Monday, September 26, 2011

HAYA, KWA WALE WALIOHITAJI VITU NINAVYOTUMIA KATIKA KUJAZA,KUKUZA NA KUPENDEZESHA NYWELE ZANGU

Kwa leo ninawaambia ni nini na tumia, ila nitaandaa picha za hivyo vitu pia ili niwatumie wiki ijayo,
Dawa ninayotumia ni Olive Oil,  zipo za aina tatu, na zote ni bidhaa za olive, na ambayo huwa naitumia sana ni ile yenye picha ya mtoto kwenye box, ambayo ndani yake ina kikopo kidogo cha steaming


Natumia Avocado shampoo, ni nzuri sana, lakini hata kama utaikosa kwenye haya masalon yetu waweza tumia shampoo yeyote ile,  mradi nywele zioshwe na zitakate, na pia tutumie conditioner, baada ya kuosha na shampoo, conditioner inasaidia sana kulainisha nywele na kuzuia zisikatike wakati wa kuchana, ni muhimu sana kuwa nayo, kama kwenye masalon yetu hakuna, basi nunua kifumu au kopo lako then unakuwa ukienda salon unamimina kidogo unakwenda nayo,


Huwa natumia mayonise steaming,  hii pia ziko za aina mbili, kuna le kubwa kabisa ambayo ni white cream, na kuna kubwa kias ambayo ni dark cream, I mean cream iliyokolesa sanaaaaa,
Sasa hii iliyo koleza sana ndio huwa natumia, na ninaitumia kila wiki, yani kila juma pili lazima nifanye steaming
                                      
Baada ya kuosha nywele zangu toka kwenye steamer kabla ya kupaka pinki lotion na kuanza kuseti huwa napaka kwenye ngozi ile steaming iliyopo ndani ya dawa,  naipaka kwenye ngozi tu! Kisha inachanganywa, halafu ndio unapaka pinki lotion kiasi tu(hii haioshwi, unasetia
 

Baada ya nywele kukakuka huwa natumia Blue magic chafu, wenyewe wauzaji wanaita blue magic ya chenga, inapakwa kwenye ngozi, na juu, kama ukikosa tumia hata Venus, but  blue magic ni nzuri zaidi naona inajaza sana nywele, inalainisha, na kuzifanya zikae wiki nzima zikishine, coz mimi huwa nikipaka jumapili sipaki tena hadi jumapil ingine na nywele huendelea kulegea na kubaki katika mvuto wake

HIVYO NDIO VITU NINAVYOTUMIA KICHWANI KWANGU

ADDITION

1.     Usisubiri harusi au sikukuu ndio uende salon, jitahidi kila wiki, au kama utashindwa basi atleast mara mbili au tatu kwa mwezi

2.     Kata ncha za nywele zako kidogo kila baada ya miezi miwili unapotoka kuretouch

3.     Usisuke nywele siku chache baada ya kuretouch, utazikata,  acha ziotee kwanza ndio usuke,

4.     Usifumue nywele kama unagombana, fumua taratiibu, kama umesikuka kimasai basi ikibidi chambua nywele moja moja kwa kutumia sindano,

5.     Usipende sana kutumia loterbody au jerry, hii inakata sana nywele labda kuwe na sababu maalum ya kufanya hivyo, lakini, mh! Sishauri sana
6.     Kwa wale wapenda rangirangi kama mimi, unapoweka breach, usifikishe kwenye ngozi, (shina la nywele) breach inapakwa kwa juu tu!

7.     Pia wale wa kutong, ni nzuri sana kutong kwa kutumia rolas au mabomba ya mipapai au mirija ya juice, lakini kutong kwa kutumia mashine, sio kuzuri sna  sababu mashine inaunguza nywele, 

8.     Usiwejiweke dawa mwenyewe kama sio mtaalamu au usimpe mtu asielewa namna ya kuweka dawa , atafanya zikatike, that’s  whay unashauriwa kwenda salon,


Kuna uwekaji wa aina mbili,
a)     Kwa wenye nywele nyingi na kavu hadi juu, unaporetouch anza chini, then katika kuchanganya apake hadi juu ili kulainisha zile za juu, 


b)    Kwa wale wenye nywele chache, na laini, unaporetouch usifikishe dawa juu utazimaliza, weka dawa chini tu! Kule kuliko otea, na kama ni chache halafu kavu, basi rambisha kidogo kwa juu dakika kumi au 15 kabla ya kuosha,
c)     Jitahidi unaporetouch usiwe na Mba nyingi kichwani, maana zinasababisha kuungua sana na kung’oka nywele kutokana na majeraha,

PAMOJA NA VYOTE HIVYO, NYWELE ZINAHITAJI USAFI SANA, ILI ZIPATE NAFASI YA KUKUA VIZURI, HATA KAMA UMESUKA UNAWEZA KWENDA SALON UKAOSHA NA KUKAUSHA, HIZO NYWELE ULIZOSUKA
HIVI  NDIVYO NINAVYOFANYA MIMI KWENYE NYWELE ZANGU, BUT KAMA NILIVYOWAAHIDI WIKI IJAYO NITAWATUMIA PICHA YA HIVYO NINAVYOTUMIA ILI UVIONE,

4 comments:

  1. waooooo, nice hair dada, ila nimejifunza kitu, kwamba lazima utenge muda kwa ajili ya nywele zako kila wiki, aisee una nywele nzuri sana dada, yani hadi nimekutamani, zimependeza sana
    hiyo picha ya mwisho nilijua ni weaving (salsa fupi) kumbe ni nywele zako, dear, ngoja mwezi huu nianze rasmi, nikifanikiwa nitakwambie, ila usisaha kututumia picha za hizo product zako,
    JEMIMA,

    ReplyDelete
  2. Teh teh teh, violet umenichekesha sana, unatushauri huku unatupa madongo, eti sio tusubiri hadi sikukuu ndio twende salon, uminigusa kweli, yani mimi kwenda salon m! kwa mwezi mara moja, ila mungu akubariki kwa maelekezo yako haya, nitajitahidi niyafatilie, asante sana
    MDAU

    ReplyDelete
  3. shost hongera, kama ni nywele tu! umejaliwa, mimi ninazo ndefu sana, ila hazina afya, nifanyaje zijae, pia nasikia kusuka kunakuza nywele, na kujaza, ni kweli?

    ReplyDelete
  4. dada umebarikiwa na nywele nzuri hongera sana tunashukuru kwakutujuza kitu chakutumia nywele ziwezekukuwa vizuri dada mbona siku hizi hutuwekei tena watu wanaoomba ushari kwa matatizo mbalimbali kama zamani ilituweze kuwachangia mawazo?vipi tena mbona blog yako imekuwa kimya hakuna jipya tena yaani mimi ninavyopenda blog yako haipiti siku sijachungulia hata mara mbili au tatu kama kutakuwa na jipya mbona hivyo dada unatuangusha bwana jitahidi kutuwekea habari ni hayo ubarikiwe sana na kazi yako nzuri

    ReplyDelete