Monday, March 29, 2010

BAADA YA KUSOMA SAANA, JANA JIONI NILITOKA NIKAKUTANA NA........

Kama ukihesabu vizuri kuna watu 8 kwenye BODA BODA hii.


MSIONE KIMYA WAPENDWA

Niko kwenye Mitihani wala sijawatupa, masomo yemenibananisha sana. Tupo pamoja....

Monday, March 22, 2010

RANGI GANI YA GAUNI LA BIHARUSI INAFAA KUVALIWA SIKU YA HARUSI?

Nimekuwa nikuhuduria sherehe za harusi kwa miaka mingi sana na hata yangu pia nilikuwa muhusika. Ni siku watu huwa na furaha na wanapendeza sana kwa mavazi maalum yaliyoandaliwa kwa siku maaluum pia. Lakini kuna jambo nahitaji kujifunza na kuwafunza na wengine ambao pia hawafahamu kama mimi. Huwa najiuliza :Je ni rangi gani ya SHELA inatakiwa ivaliwe na BIHARUSI gani? Hii sina maana ya kuwa ni mweupe/maji yakunde au mtanzania harisi/mweuzi. Ok ina weza kuwa point ila point yangu ni hii. Wanawake anayeolewa akiwa mwanamwali/bikira nasikia ndio anatakiwa avae SHELA jeupe peee na mwanamke ambaye si mwanamwari avae rangi yoyote apendayo.  Hapa mimi bado sijawekwa sawa kabisaa na bado sijafumbua jibu kwanini iwe hivi? Naamini kunawenye upeo mkubwa juu ya hili watatufunza wooote. Naomba maoni yenu.



Wednesday, March 17, 2010

NILIKUWA MZIMA, NILIPATA ULEMAVU WAKATI NAJIFUNGUA-MUME WANGU HANITAKI TENA

Taarifa ya Mama huyu imenisikitisha sana, imenitoa machozi, kuna watu wanapata shida sana jamani, tumsaidie kwa mawazo, ajuwe nini cha kufanya, inaumiza sana.

Habari yako mdogo wangu Violet, naandika kwa uchungu sana, moyo wangu unaniuma na machozi yananimwagika. Maana sina thamani ya kuishi kama binadamu wengine, naamini nilizaliwa kwa bahati mbaya, Naona bora hata ningekufa nilipozaliwa tu kama alivyokufa mwanangu. alienipa matatizo

Miaka nane iliyopita nikiwa chuoni Tabora, nilizaa na baba mmoja, baada ya kutoka chuo tukaamua kuishi pamoja kwa makubaliano, mtoto akuwe kidogo ndio tubariki ndoa, but since there tukawa busy na kuendelea kufurahia maisha yale, hatukuwa interested tena na kufunga ndoa, (ni kosa ambalo nakubali nililifanya) tulikuwa na maisha ya kawaida sana, ila kwenye upendo hata kama kuna shida huwezi kuona karaha sana, upendo unafunika kila kitu, Nikiwa na Yule baba tulikuwa tumepanga, badae tukajenga kwetu huku Shinyanga. Tukahamia hapa, akanifungulia biashara, nikawa nafuga, Catering, grocery, mambo yakawa safi kabisa,

Mwaka juzi nilipata mimba, tukakubaliana kabisa nizae, na alinihudumia sana hadi naenda kujifungua, nilipofika hospitali wakati najifungua nilipata kifafa cha mimba, nilizaa mtoto ambae alikaa siku tatu akafariki, mwanangu alikuwa wa kike, wakwanza ni wa kiume, niliumia sana,

Kitu ambacho sikielewi hadi sasa, nikwamba baada ya mwanangu kufariki, nilikuwa bado niko hospitali, siku ya nne nikawa siwezi kuamka, yani nikikaa tu miguu haisogei kwenda kokote, ikawa inajaa maji tu, na sehemu ya kiunoni nikawa sihisi chochotekile, nilijua nia maradhi tu na yatakwisha, lakini siku zina kwenda, ikabidi hospitali wanipatie wheel Chair, ili kunisogeza

Nimeumiasana, maana mume wangu amebadilika ghafla, kipnindi cha mwanzo alikuwa ananipendapenda, lakini ss ananichukia ile direct, miradi amempa dada yake ndie awe msimamizi, anasema mimi siwezi, nilijuwa nitapata support yake, roho inauma sana, Napata support toka kwa mwanangu James, nampenda mwanangu, yeye ndie atake nizika,

