Habari violet,
Naombeni msaada wa
maawazo yenu, nimegundua kuna mwanamke anatembea na mume wangu, mume wangu
alikataaaaaa kwa mara ya kwanza, lakini baada ya kufatilllia na kuchunguza kwa
muda mrefu nikaja kuhakikisha ni kweli kabisa, mwanamke anaomba msamaha kwamba wataachana
na hatorudia tenaa, na mume wangu pia anasema hatorudiaa,
Nimeumia sana
mwenzenu, nimeumia kupita kias, kwakuwa nilimpenda, nilimheshimu, nilimjali
sana mume wangu, nilikuwa teyari kumuachia yeye kila kilicho changu,
nilimsikiliza sana, sikutegemea kama atakuja kunitenda hivi, imekia kipindi
najuta kwanini niliolewa nay eye,
sikutegemea kabisa kutokana na muonekano alio nao,,, details zoote za
huyo mwanamke wake niko nazo, niliomba niprintiwe kupitia mitandao ya simu
wanayotumia, niko nazo mkononi, staki kuamini, ninalia kama mtoto mdogo, ni
bora niibiwe pesa nitatafuta, kuliko kuibiwa penzi,, nitalipata wapi,,
Nimechanganyikiwa,
nataka kuondoka kwenda kwetu nikapumzike, nimwache kwanza, maana kila nikimuona
Napata hasira natamani kumkaba kabisa, nimemchukia mno,,, sina amani ya kuwa nay
eye, hali hii hadi lini?? Nifanyaje?
pole Sana dear, wanaume sijui hata sijui wakoje jamani, kwanini huwa hawatulii na wake zao? hata hivyo nakupa hongera sana kwa kuwa mfatiliaji mzuri, nahisi mimi ningejua ujinga huo kwa mume wangu, ningemmwagia tindikali usoni nimuharibu kabisa, na ningefanya juu chini kutafuta anapoishi huyo mwanamke wake, nae ningeharibu sura yake iwe fundisho na kwa wengine,,, pole sana
ReplyDeleteDada pole sana!!nakushauri msamehe tu mama yaishe na uendelee kutulia maana hata ukiondoka bado hutakuwa umetatua tatizo.Kaa naye mweleze jinsi ulivyomwamini na kumjali na jinsi alivyokuumiza kwa kukufanyia ujinga huo.Pia muulize kama kuna upungufu wowote anauona kwako kiasi cha kukukimbia kwenda kutiana na huyo wa pembeni.Mwisho mpe onyo kali sana na hatua utakayochukua akiendelea na tabia hiyo.Mungu akutie nguvu mama.
ReplyDeletePole mpenzi wangu ,hata mimi imeshanitokea. Maumivu yake hayasemeki ! Pole sana.
ReplyDeletePole sana, Sidhani ukimuacha mumeo ndo itakuwa suruhisho,unaweza ukajifariji kwamba ukipata mwingine atakuwa poa zaidi ya mumeo kumbe ndo unajichimbia kaburi, jaribu kuongea nae mara kwa mara masuala yenu,mimi na mke wangu huwa tunaita "Makavu Live" eg.
ReplyDelete1: kuulizana ni kitu gani mumeo hakipendi toka kwako na kitu gani haukipendi toka kwa mumeo?,
2: kuna kitu ambacho umekosea/amekosea siku chache zilizo pita?
3: Unapenda nini mumeo akukufanyie nini kitandani unasikia raha kupita kiasi na Yeye anapenda umfanyie nini kitandani asikie raha.
Na chochote mtakacho ambiana hakuna kununa wala kukasirika wala kufikiriana vibaya, ni moja ya njia kudumisha penzi lako lisitoke nje.
Note:"Jasiri haachi asili" inategemea na tabia ya mtu.
pole dada kwa hayo majaribu usijali yatapita tu mwombe Mungu akupiganie jipe moyo utashinda jamani ushauri mwingine usipokuwa na akili unaweza ukaufuata kama huyu mchangiaji aliye sema angekuwa yy angemwagia huyo mume tindikali pamoja na huyo hawara hapa kabisa unaweza kusema unatatua tatizo kumbe unaongeza tatizo mtu unapopata tatizo usikurupuke kwa hasira na kujaribu kulipiza no hapana kabisa hasira hasara tena kubwa sana ambayo itakugarimu sana baadae wahenga walisema hasira hasara na majuto ni mjukuu umefanya vizuri dada kwakuwa mvumilivu japo unaumia mimi ushauri wangu kwako ni kukaanaye umuulize taratibu bila ya hasira usikie atasema ndipo utafute uamuzi wenye busara good luck
ReplyDeletemimi nakushauri mtafute huyo malaya huko aliko, kamtie adabu msenge huyo
ReplyDeleteusiondoke ,nakwambia inauma sana,ila msamehe ,najua ni ngumu sana ila itafika siku yatapoa tu na utasahau,kuna baba mmoja alionekana ni mtu na heshima zake,ila Mungu alipomchukua,ulikuja msururu wa watoto embu oana sasa,so ona hakuna mkamilifu hapa duniani,sali sana,omba rehema za Mungu,na hakika Mungu ndiye muweza.
