Wednesday, October 6, 2010

NAMCHUKIA SANA MUME WANGU- NATAMANI HATA KUACHANA NAE, NIFANYE NINI


Habari, mimi ni mama, nina miaka 12 kwenye ndoa yangu, na nimejaaliwa kuwa na watoto watatu,
Mimi na mume wangu ndoa yetu ni ya kanisani, isipokuwa bamiaka minne iliyopita, mume wangu alianza vituko vya ajabu ajabu, akawa ananichukia hadi watoto wakajua hilo, ananipigiga, kuna kipindi alitoa hadi nguo zangu nje ili niondoke na kudai namng’ang’ania kwanini, hali hii iliniumiza sana, baada ya kuchunguza nikajua amepata mwanamke mwingine. na ameshazaa nae na mtoto wao ana umri wa miaka mitatu sasa

 Niliumia sana, maana hata huduma nyumbani zilisitishwa. tukaanza kuishi maisha ya shida sana na wanangu. nikajitahidi kuwasomesha, nashukuru mungu wanangu wanaendelea vizuri. sasa juzi juzi hapa nimepata taarifa kuwa wameachana na yule msichana waliezaa nae, tena kwa ugomvi mkubwa, cha ajabu eti ndio mume wangu anahamishia mapenzi yote kwangu. 

 lakini kwa upande wangu sasa hivi nimetokea kumchukia kupita maelezo, yani nimemshiba kabisa, sijiskii kushirikiana nae jambo lolote, namuona kama ananuka vile, najitahidi kuicontrol sana hali hii, lakini nashindwa kabisa, unakuta akija tu! Natamani hata nikajifiche mahali na staki hata anisemeshe, nimejaribu kwenda kuombewa, lakini wapi, hali ipo pale pale, sijui kwa kuwa alinitesa sana, yani sasa hivi hata kutoka nae kwenda nae kwenye sherehe siwezi, akienda yeye mimi bora nibakie, na akibakia yeye bora mimi nitoke,


tena sasa hivi hata nisikie yuko baa gani sijui anakunywa na wanawake, sishituki wala kuumia naona afadhali aendelee kunywa huko akirudi amelewa anafikia kulala, kiufupi simpi huduma yeyote ile, mimi sijisikii kufanya chochote kile, sasa naona kama vile ninaishi maisha ya mateso, nifanyaje wamama wenzangu?  na kikubwa ni kuhusu huyo mtoto, jamani inauma sana, isikieni tu kwa wenzenu, mimi yamenikuta naumia nateseka sana, hata kama wameachana mtoto si atawaunganisha tu???

Naombeni mawazo yenu.

4 comments:

  1. pole sana dada, mimi nakushauri kazna maombi tu, mungu atakusaidia na utampenda tu! shida niliyoiona hapo kwako ni moja tu, wewe unahesabu makosa, ndio maana unajikuta unamchukia,hebu kubali kusamehe kwa moyo mmoja na ufanye kama vile hakuna kilichotokea, Mungu atakusaidia

    ReplyDelete
  2. mh! inaumiza sana jamani, tusikimbilie tu kusema msamehe na usahau, bora hata wangekuwa hawajazaa na huyo mwanamk nje, lakini atakumbuka makosa kila atakapoiona damu ya mumewe lazima uumizwe lo! mh! pole dada

    ReplyDelete
  3. Pole sana mdogo wangu, hawa wanaume sijui wamelaaniwa? Maana tabia zao ni kama zinafanana. Kwa kuwa ameachana na hawala yake ndo kakuona unafaa? Achana naye chamsingi kaa tu ili uwalee watoto wako. Uishi naye kama kaka maana huwezi jua huko alikokuwa kama ni salama au la asije akawa kakuletea magonjwa.

    ReplyDelete
  4. Pole sana dada. Mimi pia nina tatizo na mume wangu tumeishi miaka 11 sasa na tuna watoto wawili. Mume wangu ni malaya kupita kiasi kila msichana anamtongoza mpaka ndugu zangu. Mpaka house girl wangu anamsifia kwamba yeye ni mzuri sana kwa hiyo matokeo yake msichana haniheshimu tena mimi ndani ya nyumba. Kibaya zaidi hanipi hela ya matumizi mimi ndio namhudumia. Nilisafiri kikazi nikakuta gari yangu moja ameiuza hela haijulikani ilipo. Kila siku anarudi usiku wa manane na tunaweza tukakaa hata miezi 8 hatujakutana kimwili kila nikimuomba tendo ananiambia amechoka tena ni mkali kweli. Ndoa yetu ni ya kanisani na hii tabia ya umalaya hakuianza leo nimekuwa nikivumilia kwa miaka yote 11. Ila nahisi nimeshindwa nitakufa si zangu si kwa ukimwi tu bali hata kwa mawazo. Kinachonitia huzuni zaidi mtoto wangu wa miaka 5 ana matatizo hajui kuongea, anapatwa na degedege kila mara hivyo anatumia dawa kila siku za kuzuia degedege. Kila nikitaka kuondoka namuwaza mtoto wangu huyu namuachaje? Huyu mwingine wa miaka 10 yeye ni mkubwa sina wasi wasi hata nikiondoka. Nimechoka sana kuishi maisha ya masononeko jamani naombeni ushauri wenu.

    ReplyDelete