MM SITASAHAU SIKU NESI ALIVYOMVIRIGA SHUKA MWANANGU WA KIUME AKIDHANI AMEKUFA! KUMBE NI MZIMA!
MIMI KWA UPANDE WANGU, siku ambayo sitaisahau maishani mwangu ni siku ambayo nesi alifikiri mwanangu amekufa na kumviriga katika shuka ili mchukuwa mait akija amchukuwe na yeye, aisee, siku ile hadi leo nikikumbuka huwa moyo unaniuma sana, nina watoto wangu wawili (TWINS) baada ya kujifungua niliruhusiwa kwenda nyumbani, nikaka wiki moja waototo wakaanza kuumwa nikawarudisha tena hospitali,(Muhimbili) nikalazwa, basi kama ilivyokawaida mtoto mchanga akilazwa, wanalazwa kwenye ward yao nyie wazazi kazi yenu kwenda kunyonyesha tu! kila baada ya masaa matatu,
basi mwenyewe ndio wanangu wa kwanza hao tena mapacha, wa kike na wakiume, niliwapenda kama roho yangu, baada ya siku mbili kupita mwanangu wa kiume hali yake ilikuwa mbaya zaidi, akawekewa oxgen kwa ajili ya kumsadia kupumua, nilipoendakunyonyesha mida ya saa sita, hali yake haikuwa shwari kabisa, lakini huwa namwamini Mungu sana, nilikazana kuomba na kumwambia Mungu, niachie watoto wangu? lakini kama ni mapenzi yako basi na yatimizwe ! Ilifika kipindi nikawa nalia tu!
Baada ya kwenda saa tisa tena kunyonyesha, sikumkuta mwanangu kitandani, nilimkuta mmoja tu! yule wa kike ambae nae alikuwa anaumwa, nikauliza wenzangu walioanza kuingia, jamani mwanangu yuko wapi? mmoja wao akanionyesha chini ya kitanda, na kusema bahati mbaya!, amekufa! nilijikuta naishiwa nguvu na kuanguka chini huku nikilia sana na kwa sauti, basi wakaja wakanishika wakati wananitoa nje tuko mlangoni tukakutana na Dr. mmoja mlangoni, akauliza nini? na kwanini kama mtoto wake amefariki mmemruhusu kuingia huku? wakamwambia kuwa nina watoto wawili, hivyo niliruhusiwa kuingia ili nikanyonyeshe aliebaki
Mungu wa ajabu jamani, yule Dr. akaingia hadi ndani na kuuliza yuko wapi aliekufa, wakamwonyesha, akamfungua shuka, kukuta katoto kanahema ila kwa mbaaaali kabisa, alicho kifanya na sitasahau alisema hivi
FUTA MACHOZI YAKO! MUOMBE MUNGU MTOTO WAKO NI MZIMA NGOJA NIMSHUHURIKIE, NISIKUSIKIE UNALIA HATA KIDOGO!, nilipata nguvu za ghafla nikasimama nikamfata Dk. nikamuangalia alichokuwa akifanya, alimuingiza mtoto puani mpira, akawa anamjaza hewa, gafla tumbo la mtoto likawa kubwaaaaa, akatoa ule mpira akamchukuwa mtoto wangu hadi kitandani akamuewekea mpira mwingine mdogo wa oxgen na kuniambia kila nikiingia kunyonyesha nihakikishe mpira uko pale pale puani, kisha akamuita yule nesi aliekuwa zamu na kuondoka nae, ambae sielewi ni action gani ilichukukuliwa juu yake, maana hadi naruhusiwa hospitali sikumtia machoni tena,
Kumbe pale alipokuwa amewekwa mwanzoni ni kwamba alikuwa akisubiriwa mchukuwa maiti aje azikusanye, hatimaye mwanangu aakawa mzima, huwa nikimuangalia simmmalizi, Mungu alinitetea sana, na nilisimama katika imani tu! nilikaa muhimbili mwezi mzima, lakini MUNGU WANGU NI MWAMINIFU hadi leo wanangu ni wazima kabisa, na nikiwaangali tu! huwa nafurahi sana, nawapenda mno, na siku ileile nilimsamehe yule nesi,
NA HAWA NDIO TWINS WANGU, TRACY & TYMON ni wazima kabisa
na hapo walipiga mwaka jana mwezi wa tatu walikuwa wanatimiza miaka mitatu,
wamesheaanza kusoma, basi huyo mtoto wa kiume nikimuangalia, Mh! namshukuru Mungu tu!
aisee pole sana dada!
