Saturday, September 17, 2011

NAUMWA SEHEMU ZA SIRI, NIMETUMIA DAWA SIJAPONA NIPENI USHAURI

Pole na kazi dada yangu. Mimi ni mpenzi sana wa kusoma hii blog yako na nimefaidika na mengi juu ya hii blog yako. TATIZO langu ni kwamba nilipata infection/ maambukizi nadhani ni ya ugonjwa wa zinaa kutoka kwa mchumba niliokuwa nikamwamini sana

lakini kuna Siku baada ya kusex nae niliona kama maziwa yananitoka kwenye uume wangu hiyo ni kabla ya kukojoa. Nilienda hospitali siku hyo hyo. Docta aliniambia ni kisonono. nilitumia dawa ikaacha but ikarudia tena. Nilienda tena hospitali wakanifanyia culture and sensitivity wakasema hamna wakanitoa damu wakasema pia hamna lakini bdo tatizo lipo tu nikitumia dawa linaacha baadae linarudia na kwa sasa ule ute unazidi kuwa mzito inakuwa kama chai ya maziwa hivi au cream ya njano isiyo kolea.

Nahitaji msaada wa haraka sana naomba hta mtu nipe namba yke kama anaexperience na hicho kitu. au labda kuna doctor atakaeweza kunitibu, hali hii imeninyima raha sana. hadi sasa, yani sijielewi, Huyo msichana nilishatengana
nae siku ileile nimechanganykiwa plz nisadien huu mwez wa 3 sasa




Sunday, September 11, 2011

MZAZI, MUDA GANI UNAKAA NA WATOTO WAKO NYUMBANI??




Swali hili ni la msingi sana kwa mzazi anaejali mtoto wake, wazazi tumekuwa busy mno, kiasi kwamba tunawasahau watoto wetu kabisa, kuna kipindi kiliwahi kunikuta mimi nikitoka saa 12 naenda kazini naacha wamelala, nikitoka kazini naenda chuo, narudi home saa mbili na nusu au saa tatu nakuta wamelala, yani ilinipa wakati mgumu sana,sasa naamini hii inatokea na kwa wengine pia kutokana na shughuri tulizonazo, muda umekuwa upo pale pale ila majukumu ndio yametuzidi


Nawakumbusha tu! Wazazi wenzangu siku tunazokuwa na muda, lets say ni weekend, tukumbuke kuwa karibu nao sana, tuwadadisi kiundani sana kujua mawazo yao, michezo yao na hata mahusiano nao na dada zao (mahousegilr) tuangalie homework zao, tukague madaftari yao, kwa kufanya hivi tutagundua vitu vingi sana, ambavyo wamejitahidi, au wanahitaji msaada zaidi


 nilichogundua kwao hasa kwa hiki kipindi ambacho niko rikizo ni kwamba wanapenda sana kila kitu niwafanyie mimi, mfano wakiamka tu! wanakuja chumbani kwangu moja kwa moja, na kunitaka mimi niwaandae, na sio dada tena, so namwambia dada endela na kazi zingine, ngoja niwahudumie mimi. basi wanafurahi sana, nikimaliza kuwapa chai, wananiambia mama utupeleke hadi shuleni kwetu, kwakuwa sio mbali na nyumbani, basi nawasindikiza wananipa mabegi yao niwabee, yani wanaenjoy kupita kiasi, hata kwa kuwa namimi kwa dakika chache tu!


Tusiwaamini sana wadada wa kazi, coz wao sio wazazi, ni wachache sana wanaofanya exactly like mother, but mmmmm… bado kama mzazi especially mama, unahitaji kuwa karibu na mtoto sana, ukiwa na mtoto ambae sio muoga atakufanya ujue vitu vingi vinavyojiri nyumbani wakati haupo, mfano tracy wangu, kila kinachojiri nyumbani hasahau,  ukirudi tu! Kama akiwa macho anakuelezea, naanza kumfanya rafiki yangu tangu akiwa mdogo, ili asiniogope bali aniheshimu  na awe wazi kwangu, maana kumkaripia sana kunampotezea confidence kabisa, anahisi kila atakachofanya atafokewa, so nivizur sana kusoma tabia za watoto wetu INAPOBIDI KUWA MKALI, KASIRIKA NA MTOTO AJUE NIMEMUUDHI MAMA AMEKASIRIKA, LAKINI ISIWE NONGWA, KILA SAA UNAKASIRIKA MTOTO ATAKUCHUKIA