Kuna watu walinishauri nirudi kwetu, maana ilifikia kipindi akawa ananikashfu, anasema mm ni mzigo, kwanza hatuna vyeti vya ndoa, nimwachie mwanae niondoke, sasa mimi nitaenda wapi na hali hii jamani? Bila yeye kutaka nizae tena ningepata ulemavu huu, Dunia imeniangukia jamani, sina wa kunitetea, mama alishakufa zamani, baba yangu ni mgonjwa nae alikuwa ananitegemea mimi,

Tumechuma mali nyingi sana na baba James, nilimwambia basi nipe nyumba moja(maana ziko tatu) na mtaji kidogo kasha mimi nikakae huko na mwanangu, nitatafuta mtu atakuwa ananisaidia kusimami vibiashara vyangu, anasema atanipa kwa misingi ipi, anasema eti karibia nakufa, hizo mali nitaziharibu tu!, anatamani nife siku yeyote ile anaona kama namchelewesha, inauma sana violet

Kuna dada mmoja , alinipa jina la blogu yako, akanieleza ilivyo, nikaona namimi niandike ili nipatiwe ushauri, nifanye nini? Natamani hata kujiua, lakini moyo unagoma kufanya hivyo, nisaidieni mwenzenu.




Sunday, March 14, 2010

HAPPY BIRTHDAY MY TWINS (TYMON & TRACE)

This saturday ilikuwa ni birthday ya watoto wangu, wamefikisha miaka minne, hahahaaaaaaaaaa, nimekuza jamani lo! nikiwatazama narudisha sifa kwa mwenyezi Mungu, nikiangalia mapito niliyoyapita toka nilivyowazaa, hadi sasa wamekuwa hivi, huwa sometimes siamini kabisa. (4 years now) Namuomba Mungu awape afya njema, awakuze wanangu
Huyu ndie Binti yangu (kurwa - TRACE)

Na huyu ndie Kijana wangu  (Doto - TYMON)

Dadaa kaweka pozi, we!

kama kawaida, haiwi birthday bila kuwepo keki, hii ni ya Trace

Nahii ni ya Tymon, was simple but fun!

walizma mishumaa, kwa pamoja

Na kila mtu alikata keke yake kumlisha mwenzie, hahaaaaaa raha jamani da!

Mh! kazi ipo hapa, huyu trace hizi pozi sijui anazitoa wapi, du!

hawakuwa wachoyo, waliwaalika na wenzao, atleast wawaimbie
(asieimba hali keki, aseimba haliiiiiiiiii)

At the end, nilipata picha moja na wanangu ya ukumbusho, mh! pozi za picha ndio sina kabisa yani, lo!
all in all, tulimaliza salama kabisa, Naomba mwenyezi Mungu awape maisha marefu kabisa, awalinde, awatangulie kwa kila kitu, wakafanyike baraka kwa kila mtu, akawaepushie yote yaliyo mabaya, na kuweka rehema nyingi juu yao, (ASANTE MWENYEZI MUNGU KWA ZAWADI HII)
STAY BLESSED MY LOVELY TWINS


.

Saturday, March 13, 2010

MAAUMIZI YA BINAFSI YA KUFANYA KABLA HUJAAMUA KUOLEWA

Tuliangalia namna ya kuchagua mchumba, na sasa tunangalia namna ya kufanya maamuzi ambayo yatakupunguzia stress ndani ya ndoa, kwakuwa utakuwa umefanya maamuzi sahihi toka moyoni na wala hukukurupuka tu kuamua kufunga ndoa.

Remember that marriage is a holy union, so do not take into it, anything that is unclean or indecent. What do I mean by unclean? Read on. Before saying, “yes I do”, make sure that:

1. Hakuna mtu mwingine uliahidiana nae kuoana.? isije kuwa ulikuwa na mchumba huku una mwingine tena, at the end of the day, inakuwa aibu kwako, so you hv to think about it, na kama alikuwepo ni wewe sasa kufanya maamuzi sahihi, usifunge ndoa huku kunamtu umempromise ndoa, ni bora umwambie tu kwamba haiwezekani kwa sababu hizi na hizi na hizi, ili awe clear on that na wewe uwe huru coz ukweli humuweka mtu huru.

2. Ulishawahi kuolewa  mkaachana?, je  ulisha wahi kuolewa before? na kama mliachana, na umeamua kuolewa tea, huuyo anaetaka kukuoa anafahamu kwamba wewe ulishawahi kuolewa? ni vizuri akatambua hili, na kumuweka wazi yule anaetaka kukuoa.

