Mimi ni mama wa mtoto 1 nina miezi 6 tangu nimefunga ndoa, pia nina umri wa miaka 24. Tatizo langu ni kwamba simuelewi mume wangu kama kweli ananipenda au alinioa tu kwa sababu nilimzalia mtoto? Kwa sasa mi ni mama wa nyumbani nimemaliza chuo kikuu mwaka jana na mpaka sasa sijabahatika kupata ajira.
Kwanza mume wangu alianza kuwa ananifokea hovyo hata mbele ya wageni kwa makosa madogomadogo. Pia ni mwezi wa 3 sasa mume wangu amekuwa na desturi ya kurudi usiku wa manane akiwa amelewa au hata alfajiri siku nyingine na mara nyingi siku za weekend huwa harudi nyumbani. kwa kweli huwa naumia sana na mara nyingi huwa nalia na kusali peke yangu maana nikijaribu kuongea nae kumuuliza nini tatizo mbona unanifanyia hivi huwa ananijibu "unataka nisirudi kabisa au?" Naona aibu kuwaambia wazazi kuhusu hili maana ni muda mfupi sana tangu tumefunga ndoa.
Kuna kipindi nirijaribu kumshirikisha bestfriend wake labda kama angeweza kunisaidia kwa kumshauri rafiki yake ila cha kusikitisha nayeye akanitaka kimapenzi. Yaani sielewi maana somatimes nahisi labda mume wangu kalogwa
. Ila cha kushangaza ni kwamba mume wangu ana wivu sana na mimi kila mara anakagua simu yangu, hataki niende hata saluni kanisani kwenyewe naenda kwa kulazimisha ila huwa naona kama hafurahii. Sikumbuki mara ya mwisho mume wangu kwenda ni lini.
Kuna kipindi nilijaribu kuangalia simu yake kwa kweli niliumia sana kwani nilikuta kanisave 'mama com' na si 'wife' kama alivyokuwa amenisave mwanzoni.
Kwa kweli watanzania naombeni ushauri wenu maana naogopa naweza kuja kuambukizwa gonjwa la Ukimwi kwani mimi bado ni mdogo na bado nina ndoto zangu nyingi.
Nampenda sana mume wangu ila simuelewi kwa kweli. tumeishi miaka 3 kabla ya kufunga nae ndoa na hakuwa hivi alinipenda sana hadi watu na rafiki zangu hawakusita kuniambia jinsi alivyokuwa ananipenda. Natamani angeniambia nilichomkosea mume wangu kwani ninajaribu sana kuwa good wife but he never appreciate it.
Tafadhali naombeni ushari wenu watanzania wenzangu.