Weekend hii nimekumbuka kugusia watoto, naona limekuwa ni tatizo kwa baadhi ya wamama,  siku ukipata nafasi, andaa chakula cha watoto wako wewe mama, dada nae apumzike, angalia walipohifadhiwa nguo zao za kushindia, angaliwa walipolala kila siku, kagua kabla hujalala,  je vyandarua vyao ni salama? Kagua kucha zao kila weekend, kata ziwe fupi, yani atleast uwe na hata nusu siku kwa ajili yao,



Kweli nawaambia mtoto hujiskia fahari sana anapokuwa na wazazi wake, baba au mama au wote, japo watoto wengi wameegemea sana kwa mama, hawataki utoke, ukitembea nao wanajiskia raha sana,

 
KWENU WAZAZI NATAMBUWA MNAFAHAMU WAJIBU WENU KWA WATOTO,  BUT WENGI WENU MNAJISAHAU SANA KUTOKANA NA SHUGHURI ZA KILA SIKU, NAJARIBU KUWAKUMBUSHA TU,  JINSI TUNAVYOLEA WATOTO WETU, NDIVYO WATAKAVYOKUWA KUWA,

KIKUBWA NA CHA MSINGI, PAMOJA NA UBUSY TULIONAO TUSISAHAU KUWAOMBEA KILA SIKU, ILI MUNGU AENDELEE KUWALINDA KWA KILA KITU

NAWADORISHIA NYWELE ZANGU


MWANAMKE NYWELE BWANA, MAWEAVING KILA MARA YANACHOSHA NA JOTO HILI LA DAR

SIO WEAVING WALA NINI

Add caption

KWA NYUMA

NIKO NA AUNT WANGU CAREEN, NATAMANIA KWELI KAKUWE ILI NIKASUKE


Friday, September 9, 2011

MTOTO WA MUME WANGU ANANIFANYA NITAMANI KUIKIMBIA NYUMBA YANGU- NISAIDIENI

Mimi ni mama niliolewa miaka mingi iliyopita, nilimkuta mume wangu ana mtoto mmoja ambae ni mdogo sana, mama yake alikuwa amefariki ndio nikaolewa mimi,
Nilimlea Yule mtoto kama wa kwangu mwenyewe, nilimuhudumia na kumpa mapenzi yote ya mama, nami mungu akanijalia nikapata mtoto mmoja wa kiume,

tatizo ni kwamba huyu mtoto wa mume wanguameshakuwa  yuko form four sasa hivi,lakini nilianza kumlea toka akiwa na miaka mitano,
Juzijuzi hapa nilihisi ni mjamzito, nikampima nikakuta ni kweli, iliniuma sana kwakuwa bado ni bint mdogo istoshe hata shule bado hajamaliza, nilimsema sana, cha ajabu baba yake toka kipindi hicho hadi leo hii hajasema chochote na binti yake kuhusu huo ujauzito, mbaya zaidi anamtetea kwa kila kitu kias kwamba Yule mtoto anaweza kunijibu vile anavyotaka, nikijaribu kumuonya anakuja juu sana, na baba yake anamtetea,

Natamani hata kuikimbia nyumba yangu, maana sielewi itakuwa hivi hadi lini, mtoto amekuwa mjeuri kupita maelezo, tena anasema kwanini wewe unifatilie fatilie wakati baba yangu anajua na hajasema lolote juu ya hili, wewe ndio una uchungu sana???
Sasa jamani mimi kama mimi sijui nifanye nini kabisa, tunaishi kama mtu na mke mwenzie yani ukikuta ananijibisha as if ni mdogo wake, naombeni  ushauri, nifanye nini mwenzenu??



Monday, August 29, 2011

POLENI NILIWAKIMBIA WAPENZI WANGU, NILIKUWA NA MITIHANI, SAFARI HII NIMEKAMATIKA BALAA

NAWAPENDA WAPENZI WANGU, NILIKUWA NA MITIHANI CHUO, LAKINI NAMSHUKURU MUNG SANA NIMEMALIZA MITIHANI SALAMA, NIMEBAKIZA MASOMO MAWILI TU AMBAYO NITAAZA MWEZI UJAO ILI KUMALIZIA COZI YANGU

ANAITWA ASHA, SHOST YANGU AMBAE TULIKUWA TUKIELEKEZANA KATIKA MITIHANI YETU





KAZI NA DAWA, HUYU NI MAMA YETU, TUNASOMA NAE, KWELI ELIMU HAINA MWISHO, NIKISOMA NA HUYU MAMA, TUNASOMA HUKU ANATUFUNDISHA MAISHA JINZI YALIVYO, KAMA UNAVYOONA ANATUBEBEA NDIZI, ANATUONYA, PH PSSS!!!! KWA UFUPI TUMEENJOY NAE SANA

NIKIWA BUSY UTANIJUA WEWE!,    ALL IN ALL, NAWATAKIWA WAISLAMU WOOOOTE EID NJEMA, 




Thursday, August 11, 2011

KUNA KINYAMA KIMEOTA SEHEMU YANGU YA HAJA KUBWA, KINANITESA SANA, NIFANYAJE???




