Monday, June 21, 2010

NILIKUWA NAUMWA JAMANI - NILILAZWA, BUT NOW IM GUD




Sijawatupa, tena niliwamisi vibaya mno wapenzi wangu, but nilikuwa mgonjwa, vidonda vya tumbo vinanisumbua sana, nililazwa pale Dar Group, but now namshukuru Mungu niko safi kabisa, na ninaendelea vizuri, Im back dears.


kwenye ward yetu tulikuwa wawili, nikapata na shost humo humo, kitoto hiki kinaitwa Rachel au Nyambura, kilitokea kunipenda sana, hadi kulala kikawa kinataka kulala na mimi hakimtaki mama yake, nikichomwa sindano nikikunja uso, kinaanza kulia chenyewe, huku kinanipapasa,


kwakuwa chakula kilikuwa hakikai tumboni basi, nilipopata nafuu nilikuwa nasikia njaa hadi miguuni, nilikunywa juice kama maji, coz ndio iliyokuwepo kwa kipindi hicho, jamani vidonda vinatesa lo! halafu vinatokeaga gafla tu jamani,


at the end of the day, nilipata discharge na kumuacha shost wangu hospitali, wakati natoka mtoto alinililia sana, mama yake akaniomba nimsubiri ambembeleze alale ndio niondoke, yeye shost alikuwa ana malaria, hata hivyo ni kajasiri sana, yani kalijikaza kweli, basi nilimbembeleza mwenyewe, hadi akalala kabisa ndio nikaondoka, nashukuru Mungu after two days mama yake akaniambia nao wameruhusiwa,

all in all narudisha sifa na utukufu na shukrani za pekee kwa Mungu wangu, kwa kunitetea na kunipa nguvu, uponyaji na afya,



Sunday, June 13, 2010

HAPPY BIRTHDAY TO MEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!


Nimeongeza mwaka jamani, nimekua, tunafurahia kuufikia utu uzima, namshukuru sana Mungu, kwa kuniongezea mwaka mwingine tena!
also many thanks to my Mom, Coz bila yeye mimi nisingekuwa hapa nilipo, amenipa malezi yapasayo hadi sasa nami naitwa mama kama yeye na nina familia yangu sasa, hakika misingi yake imara aliyoijenga alipokuwa ananilea, ndio hiyo imesimama hadi sasa, nafurahi kuwa na mama kama huyu! Mungu akubariki mama yangu, wewe ndiwe nguzo ya maisha yangu, zaidi ya mama wewe ni rafiki na mshauri wangu



Dad too, thanks for your support to mother, umetusomesha, umetuongoza, umetufundisha maisha, umetusaidia kwa mengi, kwa niaba ya watoto wako woooote watano, nawawakirisha kwa kusema MUNGU AWABARIKI WAZAZI WETU!

mwingine ni dada yangu (mama Godluv) Joy, coz ndie alieniandalia this small function, but ilinoga kusema ukweli, nilikata keki, nilikula, nikaimbiwa, we! raha jamani, mwenyewe nilikuwa sina hata mpango, lakini akasema no! ill do it 4 you, '' be under blesses of God dada! wengine ni wanangu, japo siku ya party walinitoroka, walienda kusimamia birthday ingine ya rafiki yao,nawapenda sana wanangu, coz wao ndio wanaonipa heshima ya kuitwa mama, wao ndio wananifanya niwe na furaha every minute


Pia namshukuru Mume wangu, thanks baba ''T'', coz yeye ndie alikuwa wa kwanza kuniwish happy birthday, na ameninunulia gift nzuri ambazo wala sikuwa nimetegemea kwa sasa, ameninunulia handbag nyekundu, kigauni chekundu na Belt lake, na viatu vyekundu, we! nimenoga kama nini? asante sweet heart!
namuomba Mungu, anipe afya njema, amani, furaha, abariki kila ninachokifanya,
AMEN!

Friday, June 11, 2010

NIMEMFUMANIA MCHUMBA WANGU, AMETUBU NA ANATAKA TUFUNGE NDOA, NIKUBALI?

Watanzania wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu,

Katika maisha yangu yote hadi sasa nina miaka 24, sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine, zaidi ya huyu mchumba wangu nilie nae, nampenda kuliko kitu chochote

Tumeanza urafiki wetu nikiwa na miaka 21 ila mchumba wangu amebadirika sana, alisema atanioa, amejitambulisha na kwetu, lakini gafla, ameahirisha, anasema kwa sasa mambo yamekuwa mengi sana, na hata maongezi yake si ya kawaida, yani anaongea as if amekasirika, sasa ile hali mimi siipendi, kila nikijaribu kupeleleza ili nijuwe labda nimemkosea, sipati jawabu lolote,


Baada ya kuchunguza sana, nikagundua anatembea na secretary wao, na ninasikia tu kwa watu kuwa anataka kumchumbia, nimelia sana na moyo wangu wala hautaki kuamini hili, nilishawahi taka kunywa vidonge nife, dada alinikuta, na kunisema sana, lakini bado akili haijakaa sawa,

Mwezi uliopita rafiki wa mchumba wangu, alikuja yeye na dada yake, wakaomba kuongea na mimi, I thought kwamba wametumwa na Rick (mchumba wangu), kumbe walikuja kwa mengine,

Kilichomleta ni kwamba, anataka kunioa yeye, anadai alikuwa akiichunguza tabia yangu toka siku nyingi na kudai kuwa mchumba wangu si mwaminifu, lakini kwakuwa hatujafunga ndoa, basi yeye anataka kunioa, na dada yake ni mtumzima amethibitisha hilo, mimi nilikataa kata kata, nikawafukuza kwa hasira,

Nilimpigia sim mchumba wangu kumwambia, alichukia sana, akachukuwa company yake, wakalewa wakaenda kumpiga, walimpiga sana, Yule kaka alinitumia sms hii, ‘’ iko siku utanikumbuka’’ dada, sikuamini siku ambayo nilitoka safari, na kupitiliza kwa mchumba wangu nikamkuta na yule secretary wao, nilikwenda moja kwamoja kwakuwa sikumpata kwenye simu kumjulisha kuwa nakwenda. Na ni wiki ile ile ambayo rafiki yake alipigwa,

Toka siku ile moyo wangu umekufa ganzi nilimchukia gafla na nikaona siwezi kuishi bila yeye. alipoitwa na baadhi ya jamaa zangu, alisema kuwa nibahati mbaya tu shetani alimpitia! Ila Bado ananipenda, na anataka anitolee mahari kabisa ili tufunge ndoa, lakini dada yangu ananikatalia maana ndie alienilea toka mdogo. Sasa nishaurini mdogo wenu nifanyaje? Sijielewi, nimsamehe, au nimkubali Yule rafiki yake


Friday, June 4, 2010

WATOTO WA MUME WANGU, WANATAKA NIACHWE, MAMA YAO ARUDIWE

Nilikuwa na uhusiano na baba mmoja huku kondoa ambae ni mtu mzima sana kwangu, lakini kwakuwa mapenzi hayachagui umri, basi tulipendana sana, na nilipomuuliza kwa umri ule alionao aniweke wazi kama ameoa, alisema walishaachana na mkewe, ila anawatoto watatu mabinti wakubwa wawili wa umri kama wangu, na wakiume mmoja.

alinipeleka kwao mwanza, akanitambulisha kwao, na ni kweli kwamba waliachana na mkewe, basi tukaanza maisha ya pamoja, yeye ni mfanya biashara! Na mm nina grocery yangu. baada ya miaka miwili nikajaliwa kupata mtoto wa kiume, nilimwambia tumeshachunguzana vya kutosha, sasa tufunge ndoa tuishi kiharari, akakubali, wakati tuko kwenye maandalizi ya ndoa alipigiwa simu huko kwao, kwamba watoto wake wanataka kuja, mimi sikuwa na hofu yeyote, nilimkubalia waje tu!