3.Umekubali kuwa chini ya uongozi mwingine (uko tayari kufata sheria)?  Lazima ukubaliane na akili yako, kama utakuwa teyari kupunguza ikiwezekana kuacha kabisa baadhi ya tabia zako, kama ulikuwa kicheche, ndio uache utulie na mumeo, kama ulikuwa kiburi, ndio uache, kama ilikuwa huru sana kujirusha kwingi, uache, lazima ukubali vitu hivi, kwanza, na kama utaona huwez i kuacha, basi ujuwe ndoa itakushinda, hakuna mwanume anaependa kudharauliwa na mkewe, hakuana mwanaume anaependa mkewe amletee kiburi, ndio wale kila siku wanakula kibano. hivyo ni lazima uache, ufate anachotaka mume wako, kama hataki vimini basi ndio ujiandae kuvaa mavazi marefu, lakini uende ukijua utakuwa chini ya sheria, hutojiongoza kama mwanzo, na ni lazima KUTII

4. Kwanini unataka kuolewa? ni swali la kujiuliza wewe binafsi, na nilazima ujuwe jibu lake, kuna sababu nyingi, sasa wewe jiulize unataka kuolewa kwakuwa ni fassion kuwa namume, au kwakuwa anapesa nyingi, au kwa kuwa ni handsome, au kwakuwa unampenda? au kuwa unataka kupata watoto ndani ya ndoa? au kwakuwa umri umeenda sasa unataka tu uolewe tu? jibu unalo wewe uliye under someone. nalo ni la kufikiria pia, mfano mimi najua kwanini niliamua kuolewa,

5.Wazazi wa pande zote wamekubaliana na maamuzi yenu? mtu anaweza sema kwamba usijali hta wazazi wasipokupenda, hii ni mbaya sana, wazazi ni miungu wa pili duniani, na wanabaraka zao ndani ya ndoa, utajisikiaje utakapoolewa halafu wazazi wa mumeo wasikupende? ukose suppot upande wake, hawakutembelei, wanakuombea mabaya tu!? ni rahisi kusema hakuna shida, lakini kwa wanaoface shida hizi, hawana raha kabisa, kwakuwa baba/mama (wakwe ) hawakutaka, so hapa kazi inakuwa kwa mume kukaa na kuwauliza wazazi wakupe sababu zinazofanya wakukatalie kuoa binti fulani, kuna sababu zinaweza kuwa za msingi, labda kama wazazi wanafahamina na kutofauti kubwa kati yao, hakuna kinachoshindikana, kama umegundua wazazi wa mwenzio hawakupendi, ni vizuri kumwambia mchumba wako nahisi hivi, then yeye atakwambia, kabla hata hujaingia kwenye ndoa, ujuwe tabia zao hata kidogo tu, ni watu wakarimu? wana upendo kweli? au ni wakorofi? wengi huwa tunalisahau ili, hadi tukishaolewa, hilo timbwili lake, shughuri tupu!. so ni vizuri kuangalia hili.
mengine wadau wataongezea, (ZAIDI MUNGU ATUSAIDIE)





Thursday, March 11, 2010

HOW TO CHOOSE A GOOD HUSBUND? (KWA AMBAO HAMJAOLEWA) THIS IS SPECIAL FOR YOU!

Ni vizuri kabla mtu hujaolewa, ukakaa ukafikiria, ni mume wa aina gani atakufaa, madhaifu yako unayajua wewe mwenyewe, kila mtu ameumbiwa wake, kuna wanawake wakorofi kupita kiasi, yani hivyo ndio walivyo, you cant change their behaviour na wanajijua kabisa kuwa ni wakorofi, na kuna wanaume ni wakali kupita kiasi, sasa niambie wanapooana wawili hawa, huko ndani nini kitaendelea? hivyo ni vizuri kufikir ni mwanaume wa aina ipi utaweza kuishi nae kabla hujakurupuka kufunga ndoa,
Neno ndoa kama nilijuavyo mimi ni Nyumbani Daima Ombeni Amani , sasa kama wote mtaamua kuoana mabaunsa amani itatoka wapi? (THINK TWICE)

Ndoa ni tamu jamani asikwambie mtu, ila some time mh! panakuwa parefu sana, kama wote mtataka kuwa juu,  naomba niwashauri wadogo/wakubwa zangu ambao hamjaolewa, niwamegeeni kile ninachokiona mimi kitawafaa ktk harakati za kutaka kujua sifa za mume atakaekufaa, zipo nyingi, zingine wadau mtaziongezea.

