Sunday, November 14, 2010

NIMEMZIDI UMRI MCHUMBA WANGU NAONA AIBU KUFUNGA NAE NDOA


 Habari ya kazi, mimi ni mpenzi sana wa blog yako, Inatusaidia sana mungu akubariki, mimi ni mama wa mtoto mmoja , nilitokea kuchukia wanaume wote pale nilipotendwa na nilikaa miaka mitatu bila ya kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote. Mwaka huu january niliingia kwenye uhusiano na kaka mmoja ambaye kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya harusi.

Kinachonifanya niombe ushauri ni kuhusu umri ninamzidi huyu mwanaume miaka miwili na ninaumbo kubwa sana naonekana mkubwa sana nimejalibu kujipunguza lakini wapi, ninakosa amani na ninapozungumza nae kumweleza mimi ni mkubwa kwake yeye hajali na anaona sawa tu.

Ninaogopa sana mwanzo wa uchumba alikuwa hataki kuniambia miaka yake sasa juzi nilipokuwa kwao ndio mama akawa anaelezea jinsi mwanae alivyomzaa mpaka kukuwa kwake. Niliumia sana dada natamani kusitisha maandalizi ya harusi lkn nashindwa maana next thursday ndio send off yangu. Jamani nifanyeje ninaumia sana moyoni.naombeni ushauri wenu wadau.

 
 
 
 

10 comments:

  1. dada mapenzi hayana umri!ndo maana wakasema mapenzi ni majani huota popote,ndo maana hata huyo mumeo mtarajiwa ameona sawa,kuwa na amani endelea na mipango ya ndoa kama kawaida.

    ReplyDelete
  2. Mimi sioni kama age ni tatizo! Maadam mume anakupenda na ameamua kufunga nawewe ndoa wewe olewa tu. Mimi sijawahi kuona ndoa inasitishwa kanisani au msikitini eti kwa sababu ya age! Kinachotakiwa tu umheshimu mumeo hata kama unamzidi umri ili ndoa yenu idumu. Nakutakia maisha mema katika ndoa yenu.

    ReplyDelete
  3. Miaka miwili tu! mbona si ishu, wenzio mitano! miaka ni namba tu, umbo kubwa ni asili si ukubwa, hata ungekua mdogo kwake still ungeonekana mkubwa. Cha muhimu jishushe sana na umuheshimu sana.

    Ndoa hazipatikan kirahic, usichezee bahati.

    ReplyDelete
  4. Dada usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu umri,kikubwa ni kupendana na kuheshimiana.Umri hauna sehemu kabisa katika mapenzi.Mimi nina mjomba wangu ameoa mke mkubwa kwake kwa zaidi ya miaka mitano na hivi sasa mkewe alishastaafu kazi toka mwaka juzi lakini yeye bado yupo kazini.Kwa hiyo usihofu endelea na maandalizi ya harusi na nakutakia kila la heri!

    ReplyDelete
  5. no comment wee nenda kale tendo..
    yellow!!!

    ReplyDelete
  6. hhehehe..wewe dada..natamani ningekua karibu na wewe naona ndio ungenielewa zaidi ..umri ni namba tu hizo mama,na umbo lako ndio kalipenda mumeo ..kama yeye amekubali kufunga ndoa na wewe..shida iko wapi mpenzi ?? mbona hujiamini..jamani unaniudhi hata sikufahamu..hebu achana na hayo mawazo ya kienyeji...nenda kafunge ndoa, mpende mume wako, ufurahie maisha yako..

    ReplyDelete
  7. Nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya hayo... umri haujalishi, ningependa kuwasifu wachangiaji waliotangulia kama walivyosema cha muhimu wewe jishushe mpende mumeo, mmnyenyekee na umthamini basi mtaishi kwa raha mustarehe bila tatizo kwani umri haujalishi hata kidogo... ni kweli hata mimi mjomba wangu ameoa mwanamke aliyemzidi miaka zaidi ya minne hivi kama sijakosea lakini ukisikia akiitwa na mumewe utasikia anavyoitika kwa heshima (bee baba) au same times utasiki ( yes sweetie) so cha muhimu ni kuheshimiana,,... we endelea na mipango yako ya ndoa na MUNGU AWABARIKI KATIKA MAISHA YENU MAPYA MNAYOENDA KUYAANZA KAMA MKE NA MUME...

    ReplyDelete
  8. Hebu nenda kaolewe acha uswahili! miaka mingi! miaka mingi! nani kaskuambia miaka inaoa au kuolewa?
    Hebu usituchefue Olewa. Eti umbo kubwa ndilo alilolipenda huyo jamaa anapenda umbo kama lako ndio maana amezimia kwako na katangaza nia, wewe vipi! mtu mzima harafu hugundui?
    Eti umemzidi miaka miwili! nini miwili MTUME alipishana na mkewe miaka Ishirini...............Kizito!!

    ReplyDelete
  9. Hebu olewa tupunguze wanaharamu mitaani....Kifuna

    ReplyDelete
  10. Olewa wala usiwe na hofu cha msingi ni kuheshimiana (utii)

    ReplyDelete