Monday, October 10, 2011

HOUSEGIRL WANGU ANA UKIMWI, NIMRUDISHE KWAO?AU NIENDELEE KUWA NAE

Mimi ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 3, nina mume wangu na tunaishi nyumbani kwao, bado tunajiandaa tuhamie kwetu, tumeamua kuishi  kwa wakwe kutokana na mume wangu kuwa na uhamisho mara kwa mara kutokana na kazi zake

Mimi nina duka langu la nguo Ilala, hivyo kwakuwa huwa nashinda huko ililazimu kutafuta mtu wa kunisaidia kulea mtoto, nilitafutiwa na mkwe wangu, kusema ukweli nilipomuona siku ya kwanza tu! Nilihisi kitu, kutokana na ngozi yake kuwa tofauti na mabakamabaka mengi sana, nikamdadisi sana , akasema huwa ana ugonjwa wa ngozi,

Nilikaa nae wiki moja tu! Nikaamua kumpeleka hsptl bila mkwe wangu kujua, nikamwambia naenda kumtafutia dawa ya ngoz, lakini tulipofika nilimuomba daktar ampime na ukimwi, alipima na kukutwa ameathirka,

Ilinipa wakati mgumu kumueleza, na ikabidi kumwambia mkwe wangu, alisikitika sana,alipomwambia huyu bint cha ajabu wala hakuonyesha hata kustuka, nikamuuliza ulikuwa unajijua kama umeathirika?? Akasema hapana, ila mimi nahisi amenidanganya. 

Lakini pia mama mkwe ananilazimisha niendelee kuwa nae eti thawabu nitapewa na Mungu, mimi binafs sihitaji kuendelea nae, siku niliyomwambia mama amrudishe hadi kwao akawaweke wazi wazazi wake, alikataa na kuniambia ameshamwambia mume wangu kuhusu hilo na mume wangu amekubali huyo binti aendelee kuwepo, kitu ambacho hata sielewi inakuwajekuwaje

Hadi hiv ninavyoandika mimi na mama hatuna mahusiano mazuri kwa ajili ya huyu bint, , na mwanangu nambeba naenda nae dukani kwangu, ninapoondoka na  mtoto mama anasema eti namnyanyapaa huyu binti nifanyaje jamani???


 

9 comments:

  1. pole dada, mimi binafsi nakushauri umrudishe kwao kutokana na hali yake, huwezi kujua the way anavyoweza kumkinga mtoto, ongea nae kwa ustaarabu sana, pia jua mtoto ni wako na sio mama mkwe, hivyo toa maamuzi wewe, usiache mkweo akuumizie mtoto,
    Pia jamii ielewe kabisa kuwa kumrudisha kwao sio kwamba humpendi, alkini unatazama hali halisi ya afya yake na mtoto, na wasichana wengine wajinga sana, anaweza akafanya kusudi kukuambukizia mwanao, nakuomba, achana na mawazo ya mama mkwe wako, MRUDISHE HARAKA SNA

    ReplyDelete
  2. makumbwa, madogo yana nafuu, ha! huyo mama mkwe anakupenda kweli??? kwanini aamue maamuzi ya kipumbavu hivyo? mwambie akae nae yeye huyo binti wewe utafute mwingine, mjinga mmoja huyo asikusumbuwe, kakuzalia mume hajakuzalia mtoto wako, hivyo yeye angekuwa na uchungu kama angekuwa anaelelewa ni mwanae, lakini sio mwanao wewe, FUMBUKA KIAKILI DADA, USITHUBUTU KUMUACHA MWANAO ALELEWE NA HUYO MTU, Tafadhari

    ReplyDelete
  3. ACHANA NA FIKRA MBOVU ZA HUYO MAMA MKWE WAKO, MIMI NAMUONA KAMA MJINGA TU! HAJUI KAMA BINADAMU TUNAPISHANA? ANAJUA HUYO HOUSEGILR ANAWAZA NINI?? JE AKIAMUA KUMUAMBUZZA MTOTO UKIMWI KWA MAKUSUDI HASARA ITAKUWA YA MKWEO AU YA KWAKO, ACHA UPOLE WA KIJINGA DADA YANGU/MDOGO WANGU, MWAMBIE HUYO MAMA YEYE NDIE AKAE NA HUYO BINT NA SIO WEWE, IKIBIDI HAMA KABISA HAPO UKAKAE PEKE YAKO, AH! IMENIPA HASIRA SANA HII

    ReplyDelete
  4. fukuzia mbali huko

    ReplyDelete
  5. Kwanza nakushangaa hata umepata wapi muda wa kuomba ushauri. Mimi ningekuwa nimemfukuza long time kitambo

    ReplyDelete
  6. usimfukuze kama mbwa jamani, wadau mnapochangia muwe mnafikiria kwanza, atamfukuzaje hivyo, cha msingi ongea nae kistaarabu mueleze hali halis ya kumtoa pale, kama una uwezo msaidie hata pesa kidogo ya biashara ili akaendeleze maisha yake huko, ila kwa kukaa nae hata kwangu hapana

    ReplyDelete
  7. nyie mnayesema fukuzia mbali na mwingine anasema sijui umepata wapi huu mda wa kuomba ushauri temee mate chini hujafa hujaubwa kama huna huu ugonjwa kwa njia moja au nyingine itakuwa imetoke japo kwa ndugu au jirani hakuna mtu anayependa kupata ukimwi bali inatokea kwa bahati mbaya haijalishi amepata kwa njia gani yoote ni bahati mbaya huyu dada aliekuja kuomba ushauri anautu sana angeweza kumfukuza bila ushauri lakini kwa sababu ya ubinadamu aliokuwa nao ameamua kuomba ushauri dada ulieomba ushauri pole sana kwa hayo majaribu kunamchangiaji mmoja naungana naye amesema usimfukuze kama mbwa kaanaye chini mzungumze na ikiwezekana mpatie hata kamtaji akaanzishe kibiasha chake huku akiendelea kusogeza maisha yake namshauri kama hajanza dawa aanze nakumtia moyo pia mwambie kupata ukimwi sio mwisho wa maisha wachana na watu wanaoongea kama vile wanamkataba na maisha ni hayo tu zungumza pia na mama mkwe wako mwabie humjanyanyapai huyo dada bali kutokana na huyo dada hana elimu kuhusu ukimwi anaweza akamwambukizia mtoto sio kwa makuzudi ila kwa bahati mbaya maana hajapata ushauri kuhusu ukimwi usikae naye mrudishe kijijni kwake lakini kwa nia nzuri tu

    ReplyDelete
  8. Pole sana,Naomba nipatie namba zako za simu au Email address yako kwa ajili ya msaada zaidi.Mama D.

    ReplyDelete
  9. mnh pole sana aunt kwa kweli mm nakushauri bora umrudishe kwao,huyo hakufai kukaa na mtoto wako mdogo,kuna wangapi watotto wadogo wameambukizwa ukimwi na mahouse girl kwa makusudi,aunt kua makini sana tena sana,wallah namuonea huruma huyo mtoto wako,kua makini ikiwezeakana hata kuhama nyumba.

    ReplyDelete