Thursday, February 11, 2010

KINA MAMA TUSIWE BUSY SANA KIASI CHA KUACHIA MAHOUSEGIRL KAZI ZOTE!

Kweli tuko busy na kutafuta maisha (pesa), kiasi kwamba lazima uweke house maid nyumbani ili aangalie watoto wako na kukusaidia baadhi ya kazi pale unapokuwa haupo.
Lakini tunajisahau sana na kuacha kila kitu kwa house maid, yani wewe ukishaitwa bosi, basi ndio kila kitu afanye mfanyakazi wako, unakuta hata kutandika kitanda chako na mumeo housegirl ndio anaetandika, 
maana wewe ndio uko busy, lakini ubusy wako usizidi kipimo,
mahousemaid wengine mabosi wao wakiwa hawapo, wanafurahi sana, wanafanya vituko vya kila aina, ukirudi wananyweaaa, wanakuwa wadogo kama piriton! wewe hujiulizi ni kwanini?
mwingine akimaliza kutandika ndio anapumzika kabisa anasoma na vitabu chumbani kwako
bora anaesoma kitabu utasema hakina shida, mahouse maid wengi wanaingia katika vishawishi kutokana na position aliyopewa ndani ya nyumba yako,
house girl atenge chakula kwa baba, tena sio atenge dinning room
anapeleka hadi chumbani alipo mumeo, kweli hii si tunawatega waume zetu??
hapo mama uko busy, nyumbani mwenyewe umemuacha DADA, aangalie familia
mh!


.
sasa, hapa analaumiwa nani?? house girl ndio anakusaidia hadi kunywa au kula na mumeo tena chumbani kwako, unafikiri mumeo mawazo yake yatakuwa kwenye hicho kinywaji au chakula alichopelekewa??

umeona matokeo yake eeeeeeee, baba ameshategwa, MDADA nae ndio anawajibika
mwenyewe ukiulizwa watoto umewaacha nanani, bila hata aibu, nimewaacha na DADA
haya sasa DADA anaacha kulea watoto anamlea DAD
HAPATOSHI........

hadi uje ushtuke ni TOO LATE, kama ndio una kitoto unakiacha na dada, basi kinaona mambo mengi, lakini ndio hakiwezi kusema, kwanza hadi urudi labda kitakuwa kimeshasahau kila kitu! kinaangalia tu!
LAKINI NANI ANASABABISHA HAYA YATOKEE??
Kweli kuna baadhi ya wanaume ambao hawaoni kichaka.......... lakini pia kwa sehemu kubwa tunachangia sisi wenyewe kina mama, si kwamba tusifanye kazi zetu,
kazi tufanye, lakini na housegirl nae umpe majukumu yake, yasipitilize, chumbani kwako akutandikie kitanda labda uwe unaumwa huwezi hata kunyoosha shuka,  mwingine ukimpata mstaarabu atakwambia, mama leo baba kaniambia hivi, lakini wa hivyo wachache, wachache sana, wengi wanakuja macho miamoja, anasubiri ategwe tu! ategeke, sasa kama unaweza zuia asitegwe kwanini usizuie?
anza na mume wako, bwanaeee chakula , kinywaji, vyote viliwe dining room, ukitaka chumbani usubiri hadi mimi niwepo!, unakuta mtu unaacha hadi nguo za ndani za mumeo unamrundikia housegirl afuwe, sasa ni nani mama hapo?? hiii nimeiskia kwenye  familia nyingi sana
mtu analalamika tu! housegirl wangu yuko hivi, yuko vile, sikuhizi anakiburi, unajibu nayeye anajibu, anakujibu si anaona mko sawa nae, kwani una nini ulichomzidi, kama ni baba nae anamjuwa kuliko hata wewe! kama  chupi za baba nae anafua, kitanda kile unachoamka wewe nae analala, sasa mnapishana nini?
MPANGIE HOUSEGIRL WAKO MAJUKUMU, kwamba dada, hakuna kuingia chumbani kwangu wakati baba yako yupo huku, ikiwezekana hakuna kuingia kabisa awepo, au asiwepo,  chumba chako na watoto ni hiki, unakuwa umezuia kitu, umemnyima sheteni nafasi, mengine ya kumshawishi baba wewe unaayajua
NI KWELI YAPO, NA YANATOKEA, TUSIJISAHAU SANA JAMANI






