Hope uko sawa wewe pamoja na familia yako, naomba ushauri mimi ni mama mwenye mtoto mmoja baada ya uzazi nimeongezeka sana naomba unishauri nitumie njia gani ili niweze kupungua kwani hata mazoezi nimefanya lakini sipungui naomba kama kuna dawa za kupunguza uzito uniambie na wadau wengine wanipe ushauri nifanyaje ili niweze kupungua sipendi kupoteza mwonekano wangu wa zamani
(Mwenzangu, hebu tushaurini, naana sio huyo tu! hata mimi nimo, toka nijifunguwe tumbo limegoma kupungua, the days goes on utafikiri nakaribia kujifungua, tupeni mbinu za kutoa matumbo, kupunguza uzito, ili turejee maumbile yetu mazuri ya zamani, )
Mimi naijua program ya kupunguza uzito ambayo ni nzuri sana. Anayetaka maelezo zaidi namba yangu 0753 352464.
ReplyDeletehapa naona kuna vitu viwili mnavichanganya, kupunguza uzito kuna mazoezi yake, na kupunguza tumbo kuna mazoezi yake
ReplyDeletenikianza na zoezi la kwanza, kupunguza uzito,
1. JITAHIDI KUACHA KULA BILA MPANGILIO, KILA SAA WEWE UNAKULA TU! HUNA MUDA MAALUMU,
2. KUNYWA MAJI YA MOTO KILA SIKU LITA MOJA,
3. USILE VYAKULA VYA MAFUTA KAMA CHIPS, NYAMA NYAMA ESPECIALLY NGOZI YA KUKU
4. MATUNDA NI MAZURI SANA, NA MBOGA ZA MAJANI CHUKUCHUKU,
5. USIWE TOO MUCH RELUX, JITAHIDI UWE MTU WA MAZOEZI MAZOEZI AT LEAST MARA 3 PER WEEK
HII INASAIDIA SANA, NA KABLA HUJAANZA ZOEZ PIMA KWANZA UJUWE UZITO WAKO, BAADA YA MWEZI (ukishaanza zoezi) PIMA UONE KAMA UMEFANIKIWA KUPUNGUZA UZITO,
KUTOA TUMBO
1. Kunywa maji ya moto lita moja kwa siku
2. Fanya mazoezi ya kukata tumbo, yale ya kulala na kuinuka kila siku asubuhi kabla hujala kitu, na jioni kabla hujalala,
3. kama una mkanda, ni vizuri kuufunga wakati unakula chakula na usiulegeze, siku zinavyozidi kwenda unazidi kuubana kila unapokula,
mimi nilifanya hivi nikafanikiwa, ngoja nitawatumia picha ambayo niliipiga nilpokuwa na tumbo, na ingine niliyopiga baada ya tumbo kuisha, (ila dada Violet, sitataka sura yangu ionekane,
fanye ni mazoezi, na acheni kula kula hovyo, ikiwemo vitu vya mafuta
ReplyDeleteacheni kula mafuta mafuta, halafu violet, mbona mwili wako wa kawaida tu! unataka kuupunguzaje jamani, mie naona inatosha
ReplyDeleteJamani kupunguza unene ni possible ila tumbo, jamani tumbo. Mimi nimeanza kunywa glass nane za maji ya moto kwa siku. Zimenisaidia kutokuwa na njaa hivyo nimepunguza chakula. Ila asikwambie mtu tumbo bado ni issue pamoja na kufanya mazoezi yote daily (kuruka kamba na mazoezi ya tumbo)
ReplyDeleteNilichokuja ku conclude ni kuwa ukijifungua mtoto mmoja ni rahisi kurudi kwenye hali ya awali, lakini kuanzia wa pili na kuendelea, labda ukafanyiwe operation ya kupunguza nyama za tumbo Ulaya; maana nyama zimelegea hata ufanye mazoezi vipi hazitaweza kukaza kiivyo.
Kwa kuwa nime conclude kuwa tumbo langu halitakuwa same again; nimejifunza kujikubali. Nina mguu mzuri, napigilia kimin changu cha kishkaji, haku... bado naonekana nina mvuto maana ndo kilichobakia. Hizi skin top mmh imebidi nipige stop, kila nkivaa naona kama am three months pregnant.