1. lazima utambuwe, ndoa ni maamuzi ya kutoka ndani ya moyo wa mtu mmoja. (wewe tu!) ukisha kubaliana na maamuzi yako, ndio unayawasilisha kwa yule ambae unaona atakufaa ili myaunge kiwe kitu kimoja.(ndoa sio lele mama, usione raha kuvaa shela na kurundika pete mkononi, kama  usipojipanga sawa, utajuta)

2.katika maisha ya uchumba, vingi sana vinatokea, vikwazo lazima vitakuwepo, sasa je unavyomuangalia ni mwepesi wa kusamehe, na kusahau? au ni yule mwenye gubu, kosa umefanya leo lakini kila mkipishana analikumbushia?

3. Angalia, ni mtu anaekujali? anakusikiliza? anashaurika? kuna wanaume wengine akisema yeye basi na ukurasa umegungwa, ''No discussion'' hata kama anakosea, hataki kuambiwa, (muhimu kulitazama hili katika uchumba wenu)

4.  Anakupenda kweli? hana tamaa? maana kuna wenawake wengine huwa wanaforce ndoa, mradi tu avae shela atujaze ukumbini tumuone alivyopendeza, kumbe mwanaume wala hakuwa teyari kumuoa, baada ya mwaka mmoja tu! anaanza, najuta kuolewa mimi, wakati alitaka mwenyewe, (fikiria hili pia)

5. Kila binadamu ana mapungufu na madhaifu yake, na kila mwanadamu ameumbiwa wa kufanana nae, ndio maana ndoa ya mke mpole na mume mkali, zinaweza kudumu sana, au ndoa ya mume mpole na mke mkali zinadumu sana, ni kwakuwa kila mmoja amecoup na mwenzie, anajua hapa kapanda sana leo, ngoja mimi nishuke, (yanaisha) na ndoa za wote wanataka kuwa waelevu kila siku mingumi ndani, - sasa chunguza kwa mchumba wako, jitazame na wewe, mnaweza kuvumiliana tabia zenu?
point hizi tano, ni za kwangu mimi ninazoona ni kubwa kuzitazama, zingine wataongezea wachangiaji, hii itasaidia kupunguza matatizo ya ndoa zetu za sasa hivi,  

 next time nitawaambia, kabla hujaingia kwenye ndoa unatakiwa kufanya maamuzi gani ya binafsi, yakwako mwenyewe bila kumshirikisha mtu!




Tuesday, March 9, 2010

WAPENDWA NIMEBADILISHA EMAIL ADRESS

Wapenzi wote mlionitumia mikasa yenu ya kuhusiana na mapenzi, na ninyi ambao mtahitaji kutuma, kuanzia sasa nimebadilisha email adress yangu,BADALA YA KUWA  viot3fem@yahoo.co.uk imekuwa violet.gerald@yahoo.com. SO kuanzia sasa hivi mtumie hii,
Karibuni

 

NIMEKUBALI KUFUATA USHAURI WENU- LAKINI NITAANZAJE KUMUACHA??

(Nashukuru kwa kuparticipate katika blog yangu, Mungu awabariki, pia mawazo na michango yenu ni vya thamani sana, maana vinasaidia watu, na kufanya wawe strong zaidi, sasa kuna hii issue jamani, huyu dada niliepost mkasa wake mara ya mwisho, amenitumia ujumbe, ambao kiukweli, mimi peke yangu siwezi kumshauri, anahitaji ushauri zaidi toka kwenu, kwakuwa tumeshauri, basi ni vizuri pia tukamsaidia kumpatia mbinu ya kufanya ili kumtema huyo mkaka)

UJUMBE
nashukuru sana kwa ushauri wako na pia kwa wadau wa blog yako, namwomba Mungu anisaidie, Maana hapa nililipo hata  ada ya shule ninayosoma analipa yeye bado nusu lakin kutokana na ushauri  nimeamua mwenyewe kumuacha namwomba mungu anifanyie njia  ingine ya kupata ada ya kumalizia, maana mshahara wangu ni mdogo. Dear naomba niambie nifanyeje jinsi ya kumwacha nimwambie live tu! au nitumie simu? maana sina hata ugomvi nae,  japo wakati mwingine huwa naamka hata usiku nalia sana, maana alikuwa akitusaidia sana mimi na mwanangu, nimeanza kumchunia, hanielewi na ananishangaa tu! hata mwanangu pia ananiuliza  mama siku hizi mbona uncle haji nyumbani - msimamo nilionao ni kuachana naye no way, nimefikiri sana ila sijajua jinsi ya kufanya. Asante sana violet, nakupenda
  