Wednesday, February 10, 2010

BREAKING NEWS




Breaking news kutoka mahakama ya rufaa: Babu Seya, Papii Kocha waendelea kutumikia kifungo cha maisha baada ya mahakama kuthibitisha walishiriki katika kesi ya kubaka , Wakati Nguza Mbangu na Francis Nguza waachiwa huru na kurudi ushwahilini




Inatia huruma sana, inasikitisha sana, waototo wawili wameachiwa huru na kurudi uraiani
lakini Nguza na Mwanae Papii warudishwa gerezani kwa kilio kikubwa sana!
habari hii imenihuzunisha sana!




Tuesday, February 9, 2010

UNAIELEWAJE VALENTINE DAY

siku hiyo zawadi zinakuwa nyingi sana, zenye red tu!

Wewe unaielewaje siku hii ya Valentine,
 kuna wengi wetu tunajua tu kwamba ni siku ya wapendanao, mwingine anakanusha na kusema kila siku tunapendana, hii valentine ina maana ingine tu!, hebu tuwekane sawa hapa.

NI SIKU IPI ILIKUUMIZA SANA MAISHANI MWAKO NA USINGEPENDA ITOKEE TENA????



MM SITASAHAU SIKU NESI ALIVYOMVIRIGA SHUKA MWANANGU WA KIUME AKIDHANI  AMEKUFA! KUMBE NI MZIMA!

MIMI  KWA UPANDE WANGU, siku ambayo sitaisahau maishani mwangu ni siku ambayo nesi alifikiri mwanangu amekufa na kumviriga katika shuka ili mchukuwa mait akija amchukuwe na yeye, aisee, siku ile hadi leo nikikumbuka huwa moyo unaniuma sana, nina watoto wangu wawili (TWINS) baada ya kujifungua niliruhusiwa kwenda nyumbani, nikaka wiki moja waototo wakaanza kuumwa nikawarudisha tena hospitali,(Muhimbili)  nikalazwa, basi kama ilivyokawaida mtoto mchanga akilazwa, wanalazwa kwenye ward yao nyie wazazi kazi yenu kwenda kunyonyesha tu! kila baada ya masaa matatu,

basi mwenyewe ndio wanangu wa kwanza hao tena mapacha, wa kike na wakiume, niliwapenda kama roho yangu, baada ya siku mbili kupita mwanangu wa kiume hali yake ilikuwa mbaya zaidi, akawekewa oxgen kwa ajili ya kumsadia kupumua, nilipoendakunyonyesha mida ya saa sita, hali yake haikuwa shwari kabisa, lakini huwa namwamini Mungu sana, nilikazana kuomba na kumwambia Mungu, niachie watoto wangu? lakini kama ni mapenzi yako basi na yatimizwe ! Ilifika kipindi nikawa nalia tu! 

Baada ya kwenda saa tisa tena kunyonyesha, sikumkuta mwanangu kitandani, nilimkuta mmoja tu! yule wa kike ambae nae alikuwa anaumwa, nikauliza wenzangu walioanza kuingia, jamani mwanangu yuko wapi? mmoja wao akanionyesha chini ya kitanda, na kusema bahati mbaya!, amekufa!  nilijikuta naishiwa nguvu na kuanguka chini huku nikilia sana na kwa sauti, basi wakaja wakanishika wakati wananitoa nje tuko mlangoni tukakutana na Dr. mmoja mlangoni, akauliza nini? na kwanini kama mtoto wake amefariki mmemruhusu kuingia huku? wakamwambia kuwa nina watoto wawili, hivyo niliruhusiwa kuingia ili nikanyonyeshe aliebaki