Violet, toka hao watoto wamefika, ndani hatuna amani hata kidogo, tunaishi kama mtu na wake wenzie, mimi kawaida huwa sipendi kuongea ongea lakini watoto hawa wamefanya niongee, Ugomvi kila siku, na kuna siku nilikuwa nafua nguo zangu, mtoto wa mume wangu wa kiume anamiaka 27, akatoa nguo zake zote mimi nifue, nilikataa kwakweli, ukizingatia hakuwa mgonjwa kusema anahitaji msaada, wale wa kike hawataki kufanya kazi yeyote ile, kukicha tu, sitting room kuangalia CD, kupika nipike mimi, au msichana wangu wa kazi wao wanataka kula tu, mbaya zaidi wanasema umemng’oa mama yetu nawewe jiandae tutakutoa, wakati mimi nilikuta wameshaachana kabisa. Na hapa tunapokaa ni nyumba yangu mimi. Baba yao kanikuta nayo

Kingine Hawampendi mwanangu kabisa, kuna siku nilirudi toka kazini, nikakuta mtoto kavimba mdomo wote, hawezi kuongea, nikamuuliza mschana, imekuwaje, akasema Regina (mtoto wa mwsho)wa mume wangu alimsukuma toka mlangoni hadi chini, akaangukia tofali, mdomo ukachanika kwa chini, nililia sana, nilichukia, nikawafata walikuwa chumbani kwao, alichonijibu akasema mwanao mjeuri, nilimuuliza wewe binti mkubwa miaka 24 utagombana na mtoto wa miaka mine kweli? wakati naongea nao walinirukia walinipiga sana,

Wakat yanatokea haya mume angu alikuwa safari, nilimpigia simu aliporudi nikamueleza, aliwasema sana, ila mimi nilimwambia hawa watoto wameshakuwa wakubwa, miaka 24 na 27 na huyo mkubwa 30. Wajitegemee, kwanini wakae kwangu ? nilimshauri awape mtaji wakafanye biashara, watoto walichukuwa pesa, na kuondoka hawakuondoka, na wamesema hawatoki pale, hadi mimi niondoke aje mama yao, sina amani wala raha hata kidogo, nisaidieni mwenzenu.

Tuesday, June 1, 2010

MUMEO NI MLEVI SANA? NA AKIRUDI TU ANAFIKIA KUKUTWANGA? JARIBU DAWA HII INAWEZA KUMSAIDIA

Nimepata rafiki mpya wadau, kama mjuavyo, wanawake tukikutana tu! Basi katika maongezi yetu lazima tufikie sehemu ya kuongelea waume zetu, iwe kwa mazuri au mabaya, lazima tuwaongelee tu! Basi jana akawa ananieleza matatizo ya mumewe, na jinsi alivyofanya hadi mumewe kuamua kutulia, nikamuomba niitoe ktk blog ili iwasaidie na wengine, amekubali. Na ndio naawapa kama ifuatavyo.

Mm nilimpenda sana mume wangu, kupita maelezo, na tangu anioe sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya ndoa,Ila alibadirika gafla sana, akawa na Company ya ajabu ajabu, akachukia hadi watoto wake,

Halipi ada ya shule, mm hanipendi hata kidogo, nimelia sanasana sana. Nimeshtaki kila mahali, hadi nikaona kama Mungu hanipendi vile, Akirudi ni usiku sana, amelewa chakari, akifika tu mimi naanza kulia kabla sijapigwa, labda atanihurumia, alkini wapi, nikifungua mlango tu! Ninae, yani ananipiga bila hata sababu

Siku moja nilichukuwa picha za harusi yangu, nikazitazama, machozi yalinitoka sana, nililia sana, nikapata wazo ambalo hata sijui ni Mungu alinipa au ni akili zangu tu, Ilikuwa siku ya juma mosi, niliamua kwenda salon, nikawaambie wanipambe mimi ni bibi harusi ila kuvaa nitavalia nyumbani, basi walikubali, wakanipamba vizuri sana, na usoni wakaniremba, nilipendeza kupita siku yangu ya harusi,

Nikarudi nyumbani nikachukuwa shera langu, nikalivaa, na kila kitu, na viatu nikashika na ua langu, nikakaa chumbani kitandani, kusema kweli nilikumbuka mbali sana, nililia sana huku nikiwa na ua langu, ni mwanaume niliempenda kwa moyo wangu woote,

Aliporudi akafungua mlango, akaingia ndani, kapitiliza hadi chumbani huku akitukana, basi kufika tu pale, alipigwa na butwaa sana, na pombe zilimwisha, akaniuliza wewe nani? Nikamwambia mimi ni mke wako? Najaribu kufanya kama bado sijaolewa vile, ni kama ndio najiandaa kwenda kanisani kukabidhiwa mume wangu,  maana haya unayonifanyia si ya mume kumfanyia mke, nahisi kama sikuwa nimeolewa, (nililia kwa uchungu sana)
Mume wangu alipiga magoti huku analia nayeye, akasema mke wangu naomba unisamehe, wewe umeolewa, na mimi nimke wako, nisamehe mke wangu , alilia sana, basi hapo hapo nami nikamuleza ninavyojisikia, nini nataka anifanyie ili nijihisi niko kwenye ndoa, nina mume,

Nashukuru alinielewa, toka siku ile hadi sasa tuna raha, kipigo kimekoma, mikwaruzano iliyopo sasa hivi ni ile ya kawaida tu, ambayo huisha bila hata kipigo.



(kiukweli jana wakati ananisimulia, nilisisimkwa, na hivi nina machozi ya promotion, we! Yakaanza kulenga lenga, ni akili ya aina yake jamani, amewaza sana, nimependa na nyie wapendwa mjifunze kitu kupitia hili, hata kama hutovaa shela kama yeye, unaweza kutumia njia ingine tu itakayomvuta karibu yako, )

Monday, May 31, 2010

BABA ANAMWANAMKE MWINGINE . ANAMTESA SANA MAMA YANGU, MIMI NI MTOTO TU! NIFANYE NINI?