ReplyDeletestory yako imenisikitisha sana, pole sana mdogo wangu, kumbe watoto wengi wanakufa kizembe sana, MUNGU NA AKUKUZIE WATOTO WAKO VIOLET
Nakusalimu katika Jina La yesu,
ReplyDeletePole kwa sana dada na hongera kwa kumngangania Mungu, wanawake kama wewe ndio wanaohitajika katika kungangania.
Mi ushauri wangu ni kumfanyia maombi ya ukombozi mwanao kwa ile roho ya mauti iliyotaka kumchukua.
Kwa kweli kama sio huyu Mungu, sijui nisemeje.Hongera kwa ushindi. Kumbuka kumsamehe na usahau maana Mungu anasema anasamehe na anasahau. jitahidi kumwomba Mungu akupe neema ya kusahau kibinadamu hutaweza.
Mh! Pole dada Violet, nimeumia as if ndo hicho kitu kinatendeka muda huu, kweli mungu ni mwema na tumshukuru kwa kila jambo. Endelea kuomba na kushukuru nami nakuombea mungu akukuzie katika maadili mema.
ReplyDeleteBinafsi sitasahau siku ambayo nilifiwa na baba yangu kifo cha ghafla, bila hata ya kuumwa wala nini. 02/04/2009, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina. Nilimpenda sana baba yangu lakini Mungu alimpenda zaidi.
Amanda
MOJA KATI YA MADA ULIZOPOST NI ILE YA KUSEMA JE MACHOZI NI SULUHISHO LA MATATIZO YA MWANAMKE? Mimi nilipinga, nikasema sio suluhisho
ReplyDeleteLAKINI KWA HII STORY YAKO YA LEO, Nimekubali kwamba machozi yanaweza kusaidia sana, JIULIZE
1. USINGELIA KWA SAUTI DOKTA ANGEKUJA KUMUONA MWANAO?
2. MCHUKUWA MAITI ANGEKUMCHUKUA MTOTO ANGEENDA KUFIA WAPI KAMA SI MOCHWARI?
3. ULIKUMBUKA KUMSHUKURU MUNGU??
4. NASISITIZA KUMSAMEHE HUYO NESI
nimejikuta natoa machozi Violet, watoto wako wazuri sana, wamekuwa, nimejaribu kumuangalia huyo TRACY, it means kwamba sasa hivi angekuwa peke yake, na hy angekufa pasipo mpango wa Mungu, KUMBE SOMETYMES KULIA KUNASAIDIA SANA
VIOLET NIMEHUZUNISHWA SANA, SIKUJUI NA WALA HUNIJUI, ILA NINACHOKUOMBA TU! KAMA HUKUMSHUKURU MUNGU JUU YA HILI, NENDA KASHUKURU HARAKA SANA! maana bila Mungu usingekuwa na huyo mtoto, kamrudishie shukrani Mungu,
kweli hata kama mimi nisingeisahau hiyo siku
NIMEUMIA SANA.
nimelia sana Violet kutokana na hii story yako,
ReplyDeletenimefikiria mbali sana, nimefikiria upweke ambao angebakia nao Tracy, kwani walishazowea kuwa wawili toka tumboni, nimelia hadi hapa ofisini wamenishangaa, nimejihisi ni mimi kabisa, Violet, MSHUKURU MUNGU MDOGO WANGU, pia nimejifunza kitu toka kwako,
NIMEJIFUNZA IMANI,
pole na hongera kwa kukuza mama, siku moja nikija dar ntakutafuta nimpatie Tymon zawadi,
nimeguswa sana. kwasasa niko UK
TASREEEN
Pole sana dada na hongera kwa kuwa na imani endelea kuamini kwa Mungu anatenda.
