Mimi ni mama wa mtoto 1 nina miezi 6 tangu nimefunga ndoa, pia nina umri wa miaka 24. Tatizo langu ni kwamba simuelewi mume wangu kama kweli ananipenda au alinioa tu kwa sababu nilimzalia mtoto? Kwa sasa mi ni mama wa nyumbani nimemaliza chuo kikuu mwaka jana na mpaka sasa sijabahatika kupata ajira.
Kwanza mume wangu alianza kuwa ananifokea hovyo hata mbele ya wageni kwa makosa madogomadogo. Pia ni mwezi wa 3 sasa mume wangu amekuwa na desturi ya kurudi usiku wa manane akiwa amelewa au hata alfajiri siku nyingine na mara nyingi siku za weekend huwa harudi nyumbani. kwa kweli huwa naumia sana na mara nyingi huwa nalia na kusali peke yangu maana nikijaribu kuongea nae kumuuliza nini tatizo mbona unanifanyia hivi huwa ananijibu "unataka nisirudi kabisa au?" Naona aibu kuwaambia wazazi kuhusu hili maana ni muda mfupi sana tangu tumefunga ndoa.
Kuna kipindi nirijaribu kumshirikisha bestfriend wake labda kama angeweza kunisaidia kwa kumshauri rafiki yake ila cha kusikitisha nayeye akanitaka kimapenzi. Yaani sielewi maana somatimes nahisi labda mume wangu kalogwa
. Ila cha kushangaza ni kwamba mume wangu ana wivu sana na mimi kila mara anakagua simu yangu, hataki niende hata saluni kanisani kwenyewe naenda kwa kulazimisha ila huwa naona kama hafurahii. Sikumbuki mara ya mwisho mume wangu kwenda ni lini.
Kuna kipindi nilijaribu kuangalia simu yake kwa kweli niliumia sana kwani nilikuta kanisave 'mama com' na si 'wife' kama alivyokuwa amenisave mwanzoni.
Kwa kweli watanzania naombeni ushauri wenu maana naogopa naweza kuja kuambukizwa gonjwa la Ukimwi kwani mimi bado ni mdogo na bado nina ndoto zangu nyingi.
Nampenda sana mume wangu ila simuelewi kwa kweli. tumeishi miaka 3 kabla ya kufunga nae ndoa na hakuwa hivi alinipenda sana hadi watu na rafiki zangu hawakusita kuniambia jinsi alivyokuwa ananipenda. Natamani angeniambia nilichomkosea mume wangu kwani ninajaribu sana kuwa good wife but he never appreciate it.
Tafadhali naombeni ushari wenu watanzania wenzangu.
HI
ReplyDeletePOLE KWA MAUMIVU UYAPATAYO ILA KWA HATUA ILIFIKIA SIO NZURI JARIBU KUWASHIRIKISHA WAZAZI AU HATA HUYO MSHENGA WAKE ILI UJUE KOSA LAKO NI NN SABABU UJUI HUKO ALALAPO UWA ANALALA NA NANI NA KIPINDI HIKI MARADHI NI MENGI MNO SO ENDELEA KUMUOMBA MUNGU USISONONEKE KWA KUSEMA NDOA YAKO NI CHANGA WAKATI UNAUMIA NDANI KWA NDANI SIVYO WATU TUISHIVYO NA KUMBUKA UNA MTT MDOGO ANAHITAJI FARAJA YAKO JE UNAPOKUWA NA MAWZO MENGI KIASI HICHO KWA KITAALAM MAZIWA YANKUWA HAYATOKI YA KUTOSHA SO LIFIKE ILI SWALA KWA WAZAZI MAPEMA ILI WAJUE NN CHA KUFNAYA KULIKO KUKAA KIMYA NDUGU YANGU.
Hi mama mtoto nimesoma habari zako na zimenisikitisha sana sana kama wewe ni christian ulieokoka hebu mtafute mungu na kumtafuta mungu anza hapo nyumbani kwako tafuta bible soma kwa kumaanisha kabisa na fanya maombi msihi mungu aingilie kati ndoa yako, na upate solution, kama mwanzo hakuwa hivyo kwanini sasa hivi amekuwa hivyo shetani ni mwizi, na pia kuwa muangalifu ikibidi hebu stop kufanya tendo la ndoa naye kwa sasa mpaka abadilike, na ukiridhia amebadilika mkapime upya ikimwi upo kama nyugu siku hizi kila kona, na wewe bado mdogo na muombe mungu mlango wa kazi ufunguke pia nayo itakusidia ili hata kama ukiamua kuanza maisha yako una kazi yako na mtoto mmoja hakushindi kwa elimu ya chuo kikuu mshahara wako ni mzuri, ila usivunje ndoa sijakushauri hivyo
ReplyDeletenakuhurumia sana mdogo wangu, Mungu atusaidie tulioko kwenye ndoa, kha! wanaume kama wamerogwa jamani, kwanini wana mambo ya kijinga namna hii? mimi wangu alikuwa hivyo hivyo ila nilimnyoosha, nakushauri anza na hatua ndogo tu! ya kuwaambia ndugu zake, ikishindikana nitakwambia nini cha kufanya, humu humu kwa violet
ReplyDeletepole
Hi dada habari!! pole sana mdogo wangu kwa hayo mambo yanayokusibu kwenye ndoa yako. ingawa alichokiunganisha Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha, nakuomba sana kaa naye mjadili ikishindikana angalia ustaarabu mwingine kwani una elimu yako sioni sababu yakuendelea kung'ang'ania matatizo utapatwa na pressure bure wkt mwenzio anafurahi funguka!!!!
