Habari
yako violet, nahitaji msaada wako sana juu ya hili, kuna mwanamke nimeambiwa
anatembea na mume wangu, huyo mwanamke namfahamu sana, ila sina mazowea nae, sasa nimeambiwa ndio
anaemzuzua mume wangu, hasikii wala haelewi chochote.
Yani hataki kuambiwa
lolote lile, maisha yetu ni ugomvi kila siku, kitandani hatuna ushirikiano
wowote, kila mtu analala kivyake, nimejishusha kiasi cha kujion mjinga, nimezaa
nae watoto watatu, wa mwisho ana miezi kumi.
Naomba sana unisaidie mawazo,
ushauri………
Pole dear, mi nakushauri usichukulie hasira! Ongea kwanza na mumeo kabla ya kumface huyo dada. Muulize mumeo anakosa nini kwako hadi anaamua kukufanyia hivyo. Najua ukiongea naye utaujua ukweli wa mambo na itakusaidia. Unajuwa wanaume ni kama watoto hivyo unatakiwa uwe hekima ya kuamua jambo.
ReplyDeletePole sana bibie. Najua uchungu unakujiria.nakuomba kwanza tuliza akili yako.Weka mambo yako vizuri kwa utulivu halafu nenda na hilo jambo taratibu ukiwa unafanya utafiti zaidi wa kumnasa mtegoni na hapo utakuwa una ushahidi wa kutosha kumhukumu kwa lolote.Usije ukawaka hasira na mtu ambaye unaambiwa tu huna uhakika.Inawezekana si huyo bali kuna mtu mwingine tu.Si unajua umbea wa wabongo wanaweza kumsakizia mtu aidha kwa sababu siku moja walimuona akicheka naye aliambatana naye mahali fulani.Kaa kimya kama vile hakuna jambo huyo mumeo atajisahau na hapo ndipo utamkamatishia.
ReplyDeleteNATAFUTA MDADA MZUUUURI TUPEANE PENZI TAAAAAMU! 0654389929
ReplyDeleteKumbe umefanya kuambiwa, mimi nakushauri usipende kusilikiza maneno ya watu subiri ushuhudie mwenyewe ndio umtuhumu huyo mumeo kuwa kuna mwanamke anamzuzua, lakini usikurupuke tu nakuanza kuzua mambo mengine , utampoteza mumeo bila sababu ya msingi . by D
ReplyDelete