Wednesday, February 3, 2010

JE, INAWEZEKANA KUURUDISHA UPENDO ULIOPOTEA??? NA JE INAWEZEKANA MTU UKASAMEHE NA KULISAHAU KOSA LAKE??

 
Katika maisha kuna mambo mengi sana, yanaumiza, yanakera, yanachoma sana
hali ambayo inafanya wengi kushindwa kustahimili na kujikuta wanajaza jazba moyoni, Na kujikuta hutamani hata kuongea na yule aliekukosea, ukimuona unatamani hata kukimbia


kama ni mke na mume basi kila mtu atalala kivyake, huyu atageukia huku, huyu atageukia kule, wengine hata kuhama chumba na kulala chumba kingine, hadi asubuhi,


inafika kipindi ukimuona aliekukosea, unaona kama moyo wako umejeruhiwa, unaona kama vile moyo wako una tundu, yani unapoteza amani kabisa, unatamani akae mbali kabisa, yani unaweza hata kumuombea mabaya yamfike ili nafsi yako idhirike.


waweza kuwa nae sehemu falagha, lakini kutokana na lile alilokukosea unajikuta unahama kabisa kimawazo mahali hapo, unaokuwepo kimwili tu! 


mwingine unakuwa na hali ya kulia tu! unajaza uchungu moyoni mwako,
LAKINI JE? KUNA KOSA LISILOSAMEHEKA? huwezi kusahau,  wengi hupenda kusema nimekusamehe lakini sitokusahu, ukisimama kidini hapa maana yake hujasamhe kabisa,  
(hii ni kwa Vivian ulieniomba ushauri kwamba mpenzi wako amekuudhi na ametubu bado hutaki kumsamehe)
na kwa wengine pia tujifunze kupitia ushauri wa humu tutakaokuwa tukishauriana, kwanini usimsamehe mpendwa wako??? kwanini asikosee? yeye ni malaika? ni bin adam kama wewe, je Mungu akisema aifunue Dunia hii kila mtu aonekane anachokifanya kisichostahili, kuna atakaebaki salama??kwanini tusijifunze kusamehe na kusahau, kwanini tusiachilie mioyo yetu ikawa na amani na kila mtu?? 
tujifunze kusamehe itatusaidia kwenye maisha yetu, pia hutashindwa kuishi na mtu kama utakuwa ni mtu wa kusamehe, wapo watu wa namna hii, ningumu lakini ni inakupa amani ya maisha yako, Ukisamehe unakuwa huru hata nafsini mwako,   YES! Inawezekana kusamehe kabisa,
au wewe msomaji utuambie wewe huwezi kusamehe mtu aliekukosea na ukaamua kusahau??? SIO KUDHARAU, namaanisha usamehe na usahau, HAIWEZEKANI???????
 

6 comments:

  1. kusamehe ni jambo jema sana kama umekorofishwa au kuumizwa sidhani kama ni vyema kutomsamehe mtu, hata vitabu vya dini vinashauri hivyo, mtu anayesema nimekusamehe lakini sitakusahau huyo hajasemehe, unaposemehe kitu/mtu huwezi kutamka neno jingine

    ReplyDelete
  2. Helow mama tracy,kusamehe kupo ila cunajua watu tumetofautiana,wengine kusamehe na kusahau ni kitu rahisi sana ila wengine ni ngumu,pia kuna wengine anaweza kwambia nmekusamehe kumbe moyoni bado analo,kitu ambacho c kizuri,khs huyo dada inawezekana huyo mwenzie alikuwa anamsamehe ila akawa anadrudia kumkosea,sasa hapo inafikia kipindi mtu unachoka unasema sasa bac!pengine kutomsamehe kwake kunamfanya ajifil ana amani kuliko akimsamehe,ASIA ALAWI

    ReplyDelete
  3. Kusamehe inawezekana kabisa na bila wasiwasi. Ila kusamehe huko kutokane na mkosaji kukiri kosa na kutolirudia tena. Sasa utasamehe vipi kama mkosaji hajakiri kosa na hata hilo kosa halijutii? Ni wazi itakubid upuuze kosa na mkosaji pia umpuuze. Kusamehe ni jambo jema sana na linaleta amani kwenye mahusiano na kujifunza mengine. Hakuna sababu ya kukaa na kosa moyoni wakati mkosaji kaomba msamaha na kakiri kosa lake. Unafikiri hapo nini cha kufanya ni amani na upendo. Tatizo liko kwa yule mwenza wako anajua kuwa unajua anafanya kosa fulani ila yeye anatafuta mbinu ya kulifanya kwa siri na kusimama kwenye msimamo kuwa yeye hafanyi hivyo kwahiyo unamzushia. Je utasamehe vipi hili DADA Vai? Mtu anatumia hata uongo na hata kukutengenezea makosa kwenye familia uonekane wewe ndio mkosaji. Je mtu huyu utamsamehe vipi?
    Kwahiyo msamaha huja kwa mkosaji kukiri kosa na kutorudia kosa kwana namna yoyote ile iwe kwa siri au waziwazi. INAWEZEKANA KUSAMEHE NA KUSAHAU KOSA ALILOFANYA MWENZA WAKO.

    ReplyDelete
  4. ISSUE SI KUANGALIA NANI AMEKOSEA NINI?
    HAPA ISSUE NI KUSAMEHE TU NA KUSAHAU KAMA KWELI MNAPENDANDA,
    LAKINI MKIANZA OH! HUYU KAPELEKA KWA WAZAZI, MARA OH! YULE KAPELEKA MTAANI, MARA OH! HUYU KAPELEKA KWA MAPADRI,
    YOTE HIYO NI KUTAFUTANA NA KUENDELEZA BIFU AMBAZO MIMI NAITA NI ZA KIPUUZI,
    HAPA ISSUE NI KUTOTAZAMA NANI AMEKOSA NINI
    HAPA ISSUE NI KUSAMEHE TU! BILA KUANGALIA UZITO WA KOSA
    JOYS

    ReplyDelete
  5. JOYS unaweza ukawa unajua kusoma ila ukawa hujui kutafasili maneno. Kwa lugha ingine unasomo ila hupata maana wala ujumbe wowote.

    ReplyDelete
  6. JOYS USHAURI WAKO NI MZURI SANA ENDAPO KAMA HUJAWAHI KUKOSEWA KOSA AMBALO LIKAITWA KOSA HASWAAA, UNAJUA KUNA MINER KOSA AMBALO UNAWEZA KUFATA USHAURI WAKO LAKINI KUNA MAKOSA MENGINE NI MAZITO KWA USHAURI WAKO INAKUWA NGUMU KUFUATA...

    VINGAWAJE

    ReplyDelete