Mungu wa ajabu jamani, yule Dr. akaingia hadi ndani na kuuliza yuko wapi aliekufa, wakamwonyesha, akamfungua shuka, kukuta katoto kanahema ila kwa mbaaaali kabisa, alicho kifanya na sitasahau alisema hivi
FUTA MACHOZI YAKO! MUOMBE MUNGU MTOTO WAKO NI MZIMA NGOJA NIMSHUHURIKIE, NISIKUSIKIE UNALIA HATA KIDOGO!, nilipata nguvu za ghafla nikasimama nikamfata Dk. nikamuangalia alichokuwa akifanya, alimuingiza mtoto puani mpira, akawa anamjaza hewa, gafla tumbo la mtoto likawa kubwaaaaa, akatoa ule mpira akamchukuwa mtoto wangu hadi kitandani akamuewekea mpira mwingine mdogo wa oxgen na kuniambia kila nikiingia kunyonyesha nihakikishe mpira uko pale pale puani, kisha akamuita yule nesi aliekuwa zamu na kuondoka nae, ambae sielewi ni action gani ilichukukuliwa juu yake, maana hadi naruhusiwa hospitali sikumtia machoni tena,

Kumbe pale alipokuwa amewekwa mwanzoni ni kwamba alikuwa akisubiriwa mchukuwa maiti aje azikusanye, hatimaye mwanangu aakawa mzima, huwa nikimuangalia simmmalizi, Mungu alinitetea sana, na nilisimama katika imani tu! nilikaa muhimbili  mwezi mzima, lakini MUNGU WANGU NI MWAMINIFU hadi leo wanangu ni wazima kabisa, na nikiwaangali tu! huwa nafurahi sana, nawapenda mno,  na siku ileile nilimsamehe yule nesi,

NA HAWA NDIO TWINS WANGU, TRACY & TYMON  ni wazima kabisa
na hapo walipiga mwaka jana mwezi wa tatu walikuwa wanatimiza miaka mitatu,
wamesheaanza kusoma, basi huyo mtoto wa kiume nikimuangalia, Mh! namshukuru Mungu tu!


Monday, February 8, 2010

MUME WANGU HANA HAMU NA MIMI- SIMUELEWI

nahitaji msaada wenu jamani
mume wangu hana hamu namimi kabisa, nakuwa nashindwa kumuelewa kabisa, yani huwa najitahidi sana kuwa karibu nae, huwa naonyesha kabisa kuwa namuhitaji na sio kunyesha tu! bali huwa namuhitaji toka moyoni kikweli kabisa, lakini mwenzangu huwa haonyeshi kabisa kama yuko namimi, mara nyingi sana imetokea hii, na kabla hatujafunga ndoa hakuwa hivi, kilichozidi sana ni pombe anazo kunywa, alikuwa akinywa toka zamani, lakini hivi karibuni amekuwa mlevi wa kupindukia, akirudi nyumbani ni kuanzia saa tano usiku, napo amelewa sana, 
 
