nisaidieni wapendwa,
nilikuwa safarini Arusha kikazi, kwa muda wa wiki mbili, nyumbani nilimuacha mdogo wangu ambae ni mwanafunzi wa form three, mume wangu , housegirl wangu na mtoto wangu mwenye umri wa miaka minne na nusu.
niliporudi safari nikakuta amani kama kawaida, na wala sijaona mabadiliko yeyote kwa housegirl wangu, kesho yake mume wangu nae alisafikir kikazi, yeye ni dereva wa Bank Fulani hapa Dar es salaam, sasa baada ya kusafiri, usiku niliamua kulala na mwanangu,
nilishangaa sana mtoto akaniambia mama basi ulipoondoka dada alikuwa analala na baba huku chumbani kwakowananichukuwa na mimi, Violet, nilishtuka sana, nikamwambia unasemaje?
Akasema kweli mama, baba alikuwa anavua nguo na dada anavua halafu wanalaliana, nikamuuliza mama mdogo alikuwa wapi? (nikimaanisha Yule mdogo wangu) akasema sijui mwenyew, basi nikaamka usiku huo huo nikamuamsha mdogo wangu nikamuuliza kama aliwahi kulala nje ya nyumbani wakati sipo, akasema ni kweli rafiki yake alifiwa, hivyo alitakiwa kuwa kwenye msiba kwa siku mbili,..........
Mschana nimembana sana, amekataa kata kata yeye hajawahi kulala na mume wangu, mume wangu nae amekana kabisa, sasa sielewi, huyu mtoto hata leo hii umuulize nilipoondoka baba alikuwa analala na nani, anasema na dada, niambieni nahisi kichwa changu kimeruka kabisa, nifanyaje?