Friday, February 5, 2010

Mazoezi ni Muhimu sana Kwa Afya Njema ( Weekend Njema)

Hii sijapata uhakika na vielelezo vya kutosha ila nilipata kusikia kwenye mazungumzo fulani mahali, kulikuwa na mkusanyiko wa wasomi wa mambo ya afya. Moja ya jambo ambalo walinigusa sana kwenye mazungumzo yale ni hili: Ajali kweli zinatokea kwa uzembe wa waendesha vyombo hivyo hasa hapa miji. Unakuta gari imepata ajali si mbaya sana lakini waliopoteza maisha ni wengi na ukiwachunguza hawana majelaha makubwa nje wala ndani ya mwili. Walisema sababu kubwa watu ni wazembe na ni twipwatipwa, utipwa tipwa sio lazima uwe kiiiibooonge sana. Hata huo mwili ulionao unawezakuwa tipwatipwa kuwa hauna mazoezi. Sasa basi unapopata mshituko mkubwa unakuwa hauwezi kuhimili vishindo hivyo na kukusababishia BP ya ghafla na kupoteza maisha. Kwa kifupi niliona kuwa mazoezi ni mhuimu kwa afya iliyo bora na si bora kunenepa tu.
Weekend hii naomba uanze mazoezi hasa wakati wa jioni unarudi nyumbani, fanya jambo lifuatalo. Shuka vituo vi3 kama viko karibu karibu au 2 ama 1 kabla ya kile unachoshuka kwenda nyumbani mwako kama unatumia daladala. Tembea kwa mwendo wa kasi mpaka ujisikie umechemka na jasho linakutoka, ukifika nyumbani utakuwa ushafanya mazoezi makubwa sana. Fanya hivyo kila siku utokapo kazini.
MAHITAJI:
1. Hakikisha unakuwa na SkinTYT ili kuzuia michubuko kwenye mapaja
2. Maji Masafi yasiyo ya baridi ya kunywa
3 Viatu Simple, ukipenda vile vinaitwa vibajaji
4 Leso ya taulo 100% Cotton ( Hii kwa wale wenye tatizo la chunusi inasaidia sana kutoa mafuta kwenye uso na kuuacha mkavu)

 FAIDA ZAKE:
1 Kuondoa uwezekano wa BP
2 Kujenga na kusafisha ngozi kwa kutoa jasho
3 Kuwa kakamavu (Strong)
4 Tabia ya mazoezi
5 Kutoka jasho usoni na kufuta kwa Taulo inasaidida kutoa mafuta yanayojihifadh kwenye ngozi ya uso na kukuleta chunusi.
6 Kupunguza uzito NK....
Data Fulani Kutoka Mtandao: IRISH MEDICAL TIMES

4 comments:

  1. mh! mwenzangu, bora hata ulivyotushauri nini cha kufanya, lakini mbona mimi ni mvivu sana kutembea? mbona nikitembea kidogo moyo unanienda mbio??? halafu mbona mimi najihisi labda nini shida? maana nikitembea kwa kasi tu huwa nawashwa mwili mzima, nawashwa sana hadi kichwani, na hasa kwenye nyayo na mapaja, kwa kifupi huwa nawashwa mwili wangu woooote, naomba ,mnisaidie juu ya hili, nalo nitalitoaje? yani hata nikikimbia tu! huwa nawashwa mwili mzima
    Emmy

    ReplyDelete
  2. Emmy
    mie mwenyewe nilikuwa na tatizo kama lako, na kwasasa hivi limepungua kidogo, lakini hili linasababishwa na mwili kutokuwa na mazoezi, kujiachia, mtu unakaa tu bila mazoezi, hukimbii hadi usikie mabomu yanalipuka ndio unakimbia, lakini kwa ushauri tu! fanya mazoezi kwa muda kidogo, then utaona tofauti zilizopo. mimi hii ya kujikuna huwa inaniingia sio tu kwakutembea kwa kasi, lakini hata nikiona uchafu, hasa kipindi cha mvua, basi we! panakuwa hapatoshi, huwa najikuna hadi nakaa chini, nilishawahi kwenda hospitali, nikapewa dawa nikatumia, lakini haikusaidia hata kidogo, nikiona mafua, kinyesi au nikikanyaga matope tu! basi mwili unasisimka sana hapo hapo naanza kujikuna hasa kwenye miguu na kwenye mapaja.inakera sana, but mazoezi yanasaidia kwa sehemu
    weekend njema mpenzi

    ReplyDelete
  3. Pole sana dada unayewashwa mwili mzima ukifanya mazoezi. Nimesoma coment yako nikajaribu kuperuzi kwenye vyanzo ila bado sijapata. Kikubwa hapo ni ile hali ya kulimbikiza kwa sumusumu kwelu ngozi amabyo ilitakiwa kutoka kwa jasho ikiambatana na maji, chumvi na mafuta. Vyote hivi vinakuwa havihitajiki kwenye mwili. Sasa unafonya mazoezi mwili huchemka na vile ule uchafu huanza kuchemka na kutakiwa kutoka. Hapo ndipo mwili unaanza kuwasha. Ila kama utaendelea na mazoezi kwa kutojari muwasho baada ya siku au hata siku hiyo hiyo muawasho hauendelei tena. Ila kesho yake utakuwepo tena kidogo mpaka utaisha kabisa. hiyo itatokana na kuondoa sumu zote kwenye ngozi. Nakushauri vumilia na endelea na mazoezi. Na kuna dada huyo amesema hata akiona matope ama uchafu, pia nae huwa anakinyaa fulani. Sasa mwili husisimka mara tu anapoona huo uchafu, na kusababisha mwili kuchemka au kuamsha mchemko fulani. Basi huamsha zile sumu zinazotakiwa kutoka mwilini ambazo zipo tu kwenye ngozi na kuanza kumuwasha. Ila si ugonjwa. Wote nawashauri kazaneni kwenye mazoezi.

    ReplyDelete
  4. Jamani nimeanza mazoezi si utani siku ya kwanza nililala mwili wote unauma. lakini sasa ninasiku ya tano mambo mazuri kabisa, na mwili na nauona mwepesi sana sasa inabidi nipunguze vyakula nataka kuwa miss angalau nivae size 14 asanteni kwa ushauri
    mpendwa

    ReplyDelete