Dada Violet, na wadau wote wa blog yako, nawaomba mmwombee baba yangu, maana amekuwa na tabia za ajabu sana kwa mama, zamani hakuwa hivyo ila tumefanya uchunguzi ni kwanini amebadilika gafla hivi, tumegundua ana mahusiano na mwanamke mwingine wa nje
Siku hizi haachi pesa ya chakula nyumbani yaani, matatizo kila kukicha, ugomvi kila siku ugomvi hauishi na siku nyingine hudiriki kuwafungia nje mama pamoja na wadogo zangu,
mama amejaribu kulipeleke kwa mkwe wake pamoja na mawifi zake ili wamsaidie lakini wanaonekana wako upande wa kaka yao (baba) sababu shangazi zangu hawampendi kabisa mama yangu, amekosa pa kukimbilia, amekosa msaada kabisa,
namshukuru Mungu nimesoma na ninafanya kazi ndio huwa kidogo namsapoti mama in short jamani naomba mumweke baba yangu kwenye maombi jamani ili abadilike sababu magonjwa ni mengi sana siku hizi najua wadau mnaosoma humu kila mtu ana imani ya lakini Mungu tunaemwabudu ni mmoja jamani nawaombeni.pili jamani kwenye ukoo wetu kuna kama kalaana ka ktoolewa sababu ndugu zangu wengi hawajaoa wala kuolewa

jamani sipendi niishie kama ndugu zangu napenda niolewe na niwe na familia yangu kama watu wengine,mimi ni msichana wa miaka 26 na nina degee kwa sasa ni mzuri sababu watu hawaishi kunisifia kila nipitapo lakini sijajua who is who jamani nimetulia sana mpaka mwenyewe kwa hilo huwa najisifu na najijua sababu mpaka sasa nimewai kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja then tukashindwa kuelewana,then nipo alone kwa sasa sijasubutu kuwa na uhusiano tena jamani naomba mniombee niweze pata mme wa maisha natamani kuolewa na kuwa na watoto,asanteni sana na imani mtaniombea.










Saturday, May 29, 2010

KINA BABA MSIOKAA NA FAMILIA ZENU- HEBU JARIBUNI WEEK END HII TUONE MTAPUNGUKIWA NINI

(wapenzi wangu, nitajitahidi kila weekend tuwe tunaongelea mambo ya kifamilia hasa kwa upande wa malezi kwa watoto wetu, pia nitoe nafasi hii kwa yeyote yule mwenye kitu chochote cha kumfanya mtoto ajisikie vizuri, basi anitumie kwenye email yangu pale juu, ili aweze kushare nasi, tunajisahau sana juu ya suala zima la watoto wetu.)









Jamani kuna kitu kinasumbuwa familia nyingi sana, nakutana na watu wengi hasa wanawake nikiwa salon na sehemu zingine, wanalalamika sana kuhusu waume zao kutokutulia nyumbani siku za weekend, unakuta mtu yuko busy kuanzia jumatatu hadi jumapili, kazi na yeye, yeye nakazi, sasa sijui ndio kazi kweli au ndio kazzzzzziiiiiiiiiiiii


inapendeza kuona familia zikiwa na furaha kwa pamoja, sio kila siku, but hata weekend moja moja jamani
chukuwa mkeo, watoto wenu, nendeni sehemu ambazo mtabadirisha mazingira ya nyumbani kidogo, japo kwa masaa machache, hebu jaribuni weekend hii muone watoto watakavyofurahia,

si lazima beach tu jamani, nendeni hata sehemu yenye hewa nzuri, ukiwa na familia yako, na mkeo inanoga jamani, mtakaa mtacheza na watoto kidogo, mtawauliza maswali ya michezo michezo, yani inapendeza sana,
lakini unakuta mwanaume mwingine, unapita hata mwezi hajuwi kama mtoto shule anaenda, anaandika, anashida gani, hajui lolote, akitoka kumi na mbili akirudi saa tatu saanne, wakati mtoto amesha lala, sijui wanafikir sifa

watoto ni wepesi sana kuridhika, chukuwa kipesa chako kidogo, wapeleke hata super market tu! wakajichagulie wanachotaka, mkimaliza mnakaa mahali mnapata chakula au hata kinywaji, then warudishe nyumbani, kweli siku hiyo mtoto ataenjoy sana, sio mtoto ametoka sana, kaendashule, akirudi kucheza cheza nyumbani, wala hainogi, na hii huzidisha sana mapenzi kwa watoto wetu, sio unakuwa busy kiasi kwamba siku ukishinda nyumbani tu! watoto wanakushangaa na kumuuliza mama, ''baba anaumwa''
hebu jaribuni jamani, muone watoto watakavyojiskia vizuri,




Friday, May 28, 2010

POLENI KWA KUWACHUNIA JAMANI, NILIKUWA NAUGULIWA




Jumapili hii nilikuwa hospitali, Twins wangu walikuwa wanaumwa,  walikutwa na malaria, 
but, many thanks to God, coz wamepona na wako shwari kabisa, kazi ya kuzaa wala sio kubwa
kiviiiiiileeee, issue iko kwenye kulea we! usipime,

tena hawa wawili ndio bonge la issue, maana kila nitakachofanya kwa huyu, basi na huyu nae lazima nimfanyie, nilijaribu siku moja kwa makusudi tu!  nikamnunulia Tymon nguo Trace nikamchunia, we! mbona nilijuta kuthubutu!

mtoto alinililia hadi nilijiskia vibaya, tena alivyo mpanaaa  mtoto huyu, akagoma kukaa na sisi ndani akatoka akaenda kukaa nje kwenye kona ya nyumba peke yake, nikamfata nambembeleza aingie ndani akagoma,

anasema ''mama wewe si haunipendi na mimi sikupendi' nikamwambia nakupenda sana mwanangu, ''wewe ndio dada mkubwa, akanibana tena ''mbona mimi hujaniletea nguo kama tyimo? nikamdanganya baba yako kasema anakuletea ndio maana sijanunua. ndio akakubali kuingia ndani, alipofikia tu kaanza kumchimba mkwara Tymo,'' usikae na mimi kakae na mama yako, namimi namsubiri baba yangu''.
 ila ilinibidi nimwambie baba, lete nguo ya Trace mwenzio nimeyakoroga huku.
akaletewa akawa na amani.

hata kuumwa, mara nyingi unakuta kidada kinaumwa, baada ya muda kidogo kaka nae anaanza vilevile, but all in all uzima wao ndio furaha yangu, wakofresh kabisa sasa hivi,
 tupo pamoja dears, nawapenda sanaaaaaa

weekend njema


Friday, May 21, 2010

JE HUYU KWELI NI MUME WANGU


Wapenzi wa Blog hii nzuri.Mimi ni mwanamke wa miaka 33, nina watoto 2 wa kike na wakiume.

Ninaishi na mume /baba watoto wangu tangu mwaka 1996 january., nilipokutana nae alanieleza kuwa ananipenda sana na anataka kunioa. Mimi nilikuwa na boyfriend wangu na yeye alikuwa na girl friend wake, kwa kuwa tulipendana tukakubaliana kila mmoja wetu avunje mahusiano na mwenzie ili tuwe huru kufunga ndoa ambapo wote tulikubaliana na kuacha na hizo dates zetu na kuconcetrate na maamuzi yetu mapya.