ReplyDeleteTumbo la uzazi halina cha kula mafuta mafuta, linalegea hata useme upunguze weight, especially kama umezaa watoto zaidi ya mmoja. Kwa hiyo msipende kuwasema wake zenu kuwa viti moto au bia ndo zinawafanya wawe na vitambi. That is the price they had to pay for bringing those angles into your lives. Hivyo muwapende na msiwafanye wajisikie hawana mvuto tena
ReplyDeletetusivunjane moyo jamani, matumbo yanaweza kupungua kabisa, ni kujiendekeza kula hovyo tu! mimi nina watoto wangu watatu, lakini ukicheki tumbo langu utadhani sijawahi kuzaa, ni kwaajili ya mazoezi, tumbo limejaa mafuta, mfano halisi, hebu angalieni wazazi wetu, wote wana matumbo mazuri, wanazeeka na maumbile yao ya awali, na unakuta mtu amezaa watoto hata nane hadi tisa, lakini ni kwakuwa walikuwa wakijituma sana, ndio maana wamekuwa hivyo
ReplyDeleteFANYENI MAZOEZI KINA MAMA, INAWEZEKANA
Labda useme kuna wenye genes nzuri. Mi niko Ulaya na wanawake pamoja na kuwa na ma gym ni full vitambi. Kama dada una watoto watatu na una tumbo la kuvaa bikini mshukuru Mungu hayo ni maumbile. Mimi niko very careful na ninachokula, mfano sili kabisa white bread na nakula wanga kidogo sana. Maji kwa sana na bado tumbo langu haliko flat kama zamani.
ReplyDeleteKikubwa tuendelee kufanya mazoezi tuwe fit na tusizidi uzito tunaotakiwa tuwe nao. Ila kusema tumbo liwe kama mwanzo, mmh. Si wote.
Mm nahic kulegea kwa tumbo ni maumbile ya mtu jaman, laweza pungua kweli ila kulegea kuko pale pale mm naumia sna na hii hali.
ReplyDeletejamani kuwa na tumbo ni maumbile ya mtu, mi nimezaa mtoto mmoja kwa opeartion lakini tumbo langu ni kubwa kama nina mimba miezi 4.nishafanya mazowezi diet na kunywa maji ya moto kwa muda wa miezi mi 4 sikufanikiwa Ila nina shoga yangu yeye amezaa watoto wa 3 kwa operation, tumbo lake ni flat kama hajawahi beba mimba tena ni mnywaji wa bia na nyama choma mpaka namwogopa. na pia kuna mdada ninaye mjua hana mtoto wala hajawahi beba mimba ila tumbo limejitokeza na kumwaribu shep, kitu muhumu ni kujikubali jinsi ulivyo, tafuta nguo zinazoendana na shep yako na kama una mguu aaah utapendeza tu
ReplyDeleteKusema na ukweli wajameni, wanawake wa KIBANTU ni wowowoo na tumbo lazima hivi vitu vikimbizane kwa sana. Usemi wa mtu hapo juu kuwa ni maumbile ni sahihi. Hata wanawake wa kihindi wakishafikisha umri fulani na kupata watoto lazima tumbo lishuke. So mtapiga tizi mpaka mkomae sura lakini kijifriza pale pale! Ila fanyeni mazoezi kwa afya zenu msiacha bana!
ReplyDeletejamani msikatishe tamaa wa kina dada,tumbo linaisha ukidhamiria,punguzeni misosi,maji moto na matunda kwa wingi.vaa nguo zinazoenda na mwili wako utapendeza tu.
ReplyDeletematumbo ni tatizo jaman yan yanatesa sana ata muda mwingine unalosa raha tushauriane
ReplyDeleteraha sina na hili tumbo jamani najionea hadi aibu,kwani kama mjamzito vile looh
ReplyDeleteDah nivyema lakini kila mazoezi nafanya ila sipungui, huo mkanda ndio nitaupataje, coz mi mgeni
ReplyDelete