alishawahi kupata ajali shauri ya ulevi, aliumia sana, Lakini Mungu alimsadia akapona ,alilpunguza kidogo kunywa pombe, baada ya muda akarudi kule kule, mbaya zaidi akaanza kunifundisha na mimi, mimi sikupenda kabisa maana sikuona wala kuhisi utamu, nikaacha wala sikuendelea kujifunza,
unakuta akirudi kama hajalewa sana basi anakuwa busy na shughuri zake zingine tu, ataangalia Tv hadi usiku sana, au ataanza kucheza game, yani hana hamu na mimi kabisa,
sikuwahi kusikia kuwa labda ana mwanamke mwingine, ila kwa jinsi alivyo sasa naanza kuhisi hivyo, ila nahisi vitu viwili, kama sio mwanamke mwingine, basi nahisi ni pombe anazokunywa.
kuna siku aliporudi nilimwambia kuwa namuhitaji, maana tulikuwa teyari tumefika wiki tatu bila kufanya kitu chcohote kile, siku hiyo aliwahi kurudi kwakuwa nilimdanganya mtoto wetu anaumwa, akarudi saa mbili, alipokuta mtoto mzima nilimuita chumani nikamwambia shida yangu, nikamueleza kwanini ananitesa hivi,
akauliza kwani nakupiga, au sikupi hela ya kula? nikamwambia hata kuwa mbali na wewe ni mateso kwangu,
akanifokea sana kwanini nimesingizia mtoto anaumwa na kunipa baadhi ya mifano kwamba inaweza kutokea kweli akaumwa, niliomba msamaha na kumwambia sitarudia tena ila kwa usiku huo anipe haki yangu, nilikuwa nikimuitaji sana, cha ajabu wala hakujali hisia zangu, ndio kwanza akapanda kitandani tena siku hiyo hakuoga wala kula, akalala, nikamwambia nimekuandalia chakula kizuri akasema anajisikia kuumwa nimuache apumzike, nilisononeka sana, kesho yake nikamdamsha ili twende hospitali akasema atanda mwenyewe, imefika usiku karudi kalewa sana, namuuliza kama alienda hospitali akasema alikunywa panadol akapona kabisa, sasa mimi sielewi jamani,
hali hii inanitesa sana mimi, niliwahi kumuita best man wetu na aliongea nae namimi nikiwepo, akatubu na kuahidi kubadilika, basi siku mshenga alipoondoka niliinjoy sana, kwani nilipata kile nilichokuwa nakihitaji kwa nafasi, niliona kama nimepelekwa mahali pazuri sana, nilijua hali ile itaendelea,
baada ya wiki kama mbili kupita, ikarudia pale pale, yani kumkuta nyumbani, hadi uweke apoint ment, hadi weekend yeye ni safari tu! hajui kanisa wala msikiti, tangu tutoke kushukuru kanisani ni baada ya harusi hakwenda tena, siku ya ubatizo wa mtoto alikwenda tena baada ya kumsema sana maana alisema yeye hatoenda, since that day, hajaenda hadi leo.

Dada violet, ananipa wakati mgumu sana mume wangu, kujali familia yake anatujali sana, tunakula, anampenda mtoto sana, hanipigi, ila hivi vitendo ambavyo anafanya simuelewi? je pombe imemaliza hamu yake??? kuna mwanaume kweli ambae ni kamili akaacha kumpa haki mkewe kwa takribani wiki tatu? nimempekuwa na kumpeleleza sana labda ana mwanamke mwingine, anasema hana, sasa mbona hanitamani??mbona haonyeshi kama anahamu namimi, mimi ni mzuri, najijuwa kabisa hilo halina ubishi, nimeridhika na mungu alivyoniumba. ninajiheshimu sana.
ananifanya nitamani sana ndoa za wenzangu, ananifanya nitamani hata kuwa na mwanaume mwingine ambae atautambua uthamani wangu, lakini naogopa sana, maana maradhi ni mengi, pia namuogopa sana Mungu,
unakuta hadi napoteza hamu yakula. na siku nikibahatika kula nae basi huwa nakula hadi najishangaa, nafurahi siku nzima, ila ujuwe siku akishinda nyumani anaumwa.hii imekuwa too much maana hata wazazi wake wakija anakuwa hivyo hivyo kunasiku alikuja mama yake mzazi kutusalimia, nikafurahi nikajua siku hiyo atawahi kurudi, lakini alirudi saa 6 na kukuta mama amekwisha lala, nilimsema sana, akalala bila hata kuoga, asubuhi akataka kutoka bila hata kumsalimia mama, nikafata nikamuuliza huyu ni mama yako mzazi au wa kukulea tu! akajitetea eti anaogopa kumsumbua nimuache alale, nikamvuta hadi kwa mama yake ndio kwa aibu akaenda kumsalimia, nilimuweka mama wazi,juu ya hali ile, mama alichukia sana alimsubiri hadi aliporudi na alimsema sana, akamwambia kama ananiona kero aniache nirudi kwetu asinifanye mlinzi, maana alikuwa hataki hata nifanye kazi anataka nikae nyumbani tu!
kama kawaida yake, aliomba msamaha tena, tukaka siku mbili hali ikarudi pale pele, nikitafuta mtu mwanaume mwingine nitakuwa nimekosea sana, sasa nifanyaje jamani?
ushauri wenu ni wamuhimu sana kwangu