Mwaka 1999 mwanzoni nikawa nimepata mimba ya mtoto wetu wa kwanza..Tukapanga taratibu zote za mahali na hatimaye akaja kwetu akatoa mahali kwa sherehe kubwa sana. Baada ya Mahali tulipanga siku ya harusi. lakini baada ya hapo, wakaleta kwetu barua ya kusogeza mbele harusi kidogo mpaka nitakapojifungua.. nilijuwa Mume wangu alikuwa na nia sana lakini nikagundua hilo lilikuwa ni shinikizo la baba yake mzazi, na kwamba yeye hakuachana na huyo girl friend wake, na ambaye na yeye alikuwa mjamzito kwa kipindi hicho ambacho mimi pia nilikuwa mjamzito

kwamaana hiyo huyu mume alikuwa anakula huku na huku..Basi mume huyu aliendelea kunihudumia kwa hali na mali na kusema kuwa nisijali ananipenda sana na ndio maana kanitolea mahali.(wakati huo wote sikuwa najua kama anaendelea na huyu girlfriend wake)

Tuliendelea hivyo mpaka tukaanza kuishi wote na kujenga pamoja. .kumbe na huku kwa girlfriend wake nako alikuwa anajenga. Mpaka hapa ninaongea na wewe bwana huyu anaishi kwa mitara. leo kalala kwangu kesho kwa huyo mama na anawatoto nae WANNE. Kitendo hichi kimekuwa kero sana kwangu kiasi naona kama siishi kwa amani. na magomvi yasiyoisha..Huyu bwana ananiregard mimi kama mke mdogo kwake cos nina 33 na yeye 43 huyo mama ana miaka 42years. Kwa hiyo mimi ndio nachukuliwa kama mke mdogo

Hayo ni machache sana nisiwachoshe.Wapendwa kwa busara zenu kama za mfalme Suleiman naomba mnishauri kama huyu ni mume wangu au ni wa mwenzangu? je nina haki nae gani??au nifanye nini?? Huwa nasikia wanakwenda kwenye baadhi ya sherehe pamoja, inaniuma sana sina furaha hata kidogo, kwani alivunja makubaliano yetu na kunidanganya, ila kwakuwa nilimpenda niliamini kuwa nae atavunja mahusiano ya nje kama nilivyofanya mimi.


NISHAURINI NILIYEVUNJIKA MOYO



 


Wednesday, May 19, 2010

KILA NIKIFANYA NAE MAPENZI- NAPATA MAUMIVU MAKALI SANA


Dada violet, pole na kazi, nahitji msaada wako kama utaweza kunisaidia nitakushukuru sana, pia kama inawezekana weka kwenye blog yako (ila usinitaje jina) ili niweze kupata ushauri zaidi,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, niko Zanzibar, tangu niwe mwali hadi leo nimekutana na wanaume wawili, mmoja aliniacha, kwa sababu ambazo hata sizielewi Mpaka leo hii na alinitamkia kabisa sina sababu ila tu sikutaki tena, iliniuma sana nilitamani hata kujiua, ukizingatia niliweka nadhiri kuwa atakaenibikiri ndie atakaenioa, lakini akawa ameshapotosha ndoto zangu,

Baada ya muda nikiwa chuo, nilipata boyfriend mwingine, ambae niko nae hadi sasa, cha ajabu kila ninapokutana nae, tukimaliza tu! Huwa naumwa sana hadi nameza dawa, yani akishaniambia kesho tutafanya mimi nitalala nawaza usiku kucha, Napata maumivu makali sana huku chini na maeneo ya kwenye kinena panauma sana, huwa naumia hata saa zima na jasho linanitoka kabisa

Huyu boyfriend wangu hadi anaogopa kunigusa, sasa nawasiwasi asije akashawishika kuwa na mwanamke mwingine, nampenda sana, na hata kwetu wameshamjua bado kuja rasmi tu!,

Aliwahi kunichukuwa kunipeleka hospitali moja huku huku Zanzibar, dada violet nilipimwa kila kitu, lakini hakukuwa na tatizo, hata daktari alishangaa, yani alichukuwa vipimo vyote, lakini hakukuwa na tatizo, siku ingine tena tulisafiri nae kwenda Kigoma, tulipofika tulilala pamoja hotelini, alivyonifanya tu! Sikulala hadi kunakucha, kiuno kinauma hadi miguu, asubuhi alinipeleka hospitali kule kule kigoma, napo wakaniambia kuwa sina shida

Tukakaa kama wiki mbili baada ya kutoka hsptl tukafanya tena, maumivu pale pale, nikaenda hospitali ingine tena kwa mara ya tatu, napo wakasema kuwa mimi sina tatizo lolote, wakampima hata na boyfriend wangu wakasema pia hana tatizo,

Hadi sasa sijielewi, maana nakosa kitendo cha muhumu kuliko vyote, naumia sana na hasa wasi wasi wangu ni kwamba huyu boyfriend wangu atanikimbia, Napata taabu sana naombeni mnisaidie nifanye nini? nawaza labda tatizo linaweza kuwa kwangu ndio maana hata mwanaume wa kwanza alinikimbia bila sababu



Monday, May 17, 2010

MCHUMBA ALINIACHA MWENYEWE- SASA ANATAKA TURUDIANE TENA, NIFANYAJE


Napenda sana ushauri wa watu na naamini utanisaidia sana, mara nyingi huwa napita ktk blog yako japo huwa sichangii, lakini sasa kuna tatizo lililonikuta, na sina ufumbuzi, nahitaji msaada wa mawazo sana

Nilikuwa na girlfriend wangu tuliekuwa tukifanya kazi pamoja na tulikubaliana kuoana, badae nilimtafutia kazi yenye maslah mazuri zaidi kwa nafasi yake ofisi nyingine, basi akaacha pale na kwenda kule kwa nilipomuunganishia. Alieniunganisha katika ofisi hiyo ni rafiki yangu mimi anaefanya kazi pale

Nilimtambulisha mchumba wangu kwake, akamfahamu, na hata wakati tunapeleka mahali kwao, nae alitusindikiza, kinachonitatiza ni kwamba, huyu mchumba wangu amebadilika gafla sana, yani mapenzi yamekwisha kabisa, kitu kidogo tu anakasirika sana, inakuwa ugomvi mkubwa, wakati hakuwa hivyo hapo zamani, kuna mfanya kazi mwenzao mmoja pale aliwahi kunitumia sms na kusema kuwa mchumba wako sio mwaminifu anachukuliwa na rafiki yako. Nilipomuuliza alikasirika sana na kukimbilia kunijibu kuwa kama nasikiliza watu basi tuachane, kwakuwa nilimpenda sana, niliamua kuwa mpole tu

Sasa niezi kama mitatu hivi iliyopita nilikuwa nimelala usiku sana akanitumia sms kwamba anaenda kuwaambia kwao wanirudishie mahali, yeye hataki kuolewa tena, nilishangaa sana, usiku ule ule nilimpigia sim kutaka kujua sababu, akawa hapokei, sikulala hadi kunakucha, asubuhi nilimtafuta kwenye simu tena ili aniembie tatizo, safari hii alipokea ila akasema hataki hata kuonana na mimi, nilibembeleza sana lakini alikataa na badae kuanza kukata simu. basi nilifikisha kwa wazazi/washenga, wazee wangu walinishauri kuwa hata hiyo mahali niiache iwe kama nimeitoa sadaka,

Nikamtumia sms nikamwambia sawa, lakini juwa umenitesa sana, nami nikaamua kufata yangu, violet kila nilipokuwa nikikaa nilikuwa nikikumbuka mazuri mengi niliyomfanyia, muda niliopoteza kwake, bado kanilipa ubaya, da!