ReplyDeletePole sana Amanda kwa kumpoteza Baba, Mungu akupe nguvu,
ReplyDeleteWAPENDWA, HUWA napenda kuomba maombi ya kuweka NADHIRI, hivyo baada ya kutoka hospitali tu! nilitoa sadaka ya shukrani Kwa Mungu wangu
ASANTENI
Mungu akubariki sana mama T endelea kuwa ushuhuda katika maisha yako mshike sana yesu ng'ang'ania sana imani endelea kuwafunika watoto wako kwa damu ya yesu ili adui asipate nafasi, Binafsi sitasahau kaka yangu mpenzi na rafiki yangu alipokufa katika Ajali ya basi la No Challenge maaneo ya msangazi muheza walikufa basi zima lakini ukiangalia maeneo waliofia kama ilikuwa nguvu za giza akaacha mke mjazito baaba ya siku ishirini mtoto akazaliwa, huwa nikikumbuka kifo chake huwa naumia sana nikikumbuka mazishi yake tulimzika akitoka damu puani masikioni mdomoni huwa inauma lakini namshukuru mungu katuachia binti aitwae Witness yuko darasa la sita sasa lakini mungu ni mwema kila anachokifanya kwetu ni chema kabisa, Ila ninachojua mungu hakutuimbia misiba wala huzuni, mungu ni mungu wa furaha amani, na ushindi.basi dada v nakupa kamstari zab 105:1-5
ReplyDeleteMpendwa
POLE VIOLET
ReplyDeleteMIMI SITASAHAU SIKU NILIYOMKUTA MUME WANGU WA NDOA AMELALA NA HOUSEGILR WANGU KITANDANI KWANGU
sijui kwanini nashindwa kusahau japo nilisamehe, nilimkuta mume wangu live na housemaid wetu, tena nilikua natoka safari, nilifiwa na mjomba wangu, nilipata lift na kurudi nilitaka kumfanyia suprise, nilichokikuta
mh! najuta mwenzio, sijui kama nitakuja kusahau, sijui
KAMA NI MIMI HUYO NESI WALA SIMSAMEHI,
ReplyDeleteLAZIMA NINGEMKOMESHA!
WE! ANIULIE MWANANGU HIVIHIVI, UNA MOYO DADA
Kusamehe mpenzi wangu ni lazima lazima usamehe ili mungu aweze kukupigania na kuingilia kati mambo yako usipomsamehe nesi wewe ni mangapi umefanyia wenzako au kwa mungu mbona mungu amesamehe, kama huna mungu hutasamehe, lakini kama una mungu utasamehe kwa mungu kuna msamaha ili mungu agopwe bwana angehehesabu maovu nani angesimama
ReplyDeletempendwa
Pole sana mama Tracy,yn wakati nasoma nlihic km ndo naona picha yenyewe,inackitisha sana,pole mumy.ASIA ALAWI
ReplyDeletePole sana inatia simanzi!
ReplyDeletePole sana yaani sina hata lakusema, mshukuru Mungu,
ReplyDeletepole sana rafiki,inabidi utumie busara sana kumlea na kumpenda zaidi,na uache tabia ya kumpipiga zaidi usiwe mkali saaaana kwa watoto boazy hapa
ReplyDeletehahaaaaaaaaaaaa
ReplyDeletewewe boazy wewe,
mh! ndio unanipaka??? kichapo lazima kitembee tu! na wananijuwa, sitaki ujinga, wakikosea mara ya kwanza nawaambia, mara yapili kichapo,
ahhahahaaaaaaaaaaaaaaa, mtoto asionywa kwa kiboko, hata tabia zake zinakuwa haziko katika mstari, mii mwenyewe nilichapwa sana tu!