Friday, February 5, 2010

Mazoezi ni Muhimu sana Kwa Afya Njema ( Weekend Njema)

Hii sijapata uhakika na vielelezo vya kutosha ila nilipata kusikia kwenye mazungumzo fulani mahali, kulikuwa na mkusanyiko wa wasomi wa mambo ya afya. Moja ya jambo ambalo walinigusa sana kwenye mazungumzo yale ni hili: Ajali kweli zinatokea kwa uzembe wa waendesha vyombo hivyo hasa hapa miji. Unakuta gari imepata ajali si mbaya sana lakini waliopoteza maisha ni wengi na ukiwachunguza hawana majelaha makubwa nje wala ndani ya mwili. Walisema sababu kubwa watu ni wazembe na ni twipwatipwa, utipwa tipwa sio lazima uwe kiiiibooonge sana. Hata huo mwili ulionao unawezakuwa tipwatipwa kuwa hauna mazoezi. Sasa basi unapopata mshituko mkubwa unakuwa hauwezi kuhimili vishindo hivyo na kukusababishia BP ya ghafla na kupoteza maisha. Kwa kifupi niliona kuwa mazoezi ni mhuimu kwa afya iliyo bora na si bora kunenepa tu.
Weekend hii naomba uanze mazoezi hasa wakati wa jioni unarudi nyumbani, fanya jambo lifuatalo. Shuka vituo vi3 kama viko karibu karibu au 2 ama 1 kabla ya kile unachoshuka kwenda nyumbani mwako kama unatumia daladala. Tembea kwa mwendo wa kasi mpaka ujisikie umechemka na jasho linakutoka, ukifika nyumbani utakuwa ushafanya mazoezi makubwa sana. Fanya hivyo kila siku utokapo kazini.
MAHITAJI:
1. Hakikisha unakuwa na SkinTYT ili kuzuia michubuko kwenye mapaja
2. Maji Masafi yasiyo ya baridi ya kunywa
3 Viatu Simple, ukipenda vile vinaitwa vibajaji
4 Leso ya taulo 100% Cotton ( Hii kwa wale wenye tatizo la chunusi inasaidia sana kutoa mafuta kwenye uso na kuuacha mkavu)

 FAIDA ZAKE:
1 Kuondoa uwezekano wa BP
2 Kujenga na kusafisha ngozi kwa kutoa jasho
3 Kuwa kakamavu (Strong)
4 Tabia ya mazoezi
5 Kutoka jasho usoni na kufuta kwa Taulo inasaidida kutoa mafuta yanayojihifadh kwenye ngozi ya uso na kukuleta chunusi.
6 Kupunguza uzito NK....
Data Fulani Kutoka Mtandao: IRISH MEDICAL TIMES

Wednesday, February 3, 2010

JE, INAWEZEKANA KUURUDISHA UPENDO ULIOPOTEA??? NA JE INAWEZEKANA MTU UKASAMEHE NA KULISAHAU KOSA LAKE??