Niliamua kuanza maisha mapya, sasa juma pili kanipigia simu anataka aonane na mimi, mimi sikutaka kumlipa ubaya, nilikubali, tukakutana pale Santina restaurant, anachokiomba kwangu, anataka turudiane nae. Anasema toka ameniacha hana raha, ni mtu wa majonzi, mikosi na hana furaha hata kidogo, sasa hadi sasa sielewi cha kumjibu, ila mimi kwake mapenzi yamepungua sana.



Saturday, May 15, 2010

WEEK END NJEMA JAMANI


jamani nawatakieni wooooote weekend njema wapenzi wangu, tukumbukane katika maombi jamani, maana hali ya sasa inatisha, tukumbuke familia zetu, waume zetu, watoto wetu, marafiki, na majirani pia,
 mie leo nina Mtoko mwenzenu,
tunaenda hukoooooo kumfundisha mwali jinsi ya kuishi na mume, asiende kutuabisha huko!!!!
hahahahahaaaaaahaaaaaaaaaahaaaaaaaaaaaaa, kazi  kwel kwel,
nawapenda wooooote


Thursday, May 13, 2010

AMESEMA HANIOI HADI NIZAE, NA WALA SISHIKI MIMBA, NAWEZA KUWA TASA??


Hello Dada Violet,

Pole na kazi za nchi hii pamoja na kutusaidia sisi.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 na ninaishi na mchumba wangu. Tumeishi kwa miaka miwili sasa, sijabahatika kupata mimba. Ila dada Violet nina tatizo moja ambalo linaninyima raha kabisa. Huwa sizioni siku zangu naweza kukaa mwaka mzima nisizione.je inawezekana kuwa mimi ni tasa?? Na mchumba niliyenaye yupo tayari kunioa lakini ndio anataka nipate mimba kwanza je kuna uwezekanano wa mimi kupata mimba kweli??

Nipo njia panda sitaki kuteseka baadae nikiingia kwenye ndoa.
Hali hii inaniumuza sana, naombeni ushauri wenu


Tuesday, May 11, 2010

NINAISHI KWA KAKA YANGU, ILA SINA FURAHA HATA KIDOGO SABABU YA WIFI


Dada violet habari za kazi?Nashukuru sana kwa blog yako maana tunapata ushauri wa
kutujenga sisi wanajamii.
Mimi ni Mischana mwenye umri wa miaka 26 nipo Tabora.Mkasa wangu ni kwamba naishi na kaka yangu pamoja na wifi yangu.Kaka yangu ana uwezo mzuri tu na amejenga nyumba kubwa na nzuri.

Sasa dada violet pale kwa kaka tunaishi na mdogo wake wifi yangu wa kike na tunalingana kiumri. Kwa sababu sis ni wasichana tunakaa chumba kimoja ila cha ajabu Yule huyu mdogo wake wifi yangu nafanyiwa vitimbi vya ajabu ajabu sana ambavyo sijui vinatokea wapi, ananichukia kupita kiasi.

Yani hataki kabisa kuniona pale, wakati yeye ni kwa dada yake na mimi ni kwa kaka yangu, hanipendi hata kidogo. Akiona nimevaa vizuri ananiangalia vibaya ila mimi sijui hili wala lile.na ameanza kutengeneza chuki kwa wote tunaoishi nao pale ndani mradi wanichukie tu, hata msichana wa kazi amemwambia asiniheshimu asiongee na mimi na kunisema mengi sana kwa msichana huyo ambayo yananichafua mimi.

Nikiwa nyumbani huwa siku nzima ananuna na haongei na mimi anaweka nyimbo za taarabu tu, mafumbo mafumbo mengi sana. Na tunaweza kuwa chumbani hakuna anaeongea na mwenzake.

Jamani nimechoka niliwahi kumwambia kaka nataka kutoka nikapange akasema bado sina uwezo wa kujitegemea na ananipenda sana. Kugombanisha ndoa ya watu sitaki na nawaza nikiondoka kwa nguvu kaka hatanisaidia tena ataona nimemdharau.

Dada zangu/Ndugu zangu naombeni ushauri wa wenu wapenzi wangu.Dada Violet naomba usinibanie ili nipate mawazo kutoka kwa wadau wenzangu. Hii blog nilipewa na rafiki yangu na namshukuru sana maana inanifundisha mengi. Dada nina huzuni moyoni hadi basi sina raha hata kidogo.



 

Monday, May 10, 2010

WAKWE WALIMTAFUTIA MKE MUME WANGU, KISA SIZAI, SASA NIMEZAA BADO HAWANITAKI, NIFANYAJE?

yamenikuta mwenzenu
nakupongeza dada violet kwa blog yako ambayo inatufanya tupate mawazo tofauti tofauti ya kutusadia wenye shida, nakuombea Kheri ndugu yangu.
Niliolewa miaka 8 iliyopita huku Njombe, nilipoolewa nilikaa miaka mitano bila kukamata mimba, nilihangaiika sana, nilienda kwa waganga wa kienyeji, nikatumia mitishamba lakini haikusaidia, ndugu wa mume wangu walianza kunichukia sana na hata mume wangu pia,
miaka mitatu iliopita, mume wangu aliniomba msamaha kwa kusema kuwa amezaa na rafiki yangu, rafiki ambae alikuwa akinificha sana kila nimuulizapo mimba ya nani, hakuwa akiniambia ansema mwenye mimba yuko nje, alipoenda kujifungua kwao singida aliporudi hakufikia pale, nikasikia amefikia kwa wakwe zangu,
nilishangaa sana, hao wakwe mimi wamenipiga marufuku hata kwao nisikanyage

wifi yangu mmoja akaja kuniambia yule rafiki yangu amepangishiwa chumba mahali, nililia kupita kiasi, lakini nilijipa moyo, huyu kaka tulichukuana tu hatukufunga ndoa, mume wangu alianza chuki na maneno ya kashfa kwangu, nilivumilia tu!,
mwaka jana nilipata ujauzito, namshukur mungu nilijifungua salama, na mtoto alikuwa amefanana sana na baba yake, badala ya kufurahi, nilishangaa mume wangu hakuwa na mapenzi na huyu mtoto hata kidogo,
ss mwaka huu mwanzoni nikaambiwa kuwa wameachana na yule mwanamke, na mtoto kaamua kumpeleka kwao, baada kama ya wiki, nikaletewa mtoto nyumbani, mimi nilikubali nikawa namlea
ss nimeletewa taarifa kuwa wamerudiana na yule msichana, mapenzi moto moto na wanataka kufunga ndoa,
yani kila nikiwaza hata sipati jibu mwenzenu, sielewi pa kuanzia wala pa kuishia,
huyo mtoto hadi sasa niko nae hapa nyumbani kwangu, na habari hizi ni zaukweli kabisa, maana niliambiwa na mshenga, kwamba nijiandae kama nina pa kwenda niende, maana huyo rafiki yangu (mke mwenza) atakuja kuishi hapa hapa na mimi
inaniuma sana

Wednesday, May 5, 2010

MUME WANGU ANANITEGEMEA KWA KILA KITU- LAKINI HAJATULIA HATA KIDOGO- NIMWACHE?

