Pole na kazi dada Violet mimi ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini ninasumbuliwa na tatizo la kuota kinyama sehemu ya haja kumbwa kuna siku nyingine kinauma sana kinyama chenyewe ni kidogo sana ninaomba ushauri nifanye nini ili tatizo hili liweze kuisha kwakweli silifurahii
, kina muda kama miezi mi tatu na hakikui ni kidogo sana kama kipele na wala hospitali bado sijaenda.
Ukifanyiwa operation maumivu yake ni makali mno maana unakuwa huwezi kula kitu kigumu ,hata uji ukinywa ukipata choo maumivu yake hayaelezeki sababu lazima utoneshe kidonda.baada ya operation maumivu yatapotea mpaka utasahau lakini baadaye tena vitaanza kuota tena.Mimi nilifanyiwa baada yakuona maumivu hayavumiliki lakini nilikaa kama mwaka nikaanza kuvisikia tena,mambo yamekuwa yaleyale,ni ugonjwa unaotesa mno.Mitishamba ndiyo tiba yake sahihi, vinapotea moja kwa moja.
ReplyDeletehayo maumivu ni makali mno huwa yanakuja kwa kipindi halafu yanapotea,kinyama kinakuwa taratibu baadaye itafika sehemu maumivu ni makali mpaka unapiga kelele chooni na damu inatoka mpaka sinki lote linakuwa halifai utashangaa hiyo damu inatoka wapi bila kupata jibu.Pole sana ugonjwa huo ni mbaya sana.
ReplyDeleteNenda hospitali kwani yawezekana kuna kingine hata kwa ndani kwani wewe mwenyewe huwezi jua. Ni tatizo ambao linajulikana kitaalamu na uwapata sana sana wamama waliojifungua. Nenda hospital watakusaidia tu kwa dawa au operation depending on how serious it is. Wahi mdogo wangu
ReplyDeletehuu ni ugonjwa,una jina lake la kitaalam.wala usiogope kwenda hospitali.dawa yake ni kukatwa.mimi nilishakatwa,ila hayo maumivu yake ni makali mno.mara nyengine uvimbe unarudi.madaktari wanasema ni vizuri kujaribu kula vyakula laini ili choo kiwe laini.saa nyengine,magonjwa kama hayo,husababisha kansa ya haja kubwa,bora tiba ya mapema,kuliko kuacha kwa kuhofia kuogopa.vivimbe vingine,vikiachwa miaka na miaka,husababisha kansa,huko ndio kubaya zaidi
ReplyDeletewahi hospitali mdogo wangu, Mungu atakusaidia utapona, maana ulivyoandika unaonekana una mateso sana, au wewe dada uliesema kuwa ulitumia miti shamba, kwanini usitoe namba yako ya simu ili huyo dada akutafute umsaidie??? au mtumie hata huyu mwenye blogu, beautytouch kama unaona utasumbuliwa ukipublish, msaidie mwenzitu
ReplyDeleteNenda hosp kaka yangu aliumwa akapewa dawa kikapona bila kukatwa, ni ugonjwa unajulikana sikumbuki jina ni gumu, alienda tumaini hosp akamuona DK KAPONA(hilo ni jina)
ReplyDeletehi!! pole saana huo ni ugojwa wa kawida tu unaitwa Anal piles a.k.a Anal fissure a.k.a Hemorrhoid unatibika hosp kuna njia nyingi za matibabu yakwanza ni dawa kama vile Anu suppositories na kama itashindikana hali yake ikawa mbaya zaidi basi a surgical option inaweza kufanyika NB; kuwa makini saana na aina ya chakula na life style unayoishi hivi ndio major factors za kuleta hii hali na hata occupation ni Risk factor nakutakia kila la kheri kwenye kutafuta tiba i hope siku moja utakuja kutuambia kuwa umepona !!
ReplyDeleteYeah,huu ni ugonjwa wa kawaida,sema unatokea sehemu ambayo ngozi yake ni laini sana. Unaitwa Hemorhoids au Anul Piles. Ukienda hospitali watakupa dawa kama ANUSOL SUPPOSITORIES na zingne mbadala wake. Ni ugonjwa wa kawaida kabisa. Kinga yake ni kula vyakula vyenye kambakamba au fibres,na kuwa makin na Bowel Movement,namaanisha uckae sana chooni. Pia ucpende kukaa kitako. ANUSOL ipo kwny blister kwa hiyo asubuh unaingiza kwny njia ya haja kubwa kimoja,jion unaweka pia. Unapoweka kinakwenda kama kimevutwa na sumaku. Ni ugonjwa unaosumbua hadi Marekani na Ulaya sana. Kwa msaada andika Hermorhoids utaona Online Doctors na wagonjwa wengi Wazungu wanavyouzungumzia. Richard Mugendi Francis.
ReplyDelete