanza kunipiga, anarudi usiku sana, Siku zingine harudi kabisa, ilibidi nimshirikishe sheikh mkuu matatizo yetu,  sheikh alimuita lakini hakwenda.

maisha ya ndoa yalinishinda, nikaamua kurudi kwetu mwaka 2008, alininyima talaka, niliamua kuondoka kwa lazima pamoja na wanangu, alhamdulillah nilipata kazi nzuri nawasomesha vizuri

Baada ya muda nikapata safari kwenda UK ndipo nilipo hadi sasa,  watoto nikawaacha nyumbani kwetu, sasa yule bwana alienda nyumbani akawachukua watoto 2. Na toka awachukue, amekata mawasiliano na mimi, hata kuwasiliana na wanangu siwezi.

Nawaombeni wadau na  dada violet mnisaidie, nipeni mbinu zozote, sababu sijui lakufanya kabisa, nimesha tuma watu wakaongee nae aniache niongee  na wanangu, lakini kawakatalia  cha ajabu anasema atawapiga hata hao ndugu zangu  kama wakirudi kwake tena.plz help me sister, I miss my babies so much



Tuesday, November 30, 2010

MUME WANGU HANISHIRIKISHI KWENYE MAAMUZI YAKE-NIFANYAJE

Mume wangu hanishirikishi kwenye maamuzi ya familia, naona tu mabadiliko yanafanyika ndani, lakini siambiwi chochote, kazi yangu kupokea tu! Sasa nimesikia tetesi kuwa anajenga huko kwao, lakini mimi mkewe wa ndoa sijui chochote, cha ajabu mama yake mzazi ndio anajua kila kitu, na huyu ni mume wangu wa ndoa, tuna miaka nane kwenye ndoa yetu, ukimuuliza anakuwa mkali sana,  tumezaa watoto wawili mpaka sasa.
Mimi nina kazi nzuri tu na nina mshahara mkubwa Ambao naweza kufanya vitu vya maana, nilivyokwisha vifanya hadi sasa nimejenga nyumba 2, moja ndio hii tunayoishi na mume wangu, sasa mwenzangu ndio kanibadilikia sana, hata simuelewi, je namimi nianze kufanya mambo kivyangu??? Lakini naona kushare Ideas ni nzuri zaid, wadau nisaidieni naona nimetegwa  sana, na pia kwanini asinihusishe mimi mkewe?? Kajenga baa kubwa tu kwao! Lakini mimi Nimejua nilipokwenda kwenye msiba wa kaka yake,  nilipomuuliza ilikuwa ugomvi sana.na hadi sasa hata sielewi nilichomkosea


Tuesday, November 23, 2010

MUME WANGU AMEOTA ANAFANYA MAPENZI NA MWANAMKE MWINGINE NINAEMFAHAMU- IMENICHANGANYA SANA HII, NAOMBA USHAURI WENU

Habari,
Mume wangu amenichanganya sana, siwezi hata kuwaza mambo mengine ya msingi, namuwaza yeye tu, nawaza nafika mwisho bila kupata suluhu, ndio maana ninaomba ushauri wenu
Hivi karibuni tukiwa njiani kwenda kazini, akaniambia kuwa ameota anafanya mapenzi na mwanamke mwingine, (alinitajia jina la huyo mwanamke, ni mtu ninaemfahamu vizuri sana, tena mimi na huyo mwanamke wala hatuivi, kutokana na kuwa na mdomo mchafu sana,
Sasa nashangaa na kujiuliza
1. Kwanini amuote yeye na asiniote mimi???
2. Kwanini aniambie ndoto ya kipuuzi kama hii?
3. Aliniambia ili iweje
4. Ingekuwa mimi ndio nimwambie yey enimeota nafanya mapenzi na mtu anemfahamu ingekuwaje?

Wadau naombeni ushauri wenu, ni jambo dogo bila kutafakari, ila ukilitafakari … inauma sana, ushauri please!!!!










Sunday, November 14, 2010

NIMEMZIDI UMRI MCHUMBA WANGU NAONA AIBU KUFUNGA NAE NDOA


 Habari ya kazi, mimi ni mpenzi sana wa blog yako, Inatusaidia sana mungu akubariki, mimi ni mama wa mtoto mmoja , nilitokea kuchukia wanaume wote pale nilipotendwa na nilikaa miaka mitatu bila ya kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote. Mwaka huu january niliingia kwenye uhusiano na kaka mmoja ambaye kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya harusi.

Kinachonifanya niombe ushauri ni kuhusu umri ninamzidi huyu mwanaume miaka miwili na ninaumbo kubwa sana naonekana mkubwa sana nimejalibu kujipunguza lakini wapi, ninakosa amani na ninapozungumza nae kumweleza mimi ni mkubwa kwake yeye hajali na anaona sawa tu.

Ninaogopa sana mwanzo wa uchumba alikuwa hataki kuniambia miaka yake sasa juzi nilipokuwa kwao ndio mama akawa anaelezea jinsi mwanae alivyomzaa mpaka kukuwa kwake. Niliumia sana dada natamani kusitisha maandalizi ya harusi lkn nashindwa maana next thursday ndio send off yangu. Jamani nifanyeje ninaumia sana moyoni.naombeni ushauri wenu wadau.

