Hello Dada Violet,
pole na kazi na majukumu mazito ya kuielimisha jamii kwa njia ya mtandao
pole na kazi na majukumu mazito ya kuielimisha jamii kwa njia ya mtandao
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25 nimeoa hivi majuzi tu lakini mke wangu amekuwa akinieleza juu ya kusumbuliwa kwake katika sehemu za siri nimejaribu kumpeleka hospitali lakini hatujafanikiwa sasa hivyi nimjamzito sasa naogopa asije akapatwa na matatizo wakati wa kujifungua naomba unisaidie, labda wewe unaweza kujua au kufahamu dawa ambayo anaweza kutumia na isimdhuru mtoto tumboni.
Pia nimesoma katika blog yako nikaona kuwa kuna aliyekuwa na tatizo kama hilo akapata ushauri wa kukunua cream lakini sijaelewa cream ya aina gani kwani zipo nyingi.
haya, kazi kwenu wadau, mimi nawaletea then tunasaidiana katika ushauri, kaka yetu ameomba ushauri, tumshauri basi atumie dawa gani, na ningeomba kwa wale wanaoadvice dawa ya kutumia basi wataje na majina ya hizo dawa kabisa,
USHAURI WANGU
Kaka yangu Mpenzi kwanza pole kwa tatizo hili, ila kwakuwa umesema mapema, naamini kabisa litapata ufumbuzi, mimi nakushauri uende ukawaone maspecialist wa magonjwa ya wanawake kwanza, ukizingatia mke ni mja mzito anahitaji huduma za karibu sana,
yawezekana mlikwenda hospitali kucheki na hakikuonekana kitu, lakini lazima kuna tatizo thats why nimekushauri ujitahidi vile uwezavyo ukaonana na watu wenye utaalamu huo, ungekuwa upo hapa Dar, ningekuelekeza kwa Daktari specilist wa wanawake tu! nahakika angekuhudumia,
but huko huko ulipo pia unaweza tafuta madaktari wazuri na ukawapata, ni vizuri kufumbua tatizo hili mapema kabla hajajifungua. hata hivyo haya ni mawazo yangu, ngoja tusikie na wadau watatushauri nini.
(kwenu wadau, tumsaidie kaka yetu)
Maskini, pole sana kaka yangu, mimi nakushauri usitumie tumie hovyo madawa, kama ni fungs kila fungus wana dwa yake, nenda hospitali, serios, usimcheleweshe, ni risk kubwa sana mja mzito kuwa hivyo, itampa tabu sana wakati wa kujingunga, wahi hospitali mapema pleaseeee
ReplyDeleteKuwashwa kwa mtu mjamzito ni kawaida kwasababu ya hormonal changes in the body.Kwakawaida ni fungus lakini ni vizuri kumwona daktari wa wanawake kwa vile umjamzito. Ningeshauri pia kuvaa chupi za cotton na kubadilisha chupi mara kwa mara kwa siku, kwa vile wanawake tunatumia maji mara nyingi kwa siku tukienda haja ndogo na utakuta chupi inakuwa na unyevunyevu kwa utumiaji wa maji na huweza kusababisha bacterial activities. Pole dear lakini very simple solution dawa inapatikan. Take care
ReplyDeletekama hauko Dar tuambie uko wapi, usitupe jina lako wewe tujulishe ulipo ili tuweze kuona kama kuna madocta wazuri tunawafahamu labda wako huko na wakakusaidia, ila ushauri wangu n i kama alivyokushauri dada Violet uwahi hospitali
ReplyDeletenenda hospitali kaka, muwahishe ili asije akaumia sana wakati wa kujifungua, usitumie dawa hovyo, kama alivyokushauri dada Violet, mpeleke kwa wale madokta ambao wako kwa ajili ya magonjwa ya wanawake tu! hizi dawa za kutumia hovyo hizi, wala hazifai,
ReplyDeletepole lakini naamini mungu atakusaidia tu!
Kwa wajawazito ni kweli kuwashwa huwa inatokea ila sidhani kuwa ni wote. Azingatie usafi na anawe na maji safi whenever possible kwani toilet papers wakati tayari ana muwasho zaweza zidisha. Ila nina imani kila ugonjwa una dawa, nenda kwa specialist wa kina mamatamsaidia. Asithubutu kutumia dawa yoyote bila kuwa recommended na dk bingwa kwa sababu ya hali yake. Na general doctors ujuzi wao ni mdogo kwa masuala ya mimba nina mfano wa dada ambaye mimba ilitoka sababu ya dawa aloshauriwa kutumia na hawa general doctors, ila yeye alikuwa na malaria.
ReplyDelete