Pole na kazi dada Violet mimi ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini ninasumbuliwa na tatizo la kuota kinyama sehemu ya haja kumbwa kuna siku nyingine kinauma sana kinyama chenyewe ni kidogo sana ninaomba ushauri nifanye nini ili tatizo hili liweze kuisha kwakweli silifurahii

, kina muda kama miezi mi tatu na hakikui ni kidogo sana kama kipele na wala hospitali bado sijaenda.

Wednesday, August 10, 2011

JAMANI TANZANIA YETU INA SEHEMU NZURI SANA ZA KUPUMZIKA,

TULIFIKA SEHEMU HII, KAMA MNAVYOONA WADAU
HEBU TAZAMA, UTASEMA MAMTONI DU!
HOTELINI HUKO HUKO UDZUNGWA
SEHEMU ZA UKWELI ( KWA WALE WA HONEY MOON)
KUSHOTO ANAITWA  BILL, EUNICE NA LILIAN, HUKO MLIMA WA UDZUNGWA
BILL AKIWA KATIKA POZI, MLIMANII,
FURAHA TUPU JAMANI, UKIENDA UTATAMANI USIRUDI
ISSUE ILIKUWA NDIO HIYO, LAZIMA UPANDE MLIMA
EUNICE AMECHOKA MASKINI, AKIFATIWA NA BILL, ABDUL & JAMES
STAFFS WENZANGU HAO, ALIECHUCHUMAA NI WAJINA MWINGINE (VIOLET)
HOTELIN
MANDHARI ZA UKWELI SANA,  TEMBELEA NA WEWE SWAHIBA WANGU, UTAENJOY SANA, YANI KULE HATA KAMA UNASTRESS ZAKO ZA MAISHA, PALE ZITAKWISHA KWA MUDA, YANI DU! NICE PLACE,

SAFARI YETU YA MIKUMI


SHOST UNA POZI!!!!!!!!
HOTELI TULIYOFIKIA INAITWA GENESIS, KUNA SEHEMU WANAFUGA NYOKA, KWA AJILI YA WATALII, NYOKA WA KILA RANGI, WALIOKWENDA KUONA WALIKWENDA, MIMI SIKUTAKA HATA KUJARIBU KUWAONA LIVE, NILIBAKI NJE NASISIMKA, MAANA MH!
NILIJIDAI KUWAONA KUPITIA PICHA TU! KAMA HUYU NI WA KIJANI
LILIAN ALIJITAHIDI SANA INGAWA ALIKUWA NA HOFU, LAKINI HADI KILIELEWEKA AKAPIGA PICHA NA NYOKA KAMA UNAVYOONA MDAU WANGU
HAHAHAA, MICHEZO ILIKUWA MINGI, TULIRUKA KAMBA,  HAPA WALINIKUMBUSHA MBALI SANAAA,
NATOA MADOIDO KWENYE KAMBA, CHEZEYA MIMI WEWE, HAHAHAH UTALOWA
WAOOOOO, WAJINA WANGU (VIOLET) UMEPENDEZAJE MAMIII
TWIGA PIA TULIWAONA,

POLENI KWA KUWATUPA WAPENDWA WANGU, NILISAFIRI KWENDA MIKUMI (TEAM BUILDING)

TULIENJOY SANA DEARS, HAHHAAAA, KWA KWELI NILIONA KAMA MUDA NI MFUPI SANA, KWAKUWA HUKWENDA, SHARE NA MIMI PICHA HIZO,


LILIAN NA MIMI


EUNICE NA MIMI
MIMI NA WAJINA WANGU (VIOLET)
EUNICE, RAFIKI YETU TUMAINI, NA MIMI
JUU KAIBISA ANAITWA ELINAMI, KATIKATI MWENYEWE, NA DADA YETU ZAI
POZI ZA UKWELI, ITABIDI NIJIGUNZE, BUT MMMM!!!! SIJUI KAMA NITAWEZA, NAFIKIRI POZI ZINGINE NI ZA VIPOTABLE,, PENDEZA SANA WEWE