Mambo Dada, please usirushe email yangu,
Mimi niko hapa dar, nina miaka 25, tatizo langu ni kwamba ninatoa harufu kali sana, mwili wote, jasho langu lina nunuka sana, kwapa, hata sehemu za siri nanuka pia, hhali hii inaniumiza sana, inanitesa na kuninyima raha, nakosa kujiamini,
Niliwahi kwenda hospitali, wakafanyia check-up, wakasema nikazane usafi tu, ndio maumbile yangu, lakini sasa mbona hali hiizamani haikuwepo??? Ni miaka mitatu sasa tangu niwe hivi, unakuta hadi nikikaa na watu nahisis wananisema mimi ninavyonuka, kwenye pochi yangu hukos perfume au deodorant za aina 4, kila mara niko washroom najipulizia, hali hii ni ngumu, kwa usafi mimi ni msafi sana, sielezi ni nini hiki,
Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja hapa hapa dar, tulidumu kwenye mahusiano miezi mitatu tu! Yeye alikuwa ni msafi sana, sasa harufu yangu ika wa inamkera, nakumbuka kuna siku aliniambia bwana nakupenda, ila harufu yako mimi mmm, hapana siwezi kuvumilia, nililia sana, sometimes hat akitandani alikuwa akijifunika shuka lake, finally tukaja kuachana, alinikwepasana, nikipiga sim hapokei, mara nikasikia anataka kuoa,
Please naombeni ushauri wenu jamani, nisaidieni mwanamke mwenzenu nakosa raha kabisa, muda mwingine huwa nalia peke yangu, serious naombeni msaada wenu, maana perfume zimenichosha sasa, nimetumia manukato yote, sasa nona yamenizowea harufu iko pale pale, sometimes huwa nahisi nimerogwa, nikaa na watu nahisi wote wananisema mimi, na wengine niliwahi kuwasikia kabisa wakinitaja na jina langu, inaniuma sana, bora ingeonekana ni ugonjwa niutibu kwa gharama yeyote,
Please dada usirushe email yangu.