 
Jamani, ujumbe huo hapo wapenzi wangu, tumemshauri mwenzetu kutokana na matatizo aliyonayo, wengie tumemshauri aachane nae, nae amekubali kufuata ushauri wetu, sasa ameniuliza, kama ambavyo mmesoma hapo juu, kwamba aanzaje kuachana nae? haelewewi maana hajagombana nae, isitoshe ndie anaewasaidia mahitaji, na ndie anaemsomesha, hivyo sehemu kubwa ya msaada wake ameiweka kwa huyo kaka,
JAMANI HII ISUE NI NZITO, si masikhara, mimi peke yangu kumshauri nimemshauri, naombeni na nyie wanawake wenzangu mumsaidie, kumpatia mawazo, afanye nini, je amuite amwambie, amchunie tu,  au awe anampotezeapotezea, yani hata sijapata jibu lililosimama, hebu tusaidiane wapenzi,
INSHORT YUKO KWENYE WAKATI MGUMU SANA!



Friday, March 5, 2010

NILIACHANA NA MUME WANGU, NIMEPATA MWINGINE ANATAKA KUNIOA- WANASEMA ANA UKIMWI.


Hi violet, kama nilivyokwisha kukueleza. Mm ni mama wa mtoto mmoja niliolewa miaka 13 iliyopita ndoa ya kikristo, niliishi na huyo mume kwa miaka 5 ndipo alipopata mwanamke mwingine na kuhama nyumbani kwenda kuishi nae.

Nafanya kazi kwenye ofisi moja hivi, Sasa hapa kazini nimepata boyfriend ambaye amefiwa na mke wake, ana watoto 5, kati ya ha 1 alizaa na dada mmoja ambaye hakumuoa, wapili ni wa mwanamke aliyefariki ambaye alizaaga na mwanaume mwingine ndo kamuachia anamlea,wengine ni wamke wake walieachana.

tatizo liko hapa! watu wanasema huyu kaka kaathirika manake amefiwa na wanawake 2 kabla ya huyo wa 1ambaye amezaa naye watoto 2 naye alifariki. Nikamshauri tukapime akakubali tukapima mara 3 angaza wote salama lakini sijui why roho yangu inataka tuende tukachek tena hosp ingine naye amekubali,

kwnn tuliamua kufanya hivyo kwakuwa anataka kunioa. Ila sasa huyo mwanamke wake aliyezaa naye ambaye yuko hai ni mkorofi kiasi kunitisha. Pia baada ya kurumbana sana akaniambia kuwa mke wake wa 2 alikufa kwa HIV na mtoto wao mdogo ameathirika. Violet! niko njia panda kwani nampenda ingawa ana madhaifu yake mengine lakini sometimes nasita kukubali ndoa naye, pia nimepata tetesi kuwa huyu mtoto mdogo ameathirika, sasa niko njia panda yani hata sielewi cha kufanya, nishaurini jamani ili nipate njia ya kutokea maana sielewi nianzie wapi niishie wapi.

ni mengi mpenzi wangu nashindwa kuandika yote.  kwa ufupi huu naomba wanablog wanisaidie kwa ushauri
asante na kazi njema





Wednesday, March 3, 2010

NINA MCHUMBA TUNAPENDANA SANA, ILA TUMETOFAUTIANA DINI - WAZAZI HAWATAKI NIFANYAJE


Habari dada Violeth, Mimi ni bint wa miaka 26 nina mpenzi ambaye tumekuwa pamoja kwa miaka 2 na miezi 3 sasa, tunapenda sana, tatizo mimi ni mkristo na yeye ni mwisilam, alimwambia mama yake kuwa anampenzi mkristo, mama yake amepinga hilo amesema anataka binti aliyekulia kwenye mahadili ya kislam, hataki kusikia kabisa ukristo, na mimi binafsi siko tayari kubadili dini, niliongea na mama yangu hakupinga ila aliniambia niendelee kumuomba mungu anionyeshe kama kweli ni yeye aliyenipangia.