 
Katika maisha kuna mambo mengi sana, yanaumiza, yanakera, yanachoma sana
hali ambayo inafanya wengi kushindwa kustahimili na kujikuta wanajaza jazba moyoni, Na kujikuta hutamani hata kuongea na yule aliekukosea, ukimuona unatamani hata kukimbia


kama ni mke na mume basi kila mtu atalala kivyake, huyu atageukia huku, huyu atageukia kule, wengine hata kuhama chumba na kulala chumba kingine, hadi asubuhi,


inafika kipindi ukimuona aliekukosea, unaona kama moyo wako umejeruhiwa, unaona kama vile moyo wako una tundu, yani unapoteza amani kabisa, unatamani akae mbali kabisa, yani unaweza hata kumuombea mabaya yamfike ili nafsi yako idhirike.


waweza kuwa nae sehemu falagha, lakini kutokana na lile alilokukosea unajikuta unahama kabisa kimawazo mahali hapo, unaokuwepo kimwili tu! 


mwingine unakuwa na hali ya kulia tu! unajaza uchungu moyoni mwako,
LAKINI JE? KUNA KOSA LISILOSAMEHEKA? huwezi kusahau,  wengi hupenda kusema nimekusamehe lakini sitokusahu, ukisimama kidini hapa maana yake hujasamhe kabisa,  
(hii ni kwa Vivian ulieniomba ushauri kwamba mpenzi wako amekuudhi na ametubu bado hutaki kumsamehe)
na kwa wengine pia tujifunze kupitia ushauri wa humu tutakaokuwa tukishauriana, kwanini usimsamehe mpendwa wako??? kwanini asikosee? yeye ni malaika? ni bin adam kama wewe, je Mungu akisema aifunue Dunia hii kila mtu aonekane anachokifanya kisichostahili, kuna atakaebaki salama??kwanini tusijifunze kusamehe na kusahau, kwanini tusiachilie mioyo yetu ikawa na amani na kila mtu?? 
tujifunze kusamehe itatusaidia kwenye maisha yetu, pia hutashindwa kuishi na mtu kama utakuwa ni mtu wa kusamehe, wapo watu wa namna hii, ningumu lakini ni inakupa amani ya maisha yako, Ukisamehe unakuwa huru hata nafsini mwako,   YES! Inawezekana kusamehe kabisa,
au wewe msomaji utuambie wewe huwezi kusamehe mtu aliekukosea na ukaamua kusahau??? SIO KUDHARAU, namaanisha usamehe na usahau, HAIWEZEKANI???????
 

Tuesday, February 2, 2010

INAKUWAJE MWANAMKE UNAKUWA NA KUCHA CHAFU?????

Jamani urembo sio usoni tu au mavazi kama ambavyo wengi wanafikiria,
tujajisahau sana kuangalia kucha zetu, unakuta mtu amependeza kweli, lakini muangalie kucha zake, unaweza kuona hata kinyaa kula nae chochote
Inapendeza sana kama mwanamke ukiwa na kucha safi, kwanza kucha chafu zinaficha uchafu mwingi
Kucha safi sio lazima upake rangi, waweza kata tu zikawa fupi zikapendeza au ukapaka corouless, 
Mh! hii iko kwa watu wengi sana, mtu unakuta anakata kucha na meno, vikucha vikitoka pale vinakuwa vifupiiiii? vinapoteza mvuto kabisa, yani tukucha tunakuwa na sura mbaya sana.