ReplyDeletepole sana mdogo wangu kwa matatizo yanayokupata ktk ndoa yako ambayo ingali changa kwakweli nimesoma hii habari yako imemeniuma sana afadhali hata wewe uliyeomba ushauri kuliko wengine wanakaa tu kimya nakufanya maamuzi ambayo haistahiimili pole sana mimi nakushauri hivi unajua hana linalomshinda mungu wetu aliyetuumba piga magoti mlilie mwombe aingilie ndoa yako na ainusuru ndoa yako hakika hataacha kukusikia na kukusaidia yeye ni mwingi wa rehema alimradi tu umwamini funga na kusali amka saa nane ya usiku piga magoti mlilie sana atakusikia na atarekebisha ndoa yako hakika ukifuat hii ninayokuambia utarudi hapa kutoa hushuhuda ni hayo tu hakika amtumainie bwana hataibika milele
ReplyDeletePole my dia,
ReplyDeleteNimesikitishwa na tatizo lako..POLE.
ngoja nikupe experience mimi nina miaka 4 ya ndoa.kawaida kuna kipindi cha furaha kuna kipindi mnanuniana kuna kipindi mnachunguzana mara anapekua simu yako na wewe vilevile...kuna kipindi hata hutaki kumuona na yeye vilevile..na kunakipindi mnapendana kupita maelezo..
Sasa mambo ya kufanya:
Mshirikishe Mungu...sala ni muhimu sana usikubali akunyime kwenda kanisani hata siku moja tena jitahidi kumshawishi nae aende kanisani
Sijajua mtoto ana umri wa miezi mingapi...lakini anza kutafuta kazi My dia...usikubali kuishi bila kuwa na kazi elimu yako inatosha kuelewa hilo..
Asijidai kuwa na wivu ni muongo huyo usikubali..mtu mwenye wivu kuna mambo anaficha...please try to set rules mapema...usikubali kurudi kwake asubuhi wala kuchelewa tafuta solution--mshirikishe ndugu yake...myaongee peaneni mikakati -3years inatosha kujuana kabisa unless kama ulikuwa mpole tangu mwanzo ndio maana anakuonea-asipobadilika kwakuwa umesema anawivu-siku akichelewa kurudi try to make yourself smart vaa the best nguo ukisikia anafungua mlango nawe ingia msalani then toka..akikuona kweli atajua na wewe ulitoka..hapo ndo wivu utamjaa- anaweza anza kubadilika although inaweza chukua muda but it is something..
Wakati mwingine try to be tofauti kama umezoea kumuuliza akiwa amechelewa siku hiyo usimuulize..tena try to find a nice sleep asubuhi do your thing happily tena kama ni redio washa sikiliza matukio ya duniani..he will change himself..POLE BE STRONG --kulia ni big cure for women...but sala is also a cure...
all the best!
pole sana dada,ukisikia ukumu wa ndoa ndo huo! na ukimwi huu ulivyozagaa kama mifuko ya plastick we acha,ushauri wangu kwako kaa kimya usimuulize chochote kile kinachohusu mambo yake anayofanya hata akilala nje usimuulize nyamaza kimya na wala usimnunie,ila atapotaka tendo la ndoa usikubali tafuta sababu ya kumwambia ili usifanye nae mapenzi,kwasababu wewe una mtoto mdogo na yeye huwezi jua anapochelewea na siku zote mwanaume akiwa ana mwanamke nje anaanza dharau na hapendi kuulizwa sasa ww cha muhimu kwako usimruhusu afanye tendo,lea mtt wako akue,ipo siku atajiona mjinga sasa atakaporudi na kuomba msamaha ndo hapo utakapomwambia mkapime,usikubali kufanya nae mapenzi kabla ya kupima utamuua mtt bado ananyonya,kama alikuwa anaona bado hajawa tayari kuwa na mke basi asingekuoa angemaliza kwanza starehe zake,anayofanya ni kama yupo bachela na mwanaume anayekupenda hawezi kukuumiza hata siku moja,mimi imeniuma sana na mengi sana ya kukwambia nakuonea imani sana ila ndo uwe imara hata kama unampenda kiasi gani,isitoshe una elimu yako nzuri tu,mkalie kimya huyo atajiona mjinga mwenyewe! na jitahidi kutafuta kazi ufanye kwani kazi zipo nyingi utapata tu,kazi ndo kila kitu hawa wanaume si wakuwategemea hata chembe! pole sana Mungu atakuongoza mpenzi
ReplyDeleteemmy
pole dada muombe Mungu mshirikishe mama yako pia kwa ushauri utaendelea kupata tabu mpaka lini maisha ndiyo haya haya huyo kapata mtu anamchanganya kichwa so cha muhimu tafuta kazi uwe na maisha yako wanaume sio watu wa kuwategemea hata kidogo hao ni watu wa kupita tu wanaume wa sasa hawana mapenzi ya dhati wengi wao.
ReplyDelete