sitaki kuishi bila ndoa maana maisha haya hayana heshima? napia raha ya ndoa wazazi wote waridhie, mpenzi wangu hajui la kufanya hadi sasa, niliwahi kumjaribu nikamwambia tuachane kila mtu akatafute wa dini yake, hataki kuachana na mimi kabisa, ananipenda sana, na kwangu pia inakuwa vigumu kuachana na yeye,
kwakweli tupo pagumu ukizingatia tunaheshimiana sana na tunaelewana. kwasasa tuko masomoni nje ya nchi na wazazi wetu wote wapo tanzania, nikifikiria najisikia vibaya sababu sijui nini mwisho wetu, na niliamua kuwa na yeye sababu nilimjua tangia tuko secondary tulisoma shule moja na badae tukakutana tena collage tanzania huko kote hatukuwa pamoja na tumekuja kukutana tena huku,ndio akaniomba tuwe pamoja. naogopa asije akaniacha kwenye mtaa badae sababu ya wazazi, naomba ushauri wenu nifanye nini, nakosa raha juu ya hili, najuwa kuna wakubwa wangu walipitia tatizo kama hili na wakafanikiwa kulitatua, naombeni mnishauri na mimi mdogo wenu, sijui cha kufanya, nina wakati mgumu sana?






Monday, March 1, 2010

MUME WANGU ANATAKA STYLE ZA MAPENZI ZA AJABU-ZINANIUMIZA


Hujambo violet, mimi ni mama wa miaka 36, nina watoto watatu, nina miaka tisa kwenye ndoa, tulipoona na mume wangu tulikuwa tukifanya mapenzi style za kawaida tu, tunabadili style lakini ni zile za kawaida

Umefika miezi mwala sasa mume wangu amebadilika sana, yani hatulii yani mimi nayeye hatukai nusu saa bila ugomvi, kitu kidogo tu, hasira kwangu na anapeleka hadi kwa watoto wangu, yani hadi wanamuogopa sasa hivi, wakimuona tu! Wote wanaenda kulala,


Hadi sasa nahisi mume wangu anamwanamke nje, tena ni Malaya kabisa, maana violet mdogo wangu, mume huyu huwa nakaa namfikiria naona kama wamenirogea vile, hajui kubembeleza kwenye mapenzi, yeye ni kuamrisha tu, tofauti na zamani, hata mimi nikimbembeleza labda nimshike shike sehemu ambazo najua akishikwa anafurahi, nimnyonyenyonye hapa na pale, zamani alikuwa anapenda sana. Siku hizi hataki kabisa, nikianza tu, anasema ah! Nimechoka mimi, kwanza nimeshaoga unanipaka matemate yako, wakati bafu liko hapo chumbani angeweza kuoga tena,

Sasa kuna kipindi nami niliamua kukaa kimya, nikawa nasubiri hadi yeye aanze, lakini sasa style alizokujanazo sasahivi mimi siziwezi, yani sio za kawaida, nina mwili mkubwa, nilizaa kwa operation, nina kovu tumboni, siwezi kujikunja kunja Napata maumivu, sasa yeye utakuta ananikunja kama samaki, yani nabanwa nakuwa mdogo, nalia sana, sio kwa raha ila ni kwamaumivu, na hata nikilia anasema nisubiri hadi amalize ndio aniache, akiniacha tu! Ujuwe lazima nitalala hata siku mbili, naumwa sana kiuno,

Kuna siku nilimuuliza kwanini ananifanya kama ananibaka vile, akasema akifanya style za zamani hasikii raha kabisa, kuna kipindi alianza kuniambia kuwa anataka anifanya nyuma, sikuamini masikio yangu, nililia sana, nikamwambia ndoa na ife, narudi kwetu, akanisihi nibaki, nashukuru hakurudia tena kutamaka ushenzi huo,

Style zake za sasa hivi sijui anazitoa wapi, yani sasahivi akiniambia kama anahitaji tu! Basi naweza meza hata dawa ili nijifanye naumwa, napoteza furaha kabisa, yani hawezi kabisa kunifanya kawaida, naombeni mnishauri nifanyaje, maana ni kweli kwa mwanamke yeyote Yule style ninazofanywa mimi, lazima angelia, mimi hadi huwa nakwenda hospitali, ila nikifika sisemi kama nimefanya style mbaya, huwa nadanganya maana naona ni aibu, nitamuaibisha mume wangu na mimi pia.