ReplyDeleteTatizo letu sote kama Binadamu ni kuwa toka tumezaliwa tumefundishwa namna ya Kufikiri, kuhisi na hatua za kuchukua kutoka katika Akili zetu kiasi kwamba huwa tunaamini vitu vyote kuwa halisi wakati sio! Kwa kweli wengi wetu tuna akili za kupewa na ndio maana kwenye mahusiano ya kimapenzi na ilie taasisi feki ya Ndoa kuna matatizo mengi ya kujitakia kutokana na akili feki tulizopewa! Kwenye ndoa huwa tunadhani kuwa tunamiliki Mwili wa huyo mwenzetu mwingine kwa asilimia zote kwa vile tuu tunashiriki nae tendo la Ndoa kitu ambacho sio kweli! Ukweli mkubwa ni kuwa sisi ni kamili bila huyo Mwingine na tukianza kufikiri vizuri ndipo ambavyo tunaweza kujirekebisha na kuwa na Upendo halisi usio kuwa na masharti na wenzi wetu na hili suala la sijui umefumania au Mwandani wako anatoka nje linakuwa halipo au kama lipo basi halikuumizi kwani sasa Akili yako inafikiri kwa ukamilifu na sio kimapokeo! Anza kujitizama wewe kwanza kabla ya kumalaumu Mumeo na hakika utagundua mapungufu mengi uliyo nayo!! Nawasilisha...
ReplyDeletePole jaribu kushinda hasira ili ufanye maamuzi ya busara wanaume sijui wamelaaniwa kwanini hawatulii jamani
ReplyDeleteMasikini pole sana dada, nafikiri ni mchanga sana katika ndoa, na ndo maana unaumia sana sana, wanaume ndio walivyo mamy hakuna mwaume asiyechiti hata mmoja katika hii dunia asikudangenye mtu, kitnachohitajika, kwanza ni heshima akuheshimu, akujali, akupe mahitaji yote yanayostahili kupewa, so mamy come down first then msamehe na maisha yaendlee, najua ni ngumu kumeza lkn pls jitahidi, ukisema uondoke ndo kwanza utampa nafasi ya kuzidi kufanya maasi. jiulize mama yako na baba yako kama wako pamoja mpaka leo hii wewe ukiwa umri huo alivumilia mangapi mpaka wewe ukakuwa? mengi sana sema wazazi huwa hawaongei, do ndoa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu subra pia na kila mwenye kusubiri yuko pamoja na Mwenyezi Mungu na usisahau kumuomba Mungu akulindie ndoa yako
ReplyDeletejua kwanza chanzo ni nini. je ni wewe? ujirekebishe. kama ni tamaazake ajirekebishe.
ReplyDeletePole sana, nakushauri umsamehe kama ameomba msamaha kweli maana asilimia kubwa ya wanaume ndivyo walivyo, ila uwe nae makini tu, kwani kiukweli huwezi kumuamini tena kama ulivyomuamini kabla, taratibu utamgundua kama kabadilika kweli au bado anaendelea kucheat, kama ukiona kabadilika basi hata hayo maumivu yataisha taratibu, ila uwe makini na vitu unavyofanya sasa, ukumbuke kujiwekea akiba zaidi ili usije kuyumba inapobidi! usisahau kumuomba Mungu sana
ReplyDeleteusijali dada wala huna haja ya kulia hao ndio wanaume ambao tulipewa na hizo ndiyo changamoto za ndoa h una haja ya kulia
ReplyDeleteUsifanye mchezo kuchitiwa...watu tuko busy tunajenga nyumba/ndoa zetu, kumbe mitaani kuna manungayembe yamekalia kukodolea waume za watu...
ReplyDeleteNimekuelewa sana bi dada maana mimi niliwahi fanya fujo mpaka polisi ilihusika...ila kuwa mkorofi kuna work sometimes kuliko kujiliza liza....mpe hard time mmeo na hicho kimeo chake....undava undava...ila usiue mchafurie tu maana wengi wa hawa vimada ni ma girlfriend na wachumba wa watu sasa tafuta boyfriend wake mpasulie a to z...tafuta mchumba wake mpe ma evidence na mwambie amkanye huyo malaya.
Afu wewe home baada ya kumba makavu live mumeo ya kutosha anza kukaba mpaka penalty maana huyo malaya akitemwa na wachumba zake akawii kuongeza kasi kwa mumeo.
Mbona hawa wananume watatuua jamani. Hawajiulizi tuko wangapi kwenye hiyo network?????????????
mmmh pole sana bidada, mie kero za wanaume nilishazichoka sana tu, mie mume wangu nilishamgundua mambo yake, nilimkanya na kumueleza jinsi gani ninavyoumia vitendo vyake kama alisikitika au kuumia nafsini mwake anajua yeye ila mm nimeamua kumpuuza yeye na matendo yake simfuatilii kabisa. kwa sasa kazi kwake roho inamuuma anahic na date na mtu mwingine eti kisa simfuatilii anapokuwa out, na wakati mwingine anauliza eti simtafute ata kumpigia simu huko aliko. na mm nakushauri achana na mawazo ya kuondoka ww cha kufanya mjali kama mke anavyotakiwa kumfanyia mume wake, mambo mengine yapuuze tu na wala usifuatilie nyendo zake zitakuumiza roho na kukupa stress bure,mradi anakujali bac angalie jinsi anavyokutreat mambo mengine acha yajipeleke yenyewe!!!!
ReplyDelete