 
 
 
 

MAELEKEZO - JINSI YA KUTUMA MIKASA YENU KWENYE BLOG

Wapenzi wa blog yangu, kipindi cha nyuma niliwahi kuelekeza namna ya kutuma mikasa yenu ili kupata ushauri,(kwa wale wanaohitaji ushauri) sasa naona wengi mnatuma mikasa kwenye comments, ili inifikie kwa urahisi na niweze kuiedit, fanyeni hivi
1. andika mkasa wako woote, ila ni vizuri kufupisha kidogo (kuandika yale ya muhimu tu)
2. then tuma kwenye email yangu mimi, na sio kwenye comment, email yangu ni violet.gerald@yahoo.com
mkasa wako utanifikia, then mimi nitaurusha, ili upate kushauriwa, 

PAMOJA SANA!

Friday, November 12, 2010

SHEMEJI ANANITAKA, NAOGOPA KUMWAMBIA DADA, NI MKOROFI NA PIA HATANIAMINI

Dada, nakupongeza sana kwa kuwa na blog nzuri, inatusaidia sana, mungu akubariki, mimi nina shida, ninaishi na dada yangu ambae tumechangia baba, ila mama zetu ni tofauti, baba yetu alikufa, ndugu wakamuomba dada anichukuwe anisomeshe kozi yoyote ile,

Nikahamia kwa dada , sasa toka nimefika hapa, shemeji yangu ananifata sana, ananitaka kimapenzi, kwa nguvu na kunitishia kuwa anaenisomesha ni yeye na sio dada yangu, hivyo nimkubalie tufanye siri, Ananifata hadi chuoni, ananinyima raha kabisa, mchana ananifata anitoe luch, yani ah! ananisumbuwa sana na namshangaa amekuwa na wivu hata kwangu, hataki nipigiwe simu na mwanaume, anapekuwa simu yangu, sana, nimejitahidi kumkwepa lakini wapi

Dada yangu ana asili ya kiburi sana, ni mkali kias kwamba hata mama yake anamuogopa, na yeye ndie ameolewa na mwenye uwezo kidogo, hivyo wote wanamtegemea yeye, sasa naogopa kumwambia tabia za mumewe,  maana najua kabisa hatoniamini, na atanifukuza nitashindwa kusoma,,

Ninawaza niwaambie watu wazima wamwambie dada, lakini nina uhakika 100% dada hatoniamini, maana hupenda kusemasema kuwa, akiskia mtu yuko na mumewe, yeye hatadili na mumewe atadili na yule anaemchukulia mumewe, sasa mimi nahofia kukosa masomo yangu, maan shemeji mwenyewe anamjua mkewe alivyo, na kuna siku aliniambia unafikiri ukimwambia dada yako ndio atanifanya nini? Acha ujinga wewe, hutamani maisha ya dada yako, wewe nipe uone ntakavyokupa maisha mazuri,
nakosa raha kabisa, nisaidieni kwa ushauri wadau

nifanye nini mimi??? Dada usiirushe email yangu please!!!





Tuesday, November 9, 2010

NILIBADILI DINI NIKAOLEWA NA MUISLAM, BAADA YA NDOA NILIRUDI KWENYE UKRISTO, MUME WANGU AMEFARIKI, JE NATAKIWA KUKAA EDA???????


Habari ya kazi dada , mimi ni mpenzi mzuri sana wa blog yako, Dada nataka unisaidie mimi ni mkristo, nilibadili dini na kuolewa na muuislam  mwaka 2006 nina watoto 2 katika muda wote huo amani  kwenye ndoa yangu ilikuwepo

Lakini  mwaka 2008 mume wangu alianza  mahusiano na mwanamke mwingine  na kuamua kuzaa nje ya ndoa,  na hapo ndipo amani, na mapenzi vilikwisha,.

Sikuyapenda maisha yale hivyo nikaona bora nitafute njia ya kumrudisha  mume  wangu katika hali ya furaha na amani kama mwanzo,  nilirudi kwenye imani yangu ya ukristo na nilianza kwenda katika maombi kwa ajili ya kumuombea mume wangu, na kwakweli niliona mabadiliko na alianza kurekebishika

Lakini baada ya muda mume wangu alifarik. Kwa kweli niliumia sana  kumpoteza  mume wangu,  Sasa je  natakiwa kukaa eda? Hiyo eda ikoje? Au kwakuwa nilirudi kwenye ukristo haina haja tena ya kukaa eda,

Nisaidieni wadau



Tuesday, November 2, 2010

NINA MAKOVU SANA KWENYE MIGUU YANGU- YANANINYIMA RAHA, NIFANYE NINI?

Tunapozungumzia urembo, hatuwezi kuacha kugusia suala zima la mvuto kwanza, haswa kwa kina dada, na hasa hasa kwa upande wa ngozi, iwe nyororo, ing'are ivutie zaidi bila kujali wewe ni mweusi au mweupe, mpango mzima ni MVUTO,  sasa hebu tumsaidie mwenzetu huyu. 


mimi ni mdada mzuri na mungu kanijalia kwa kweli namshukuru mungu kwa kuniumba hivi. Lakini nina tatizo moja tu linalonisumbua...nina makovu sana miguuuni, yani mengi sana, na yananinyima raha kabisa...nimeshajaribu vitu vingi lakini wapi, hayapungui wala kuisha. nimetumia beauty cosmetics lakini yanashine tu!

naomba msaada.  lakini nilivyokuwa mdogo nilikuwa mtundu kupindukia sasa utundu unanicost na vidonda na makovu naomba msaada wako na wengine mnaosoma blog hii kama mnajua dawa naomba mnisaidie.

ASANTENI