Jamani, nina shida kubwa sana, ambayo hata sijui kama nitakuja kuepukana nayo, na kwakuwa mficha uchi hazai, nimeona niseme ili nisaidiwe, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27, nimezaliwa na kukulia UK, ambapo ndipo alipokuwepo mama yangu, baba alishafariki wala sikuwahi kumuona
nilipomaliza elimu ya secondary nilikuja tanzania kwa aunti zangu ambao tunaishi nao hapa Mwanza, Nilikaa kwa aunt zangu, wakati nikiwa kwenye process za kutaka kurudi kwa mama, bahati mbaya mama yangu alifariki, hivyo sikuweza kurudi tena kule, na kuamua kubaki tanzania kwa ndugu wa mama yangu
hapo nilikuwa ninamiaka 23, nilifanikiwa kupata kazi airport, nilifanya kwa muda wa mwaka mmoja tu, nikapata mchumba, ambae alinipenda sana, na aliahidi kunioa, basi nami nilimpenda sana, nilimtambulisha kwetu akajulikana, na kwao alinitambulisha, kabla ya kufunga ndoa nilipata ujauzito, ambapo familia yangu iliamua nizae ndipo nifunge ndoa, ikawa bahati mbaya, kabla yakujifungua nilipata kifafa cha mimba, hali ambayo ilisababisha mwanangu afariki,
nililia sana, tokea pale mchumba wangu akasafiri kwenda kusoma, na kudai nisubiri arudi ili tufunge ndoa, ajiandae vizuri, nilikubali, lakini aliposafiri tu! mawasiliano yalikufa, wakwe zangu wakaanza kunidharau, nikienda kwao nikama mzigo, hali hii ilinisumbua sana, kwakuwa nilimpenda sana mchumba wangu, nimekaa mwaka mmoja, nikapata taarifa kwa watu kuwa mchumba wangu anao, na vikao teyari,
niliumia sana, nakumbuka nilikunywa sumu kabia, mama mdogo aliniwahisha hospitali, nikapona, sasa tokea hapo, mimi sikuwa nikitaka mwanaume wa kunioa, wachumba walikuja niliwakataaa, nikawa kama niliechanganyikiwa vile, sasa hali ile hadi leo nikikumbuka, nalia sana,
TATIZO NI HILI,
niliamua kuwa na boyfriend, ambae nae tulidumu nae kidogo tu, akaniacha, baada ya muda mfupi nae akatangaza ndoa na mwanamke mwingine, hapo ndipo nilichoka kabisa,
niliwadharau wanaume wote, waliokuwa wakipita mbele yangu, nikawa nalala nao hovyo tu, hakuna niliempenda, akinitaka nikimtamani tu! nalala nae, siku moja , ya pili nakuwa sihitaji kumuona kabisa, na simu yake naweza hata kudelete,
hadi sasa sijui nimefanya mapenzi na wanaume wangapi, NA SIWEZI KURUDIA KULALA MARA MBILI NA MWANAUME MMOJA, siwezi kabisa dada, yani kabla ya tendo lenyewe, nakuwa na hamu nae sana, nikimaliza tu! namchukia kupita kiasi,
dada, niko kama kahaba fulani hivi asijuwa muelekeo wake, yani napenda sana kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti, sio mmoja, familia hadi imeamua kunitenga, maana ninayofanya ni uchafu sana, nimepoteza muelekeo wa maisha yangu, nikaamua kuja dar es salaam, nikapata kazi hapa ........... napo hadi sasa toka nije sijui nimetembea na wanaume wangapi, kila atakaenijaribu tu! nammaliza, niko teyari kufata mapenzi hata mikoani, nikishafanywa tu! narudi natulia,
kipindi cha mwanzo nilikuwa naona sawa tu, nilijitambua kama mimi ni malaya, sikuwa tayari kupima hata ukimwi maana nilijuwa ninao, lakini cha kushangaza, kuna siku niliumwa sana nikiwa geto kwangu, rafiki yangu alinishauri twende hsptl nilikataa kabisa, baada ya kuzidiwa sana, nikasema liwalo na liwe, nikapelekwa hospitali, katika vipimo walivyopima, damu yangu ikawa iko safi, sikuamini kabisa, hapo hapo niliona nimepona, nikawa na malaria tu!
baada ya miezi mitatu nilirudi kupima tena, nikakutwa safi, hadi sasa idadi ile ya wanaume imeshuka sana,
lakini mbona naona nateseka sana? nakuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi, hadi naota kabisa nafanya mapenzi, hali hiii inanipa shida, sijui kama inatibika, natamani kuwa mtu mwenye heshima, natamani kurudisha heshima niliyoipoteza, natamani kurudi na kuanguka kwa ndugu zangu ili wanipokee upya, ila sijui kam nitaweza nimeshazowea, nisaidieni walimwengu.