Du! jamani kuna wanawake wenzetu wanashida sana jamani, hebu soma hii, maana mimi imenisisimua sana, na imeniumiza pia, ametuma ndefu sana, nimejaribu kuedit kiasi, but soma kisha mshauri, yani nawaza kama ndio ningekuwa mimi sijui ingekuwaje, yani sipati majibu maana kichwani yanakuja mfururizo kama majibu kumi hivi but yote yana madhara at the end, inasikitisha sana
Nimeolewa, miaka mitatu iliyopita, lakini nilimkuta mume wangu anawatoto watatu, binti wa miaka 16, na  wa miaka 10 na miaka 6, mimi sikuwa na mtoto hata mmoja, mama wa watoto hawa alifariki.

Tumefunga ndoa ya kanisani, sikubahatika kuzaa mapema, ila kwa sasa ndio nina ujauzito wa miezi saba, Nilimpenda sana mume wangu,Mimi nafanya kazi nzuri tu, ila mume wangu hana kazi yeyote ile, maana alifukuzwa, hivyo nafanya dili zake tu za pembeni zinazofanya aishi hapa mjini, aliponioa alihamia kwangu, maana yeye alikuwa amepanga, mimi nimejenga, hivyo tulikubaliana aje kwangu na nilikubali aje yeye na familia yake,
 nilimtafutia biashara, mradi tu! Asiwe anakaakaa nyumbani , akafungua duka la nguo za kiume huko mjini, na bila hata uoga alimuweka girlfriend wake awe ndie msimamizi na muuzaji, yeye ndie controller wa kila kitu pale. nilipogundua niliifunga ile biashara. Toka siku ile niliapa kutomsadia lolote lile.

Ni Malaya kupita kiasi, nilishawahi kumfumania na wanawake zaidi ya watatu, kuna mwingine alimpangishia na chumba akawa anaishi nae kutwa nzima, na hivi hana kazi akawa anatoka asubuhi anaenda kushinda huko, jioni anarudi kulala kwangu, nilipogundua nililia sana violet mdogo wangu niliumia sijapata kuumia vile katika maisha yangu, nilimpokonya gari nililokuwa nimempa, nikawa simpatii hata pesa. sikuona maana ya kumjali mtu asieniheshimu, lakin kama mjuavyo mapenzi tena, nikaamua kumrudishia gari ili watu wasihis kitu kwa kuona limepaki nayeye anatembea kwa miguu.

Nashukuru Mungu watoto hawa wananiheshimu na kunipenda sana, watu wengi wanajua kuwa nimewazaa mimi mwenyewe, nami nawapenda sana, Nilimfumania kabla sijabeba hata mimba, sasa mwezi uliopita nimepigiwa simu na mwanamke mmoja akanitukana sana, isitoshe amenitishia kabisa maisha yangu, anasema ataniroga nitazaa mbuzi, na maneno mengine makali sana, yani hadi huwa najuta,

Violet, hapa nilipo mimi ndio kila kitu, najua ni ngumu sana kuamini kuwa mimi ndie ninaesomesha hadi watoto wake, nawalipia ada na kuna mmoja huyu wa kati, nimempeleka boarding namlipia mimi, huyu mkumbwa nae yuko private (secondary) nalipa mimi. huyu mdogo mimi pia nimempeleka Tusiime ( international) namllipia mimi, moyo wangu unaniuma sana, kwanini anitese hivyo? Inamaana hanithamini mimi wala wema wngu kwa wanawe?

Wale watoto ni damu yake yeye, watamsaidia yeye sio mimi? Niliahidi kuwasaidia kwa moyo wangu, maana nilipoolewa mimi nilikuta watoto wana hali ngumu sana, waliona kama wamepata mkombozi wao, Sasa yeye nikimuuliza kwanini ameshindwa kufanya hata kwa siri tu umalaya wake, mimi nisijuwe, kwanini ananidharirisha, mimi nampa heshima zote, nampa matumizi yake binafsi, namlelea watoto wake, gari namtilia mafuta, lakini anakwenda kuwapakia wanawake wengine, wanapanda kwenye gari yangu,

hana cha maana anachonijibu ninapomuuliza, yeye anasema hawajui, mimi nakataa maana nilishawahi kukuta hata sms za mapenzi, anawatambua maana kuna mambo yangu mengi ya ndani tunayopanga mimi na yeye tu chubmani, cha ajabu huyo mschana  anayafahamu, hilo ndilo linalonipa hofu, wasije wakayatumia hayo kuniumizia kiumbe changu, sasa naomba mnishauri, nifanye nini? Nimfukuze?

Moyo wangu umechoka sana jamani, moyo unaniuma sana, kwanini iwe hivi? Hali hii hata kujifungua bado, nimeanza kutishiwa eti nitazaa mnyama(mbuzi) sina hata nilichowakosea,

Ananitia aibu kwa majirani, maana mtaa mzima wameshamjuwa kuwa yeye ni malaya, cha ajabu anachukuwa visichana vya ajabu ajabu, havina kazi wala pesa, vinamtegemea yeye kwa kila kitu. vikorofi, midomo imejaa matusi, na hata elimu havina, aibu hii mimi hadi lini? inaniuma, nimekuwa nikilia kila siku!

 



Tuesday, May 4, 2010

NATAMANI KUOLEWA ILA SIJAWAHI KUMPATA HATA WA KUTAMKA TU!

