Wednesday, June 27, 2012

AMANI IMETOWEKA NDANI YA NDOA YANGU- TUNAISHI MRADI SIKU ZIENDE, SASA HALI HII HADI LINI?????


Naomba ushauri  kwako dada violet  na wadau wengine, Mimi ni mke halali wa mume mmoja na watoto wawili, ndoa yetu ina miaka kumi sasa,  ugomvi huwa haukosekani ndani ya nyumba, lakin naona kwangu imezidi, mume wangu amekuwa na dharau kupita kiasi, hanijali mimi wala familia (watoto)..  yani upendo wake ni wa kubeep
 
Ananichosha tunapokuwa kitandani, yani  imefika kipindi inapita hata wiki tatu au nne bila kugusana kimwili, na kama nikihitaji  inachukuwa muda sana hadi kukamilisha tendo, hisia zake zinakuwa mbali sana na mimi, yani in short simuelewi huyu mwanaume… watu wamenishauri nimdharau tu! Lakini mimi dharau siwezi, naumia mno jamani, bora ukose pesa uwe na amani, kuliko uwe na pesa ukose amani, nishaurini wapendwa wangu



5 comments:

  1. Kama anashkwa hashkaman,kilichobak maombi au mpotezee ful,atajirud mwenyewe.

    ReplyDelete
  2. huo ni upopo nionavyo mimi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sikushauri kabisa utoke nje ya ndoa, kwani yawezekana unawaza ivyo. Unajua hawa wanaume wana silika ya kutamani tamani, yawezekana kuna alipopatamani panamzuzua. wewe kuwa mpole wala usimlazimishe asije dai umembaka, kuna wakati utafika atajishangaa mbona mke wangu simpatii haki yake na hanisumbui? antashikwa na wivu ambao utarudisha mapenzi yake kwako.Muhimu ifike mahali mlazimishane kwenda kupima na akikaidi jua pana hatari mbele yako jichunge eee dada

      Delete
  3. NATAFUTA MDADA MZUUUURI TUPEANE PENZI TAAAAAMU! 0654389929

    ReplyDelete
  4. VUMILIA DADA,KAZANA KUMUOMBA MUNGU ATAKUTETEA,,,,

    ReplyDelete