kama unakuwa unaona uvivu unaweza mwambia hata mpenzi wako akukate, kulikoni kuwa na kucha chafu, mwingine unakuta kucha chafuuu, halafu anapiga bonge ya sandols miguuni, inakuwa hainogi jamani
wa kurahisisha ukataji wa kucha kama huyu mrembo hapa wapo kibao, mm huwa nikiwakuta nawatoa mkono mdomoni, mwenyewe unakuta ametulia kabisa,
unaweza kuwa na kucha ndefu tu! lakini ukijua jinsi ya kuzitunza wala hazina shida, lakini utakuta mtu amefuga kucha, halafu full kujikuna, akitoka hapo mikucha myeusiii, na wala haoni noma, anakuwa MPANAAA, yani haoini hata aibu, mimi nikiona mtu anakucha chafu tu huwa naona hata kinyaa kushea nae chakula chochote kile, na hii si kwangu tu hata kwa familia yangu, Mr. kucha zikiwa ndefu tu! zinakatwa, waototo wangu ni kila baada ya wiki, hadi wao huwa wanakumbusha, mama leo tukate kucha,  tena kwa watoto ndio tunajisahau kabisa yani,
Vifaa vya kukatia kucha viko kibao, tena wala havina bei, simple tu! unaweza kuwa na Tsh 5000/= tu ukapata seti nzima yenye vikorokoro kibao, weekend uko home, basi unajisafisha wewe mwenyewe,
Nail Cut kama hii ikiwa peke yake ni Tshs 1500/= tu! unaitumia hadi unachoka, na kucha zinapendeza kabisa, kariakoo vimejaa kibao,
Machine nyingine ni Mkasi mdogo na ni special kwa ajili ya kucha tu! sio uchukuwe mkasi wa nguo ukatie kucha, utatoa vidole, mkasi mdogo kama huu bei yake ni 1000/= hadi 1500/= kucha zinakuwa zinapendeza ,
sasa hivi kuvaa sanviatu vya wazi (simple tu) ni fassion, basi bora uwe na kucha safi ndio uvae, huduma zote hizi waweza jifanyia wewe mwenyewe gharama yako ni kununua vifaa tu! ukiona uvivu, basi toa pesa upeleke kwa wataalam wa kucha wakusafishe, wewe upumzike tu!, wale wa huku kwetu Gongolamboto (GOMS) ukiona uvivu njoo pale DOUBLE 'T' HAIR DRESING SALON, huduma hii inapatikana
hebu jiangalie hapo ulipo, kucha zako, ni safi??? wewe unalo jibu.
mimi najaribu tu kuwakumbusha jamani, kucha zikiwa safi zina raha yake,

Monday, February 1, 2010

MUME WANGU AMEOA KWA SIRI NA SHAHIDI YAKE SIKU YA HARUSI NI BINTI YANGU NILIYEMZAA MWENYEWE

Kwakweli akili yangu haitaki kuamini kilichotokea, lakini hata isipoamini, ukweli utabakia pale pale,
Mimi ni mama wa familia yenye watoto wanne, wakwanza ana mika 23 wapili miaka 18 watatu miaka 16 na wa mwisho anamiaka 7, kinachoniumiza sana na kuninyima raha na kunifanya nijishushe thamani, ni kitendo cha mume wangu kuoa katoto kadogo sawa na mwanae, tena kaoa kwa siri, na siku ya ndoa yao alienda na binti yangu wa miaka 18, Binti alishiriki katika harusi ya baba yake na hakumwambia mtu yeyote, alinificha hata mimi mama yake niliyemzaa kwa uchungu, alikaa kimya kabisa hadi nimekuja kugundua ndoa hiyo ina miezi minne sasa, nililia nakuumia sana baada ya kuona picha ambazo Binti yangu nae amepiga na huyo Bibi harusi siku ya harusi,
kabla ya ndoa hiyo mume wangu alikuwa ni mtu wa kero, mtu mwenye gubu, kitu kidogo tu kwake kinakuwa kikubwa sana, ila mara kwa mara alikuwa akinitishia kuoa mke wa pili, ukiangalia sisi tulichelewa sana kuzaa watoto wote hao tumewazaa tukiwa watu wazima kabisa, tumepitia maisha magumu sana, lakini baada ya kupata pesa ya kustaafu tu! ndipo alipoenda kuoa, tena huyo bibi harusi kwenye picha anaonekana ni mtoto kabisa, kinacho niuma ni kwanini amshirikishe mwanangu kwa siri? mtoto amechange sana, siku nilipoona zile picha kwenye laptop ya baba yake nililia sana, nilimuita binti yangu ambae yuko for four, nikamuuliza kwanini alifanya vile na baba yake na kuamua kunificha? ukizingatia ni mtoto wa kike?, nampenda sana mwanangu, lakini wakati namuuliza  mtoto alikaa kimya, kila ninapomsemesha juu ya suala hilo hajibu chochote, zaidi ya kusema mama muulize baba mwenyewe, mtoto pia amebadilika sana,
pia nahisi ushirikina kwa sehemu fulani, maana kuna siku binti yangu yule wakwanza alipiga kelele usiku na kuja kugonga chumbani kwangu, nilimuuliza kuna nini? akasema kuwa amemuona mdogo wake(yule alienificha) kuwa anataka kumchoma kisu, niliingia hadi chumani kwao, nikakuta anacheka kitandani, nilimuuliza ana nini? na kwanini anafanya hivyo akajibu kwa dharau mama usimsikilize huyo, kalale anaota tu! sasa kisu kiko wapi? toka siku hiyo binti mkubwa amehama chumbani analala na huyu mdogo wake wamwisho. yani kuna vitu vya ajabu ajabu ambavyo sivielewi kabisa.
siku nyingine tena nilikuta khanga yangu ina damu na pia imeandikwa kiarabu, ikiwa sandukuni, sikuivaa tena niliichukuwa na kuichoma moto, mume wangu sasa hivi ananiomba msamaha, wakati aliamua kuoa bila kuniambia, sasa hivi ndio anatubia na anaomba nimruhusu awe analala kwangu siku nne kule kwa mke mdogo alale siku tatu! nilimwambia akitaka hata ahamie huko sawa tu!
wengi wamenishauri, hata majirani zangu wengine wameniomba niondoke nisijekuuliwa bure, nikiangalia na utu uzima huu mimi naenda wapi? sina raha, nishaurini , najua nawapa wakati mgumu sana, lakini ndio limeshanitokea,

