Friday, July 29, 2011

VINYWELEO VIMEJAA MIGUUNI – NIVITOE NA NINI? VINAHARIBU MIGUU YANGU


Wapenzi, mnisamehe kwa kuwatupa kwa muda mrefu kidogo, jamani niko busy kupita kiasi, nimebanwa sana kazini, chuoni , na kuna issue nyingine nafanya inanikeep busy sana, ikikamilika hiyo issue ya tatu nitawajulisha wadau wangu, but tupo pamoja sana, 

Kuna mtu ameniomba ushauri jinsi ya kuondoa vinyweleo katika miguu yake, sasa je kwa wale ambao mnafahamu  njia za kutoa hivyo vinyweleo ni nini? 
atumie wembe, uzi, veet , au hairuhusiwi kuvitoa au kuna njia zingine tena za kutumia??


Jamani vinyweleo vinakera, vinaharibu uzuri wa miguu yetu kabisa yani, unakuta mguu mweupe halafu vinyweleo vimejazanaaaaaa vyeusi,  wala hainogi,  naamini kwa kumsaidia alieuliza, na wengine watapata msaada pia



Saturday, July 16, 2011

NINA MIAKA 48 NATAKA NIISHI NA MTU MZIMA MWENZANGU, JE NITAWEZA KUSHIKA MIMBA??


Dada Beauty touch in Dar, napenda nikupongeze kwa blog yako nzuri sana, mungu akubariki maana inatusaidia sana,

Mimi ni mama mtu mzima tu! Nina watoto wakubwa, ila sikubahatika kupata elimu ya darasani, sasa hivi nina miaka 48 na nimeacha kuona siku zangu, huu ni mwaka wa sita na niliacha kuona nikiwa na miaka na 42, sasa nauliza hivi, je? Ninaweza kupata mimba?

Maana zamani nilitumia njia mbali mbali za kuzuia mimba, sasa nilipoachana na mzazi mwenzangu nikaamua kuachana  na hizo njia za kuzuia mimba, kwakuwa nilianza maisha ya kuishi peke yangu.

Lakini sasa nimepata mtu mzima mwenzangu na tunataka kuishi pamoja, je naweza kupata mimba wakati siku zangu sizioni? Mimi na mwenzangu wote hatutaki mtoto, maana kila mmoja ana watoto wake tena wakubwa ,
Naombeni ushauri wenu  jamani,



Monday, July 4, 2011

NIMEPIMA NIMEAMBIWA NINA UKIMWI?? NDOTO ZANGU ZIMEPOTEA GAFLA NAHISI KAMA NIMESHAKUFA,

Habari yako dada Violet, tafadhali usinitaje jina langu, wala email yangu, nimepewa blog yako na mtu, nahisi naweza kusaidiwa shida yangu
Nilipitiliza siku zangu hivi karibuni nilipata ujauzito,  kwa bahati mbaya ulikuwa nje ya kizazi, kusema ukweli sijaolewa, ila kuna mtu nilikuwa na musiano nae, na ni mwanaume wangu wa kwanza, kwa sasa nina miaka 22,
Ninaishi na wazazi  wangu walezi, maana mama alifariki wakati ananizaa, baba amefariki mwaka jana, sasa nina wazazi wangu wa ubatizo ndio walinichukuwa ili kunisaidia,  basi baada ya mimba kuwa nje ya kizazi nilipelekwa hsptl nikahudumiwa, nilikuwa na maumivu makali sana, na nilikuwa sijielewi kabisa, baada ya hapo nilianza kuumwa sana, siku moja mama alinipeleka  hsptl, wakapima vipimo vyote, na aliwaambiwa wanipime hadi ukimwi bila mimi kujua,

Baada ya kurudi nyumbani mama akaniambia nimeathirika, dada violet, naandika huku nalia, maana ni wiki mbili sasa tangu nitambuwe hivyo, najiona nimeshakonda, nahisi nimeshakufa, ila ninahema,  nifanye nini? Mbona sina matumaini tena, au nijiuwe? Au niende nikakae wapi??  Ina maana ndoto zangu ndio basi tena?? Ina maana sitafanya mambo yangu ya msingi yote??? Au ndio nimeshakufa mimi?? mbona mimi bado mdogo sana, ndio kwanza naanza kuyajua maisha, kwanini nakufa mapema hivi??
 
Nilikutana na yule kaka kwenye harusi moja tulikuwa maids, akanitaka kimapenzi, nilimzungusha kama miezi hivi, badae nikasema namimi nijaribu, ndio tukawa wapenzi, sikujuwa kama naenda kufa, sikujua hata kidogo dada violet, nifanyaje sasa?  Nimelia hadi nimechoka na machozi hayatoki tena, nimeanza kuvimba miguu, nywele zangu zote nimekata , najihisi kama maiti inayotembea, nitafanyaje jamaani, 



Monday, June 27, 2011

SIJUI NJIA GANI YA UZAZI WA MPANGO HAINA MADHARA NAOMBA USHAURI

Hallow dada violet mimi ni mama wa mtoto mmoja namshukuru Mungu anaendelea vizuri, dada violet naomba ushauri ipi ni njia sahihi ya kuzuia mimba kwani

nilikuwa natumia sana mipira (condom) ila naona inanidhuru kwani inanisababishia kuwashwa mara kwa mara. naomba ushauri wako na wadau wengine nitumie kinga gani kuzuia ujauzito kwa sasa kwani mwanangu bado ni mdogo anaitaji ukaribu wa mama. asante sana




Friday, June 24, 2011

WAKAZI WA MOROGORO MPO TAYARI, MMEJIPANGA????



Ni Tarehe 01 / 07 / 2011, Ndani ya hoteli Ya Ukweli  Morogoro Hotel, warembo 15 watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Morogoro 2011. Shindano litaanza saa mbili usiku hadi saa sita likishindikizwa na burudanikabambe toka kwa timu nzima ya Tip Top Connection, pamoja na vibwagizobabukubwa toka kwa msanii Wanne Star.
Kiingilio kitakua 10,000 Tsh kwa mtu mmoja.
WATAMBUWE WAREMBO HAO WATAKAOPANDA JUKWAANI SIKU HIYO

MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 BERTHALIUS USIRI AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 REHEMA MARWA AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.

MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 RUBY JOSEPH AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.

MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 SHARIFA ISSA AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAKUFUNZI WAO, MRATIBU, MKURUGENZI WA FG ARTS PROMOTION, NA WAWAKILISHI WA WADHAMI WAO. AMBAO NI REDDS NA VODACOM TANZANIA.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 REHEME MARWA (KUSHOTO) NA SHARIFA ISSA (KULIA).

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 SALMA KUYELA (KUSHOTO) NA ASHA SALEH (KULIA).

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 TOKA KUSHOTO NI NAJMA ALLY, SALMA S. KUYELA NA BERTHALIUS USIRI.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 TOKA KUSHOTO NI AGNESS ROISER, PENDO DANIEL NA HASNAT KHAMIS.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).

BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 WAKIPATA KIFUNGUA KINYWA KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.

MREMBO JACKLYN KITINKA AKIWA NA WASHIRIKI WENZIWE KWENYE CHAKULA CHA JIONI KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.

    
BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 WAKIPATA CHAKULA CHA JIONI KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.

Kazi kwenu jamani, kiingilio ni 10,000/= tu (elfu kumi)  mie ntafunga safari kwenda nikashuhudie catwalk za ukweli, hii si ya kukosa wakazi wa morogo, hii itakuwa Bab Kubwaaaa, coz maandalizi yake tu!  Ni ya kutisha, anza kuzichanga hizo 10,000 /=