(mnisamehe jamani, wiki iliyopita nilikuwa busy kupita kiasi, nikawa naona masaa yanayoyoma tu hata blog sijaigusa, lakini nshamaliza nilichokuwa nakifanya, im back wapenzi)

msaada wa mawazo yenu ni muhimu sana kwangu,
mimi ni mschana, sijaolewa bado, na nina umri wa miaka 32, nina kazi nzuri tu ambayo inaniwezesha mimi kuishi vizuri, ila nina shida moja, ambayo sijui kama dada violet na wengine mnaweza kunisaidia au hata kuniambia ni kwanini inanitokea hivi,
  
  mimi ni mzuri, nikijitazama, na pia sina ulemavu wowote,  nafanya kazi nzuri, na naishi nyumbani kwangu,
wazazi wangu wako Nairobi, ndiko nilikokulia, ila kazi nafanya hapa Dar es salaam,

katika maisha yangu sijawahi kupata mwanaume wa kuniambia anataka kunioa hata siku moja, hata nikimpata tu! tunakuwa marafiki kwa muda, then wanakimbia, ukimpigia simu anakata, sometimes hata kupokea hapokei, hadi nachoka na hatimae kuachana, naweza ingia gharama ya kumuhudumia mwanaume nitakae kuwa nae, kwa kila kitu, lakini nikishajiweka karibu yake, na kumuuliza lini tutafunga ndoa,  huwa  ni kama nimemwonyesha bomu,

niliwahi kwenda kanisa moja hivi, nikaombewa maana walisema ni laana ambayo inabidi ivunjwe, niliombewa sana, lakini since there, no any changes, nimechoka kuhudhuria na kuchangia harusi za wenzangu, wakati mimi nazeeka tu!, staki kuzaa nje ya ndoa, na staki kuishi na mwanaume nje ya ndoa,

natamani na mimi niitwe Mrs. fulani, huwa nakaa nalia sana peke yangu, najiona kama mwenye mkosi fulani.unakuta mwanaume natokea kumpenda sana, nitaonyesha njia zote za kumtamani kimapenzi, lakini tutaishia out tu!na hakuna kitakachofatia hapo. sasa sielewi, kama ndio nimeumbiwa kupata shida hii, unakuta natamani kumwambia mtu kuwa nampenda, ila nakuwa nashindwa kwa kuhofia jamii itanichukuliaje, lakini hali hii inanitesa sana, kwa msichana wa umri wangu, ninaeelekea kwenye umama, bila kuwa na mtoto wala mume





Wednesday, April 28, 2010

MUME WANGU HAJUI KUBEMBELEZA NA HATAKI KUBEMBELEZWA-HATA KITANDANI


Pole na kazi Violet, nimetuma email kama nne hivi, sijaona urushe, ss sielewi ulikuwa huipati au mimi nilikuwa nakosea address?

Tatizo langu ni kwamba mume wangu hajui kubembeleza hata kidogo, yani yeye anafoka masaa yote, na huwa hamalizi jambo, yani analibeba na kulikuza, na atalitumia hilo kukuumiza kila unapokosea,

Hali hii inaninyima raha sana, natamani sana kubembelezwa kama wenzangu, nawatamani sana, yani hata kitandani, utakuta mimi namshika shika, namramba, namchezea sana, lakini yeye anakuwa mgumu utadhani askari aliehisi kuna jambazi pembeni anamvizia, hatikisiki wala kupokea upendo wangu,

Niliwahi kutoka nae na kumueleza ninavyojisikia, akasema tatizo lako wewe nini? Kwani huwa sikufanyi ukaridhika? Mwanzoni hakuwa hivyo, yeye anafanya kazi mimi sifanyi, basi hata ukimpigia simu kama unashida, vile anavyopokea ni kama mligombana, badala ya kusema haloo anasema ehe unasemaje? Sasa ile mimi siipendi kabisa violet, inaniumiza sana

Pia tunapokuwa kitandani, nikitaka kumpa denda, anakuwa kama ananionea kinyaa hivi, nikimnyonya maeneo ya makwapa anakuwa kama ananisukuma hivi wakati hizo ndizo zilikuwa sehemu zake, zamani ukimnyonya sehemu ya kwapa tu! Analegea sana na analia kama mtoto mdogo, violet, situkani wala sitanii, hali hii inaninyima raha, na hata kunipa dozi ni kwa kifupi sana, yani dakika mbili tu amemaliza na hataki kurudia tena, sasa unakuta mmi nakuwa bado nina hamu, naishia kugugumia tu wakati huo yeye anakoroma pembeni, sasa hii si mitego hii? Nikitafuta mwanaume mwingine anikoreze nitakuwa nimekosea? Au nifanyaje?
pia unaweza kuwa unamuelekeza jambo la muhimu na kwa upendo tu! lakini anakuwa kama hakusikilizi, na anaweza fanya hivyo hata mbele za watu, ananitia aibu sana,


Friday, April 23, 2010

NAMNA YA KUWEKA NYUMBA KATIKA HALI YA USAFI







Mara nyingi tumekuwa tunajitahidi kufanya usafi kwenye nyumba zetu. Ila kuna mambo kadhaa huwa tunayafanya kwa uvivu sana ama ni mara chache sana wakati tunasafisha nyumba zetu. Hata maelekezo ya usafi kwa mahousegal/boy huwa hayalengi sana hivi vifatavyo.

1 Hakikisha unatoa nje kapeti la sebuleni unalipiga piga kuondoa vumbi na pia kusafsisha pale sakafuni kwa kuwa pia vumbi hupenye na kutuama chini. Hii ni kwa yale makapeti ya kisasa. Kutofanya hivi kumesababisha kuwa na tatizo la kudumu la kuugua mafua nyumbani bila kujua chanzo na kuona ni kama kawaida tu pale nyumbani.

2 Hakikisha unabadiri mapazia kadiri unavyoweza au kufua mara kwa mara  ili kuondoa mavumbi yanayonasa kutoka nje yarushwayo na upepo. Hii hufanya nyumba kuwa na hewa safi sana. hata kufurahi kukaa chumbani ama sebuleni hata kama ni joto. Si wajua Dar bila joto haijakuwa Dar. hahahahaha

3 Pia kumbuka sana kufuta vumbi lililopo kwenye zile nyavu za kuzuia mbu kwenye dirisha. Tena zile huzuia sana kuingia mbu ndani na hata vumbi, kwahiyo huwa na uchafu mwingi sana unaopunguza hewa safi ndani. Hewa huwa nzito sana na hata kuongeza maumivu ya kichwa. Hapa naweza sema Carbon inatengenezeka. hahaha Bios hiyo.

4 Jambo lingine ni kuhusu viatu, huwa tunavipenda sana viatu vyetu lakini hutchafulia mazingira ya ndani na kuleta taka ndani, bila kusahu harufu mbaya(Vinatema) Inashauriwa viatu viwekwe mahali karibu na mlango wa kutokea au kuingilia. Hii huzuia uchafu kuingia ndani na hata hewa ila mbaya isisumbue ndani na kusababisha makazi kuwa mazito.

5 Hii ni ya mwisho lakini sasa ngumu kiasi hasa kwenye mifumo dume. Kama kaka au baba wa nyumba ni mvuta sigara, aahakikishe ana vuta sigara zake nje kama Mita 15 kutoka eneo la nyumba. Mara nyingi moshi wa sigara hasa utokao mdomoni ndio unamatatizo sana hasa kwa watoto. Yapaswa kushauri wavutaji pale nyumbani watoke nje kwa umbali fulani kisha wamalize hamu zao kisha warudi ndani.


Chanzo cha habari hii ni  lifestyle.msn.com Decor and Organizing.








Wednesday, April 21, 2010

ITAKUWAJE UNAOMBA HOSPITAL FULANI WAKULETEE AMBULANCE

HALAFU WAKATI UNACHUNGULIA DIRISHANI KAMA WAMEFIKA UNAONA KAMA HII....




Kaazi kweli kweli!