HATIMAYE TUNAWEZA GROUP IMEFIKISHA MWAKA MMOJA

 
Jamani tuna kikundi cha kina mama huko kwetu
GONGOLAMBOTO
sasa tarehe 30 january tulikuwa tumefikisha mwaka mmoja, tulifanya party simple tu
kwaajili ya kufurahia kufika mwaka mmoja, na pia kukitambulisha rasmi kwa viongozi wetu, ukumbi ulikuwa LIBERTY HOLL kulekule GOMS'
was fun kwakweli, coz tulienjoy sana


sare siku hiyo ilikuwa pink na white,  na mie ndio MWENYE KITI, we
niliku busy sana that day,


wageni wetu rasmi siku hiyo walikuwa ni Mr. Jery Silaha, ambae ni Diwani wa kata ya Ukonga
na Mrs, Violet Mbele ambae ni Mkurugenzi wa Sacos kule Ukonga


hapo MWENYEKITI Akisoma Risala kwa wageni rasmi, mh! ilipendeza kiukweli,


Mgeni Rasmi akitupa maneno yake ya busara, kwa kikundi, tulimpenda sana coz yupo simple na charming sana


WANAKIKUNDI HAO, tunaweza group wakinipa hongera baada ya kuwasilisha Risala yetu


ule wakati ukafika, Mrs Violet Mbele, nae alipewa heshima kwa kutukatia keki
 
hahahahahaaaaaaaaaaaa, ilikuwa tamu sana


MC alinipa nafasi ya kumlisha mgeni rasmi 


wana kikundi hao


Mume wa MWENYEKITI nae alikuwepo, kumpa support mke wake,


Tulifurahi sana coz tulipata nafasi ya kukutana na kufahamiana 


Mama huyu namtengemea sana kwa ushauri, Nae alifika kusherehekea pamoja nasi
thanks MARYRYOSE


AT the end tulipata msosi, tulikula tukasaza, 


mgeni wetu akipata msosi kabla ya kutoka, pembeni pale ni katibu wetu.
  
Tulifurahi sana maana tulijifunza elimu ya ujasiliamali toka kwa mgeni wetu
Violet , ilikuwa simple sana, na ilipendeza sana. malengo yetu ni mengiiii na ni makubwa sana
TUNAAMINI PENYE NIA PANA NJIA,
TUTATOKA TU!