DEARS

wapendwa wangu mnaonitumia sms kwamba siirushi mikasa yenu mliyotuma, nataka niwaambie kuwa sijaipata, inawezekana mkawa mmekosea email adress, coz kama mnakumbuka niliwahi kuwaambia kuwa nimebadilisha email adress, so kwa sasa natumia violet.gerald@yahoo.com , kama hamkutumia hii basi mjuwe sijaipata, mbona mikasa mingine naipata fresh tu! kama vipi angalieni vizuri mtakuwa mmekosea email adress.

Tuesday, April 20, 2010

RAFIKI ZANGU WANACHUKULIANA WAUME BILA WAO KUJUA, NIKISEMA NITAKUWA MMBEA?


Kuna kitu kinanichanganya sana, hakinihusu mimi lakini kinawahusu watu muhimu sana kwangu, nina marafiki wawili, na ni wamama wenye familia zao na nimajirani zangu,  ss mmoja kati yako anatembea na mume wa mwenzie wakati wote wawili ni mashoga zangu, ila huyo anaeibiwa hajui kama huyu rafiki yangu mwingine anamchukuwa mumewe, na huwa anamchekea kabisa na kujifanya rafiki yake, wanaongea vizuri sana,

Nilishawahi kumuonya huyu rafiki yangu, kwanza ukizingatia sisi ni majirani, pili huyu akisha kuja kujuwa itaniweka mimi pabaya sana, naona bora hata asingeniweka wazi juu yahili maana linaniumiza sana, kwakuwa huyo mwanaume ameshanogewa na penzi la nje, ameshaanza kujisahau, anamtesa sana mkewe , anampiga sana, anatishia kumfukuza, kitu kidogo tu kwake linakuwa kubwa, huyo dada huwa akipigwa na kufukuzwa anakuja kwangu, akifika kwangu anajieleza sana, na kusema nahisi mume wangu ana mwanamke mwingine,

maana mwanzo hakuwa hivi, anachowaza ni sahihi na mimi nalijuwa hilo, kinachoniuma zaidi sikumoja alipigwa sana mumewe usiku, akakimbilia kwangu, akamkuta na huyu mwizi yuko kwangu, akaanza kutueleza, nilimuhurumia sana, nikamwambia vumilia tu! lakini huy mwenzangu ambae ndie muhusika wa tukio, akawa anamshauri aondoke, aliniudhi sana na huwa namsema sana, lakini hasikii, najuta kwanini nimelijuwa hili, bora ingekuwa siri yao tu!
sasa  kumwambia kuwa chanzo ni fulani,  nashindwa maana wote ni mashoga zangu, Sasa hebu nishaurini, nimwambie tu liwalo na liwe, au nitaitwa mmbea niwaache tu mwenzie huku pembeni anajifanya anampenda, inaninyima raha sana hii.

Thursday, April 15, 2010

PETE ZA NDOA ZINA MAANA GANI KUVALIWA MKONONI?

mh!jamani ni vizuri kwa wajuao wakatuelewesha tusio jua kama mimi, ili nasi tukajua, ni kuhusu pete za ndoa, ambazo now adays zinavaliwa hovyo kama fassion tu!,mtu anavaa as if it was made for decoration,
first time nilikuwa najua pete ya ndoa haitakiwi kuwa na marembo yeyote yale, inatakiwa kuwa plain tu! iwe silver/Gold lazima iwe plain, but i was wrong, coz siku hizi watu wanavaa hata pete za ndoa zenye marembo rembo, na padri anazibariki na watu kuvishana,
yaweza kuwa Gold,

yaweza valiwa silva kama hii, mradi ni pete,

ss pete zinavaliwa kwa ajili ya nini, zina maana au ni pambo la mikononi tu! tena nijuavyo mimi pete ya ndoa ni ya muhimu kuliko hata ya uchumba, maana hata kanisani unapovalishwa pete ya ndoa unatakiwa kuvua hata hiyo ya uchumba uliyoivaa,

hebu tuwekane clear juu ya hili, maswali ambayo huwa najiuliza sana, kama pete ya ndoa ni muhimu mbona wanandoa wengi hawavai? tena sana sana wanaume, hawapendi kabisa kuvaa pete, akitoka kanisani tu! siku ya ndoa basi inawekwa kapuni, hapa ndio ninapo hisi kwamba labda hazina maana
lakini sasa kama hazina maana, kwanini wachungaji kanisani huzibariki, na hata kama ikipotea ukachonga ingine inatakiwa kubarikiwa kwanza? hapo ndipo ninapokuwa confused, hebu tueleweshane juu yahili, ni wengi nakutana nao amevaa pete ya uchumba, au ndoa, unaweza kumpa pongezi , he! umeolewa au unamchumba, hongera, naona pete mkononi, anakwambia ah! ni pambo tu! nasisi tuvaage,
wewe unalionaje hili? 




Tuesday, April 13, 2010

MAMA MKWE ANANIFANYA NITAMANI KUIVUNJA NDOA YANGU- NISAIDIENI

jamani wapendwa wangu, kuna huyu mwenzetu,anahitaji ushauri wetu sana, kusema kweli story yake imenihuzunisha sana, nindefu kidogo, nimejaribu kuiedit kiasi, but tuisome tuilewe ndio tumshauri

Pole na shughuri mdogo wangu, shida yangu ambayo kwakweli nahitaji msaada wenu, ni kwamba, mimi naishi hapa dar es salaam, huku kigamboni, nimeolewa na nina mtoto mmoja wa miaka 3,nilichelewa kuzaa 


Toka nilipoolewa niligundua mama mkwe hanipendi, upande wa mume wangu wamezaliwa wawili tu, yeye na dada yake, ambae anamatatizo ya akili, ana miaka kumi na nne sasa, yani kilema chake hawezi kufanya lolote lile, ni udenda tu unaomtoka masaa yote,
Wakati tunafunga ndoa tulikuwa tumepanga vyumba viwili, mama mkwe wangu akija alikuwa akilala kwenye chumba kingine ambacho nilikifanya kama sebule, anakaa hata miezi mitatu ndio anaondoka, ila ndani ya hiyo miezi mitatu, yani mimi nilikuwa napungua hata mwili, ni mkorofi sana, mwanzoni mume wangu alikuwa upande wangu, alikuwa akinitetea kwa mama, lakini sasa hivi wote wamenigeuka, tangu mume wangu alipokuwa rikizo akaenda kwao, mimi sikwenda kwa ajili ya kazi, basi alikaa mwezi mzima, aliporudi tu! Mambo yakawa mabovu kupitiliza,


Ni kama mtego aliporudi alikuja na huyo dada yake mwenye mtindio wa ubongo, ili niishi nae na kusema maisha ya kijijini na umri wa mama umeenda hawezi kumlea hy bintie , nimeletewa huyo wifi, ni wa kumbeba, hachuchumai kujisadia, wala kupiga mswaki wala nini, akitaka kunya anayaachia tu, mimi nikirudi nafuwa, mahousegilr zaidi ya watano wameondoka wanasema hawawezi kukaa kwa ajili ya ile kero,


Mama mkwe huwa anakuja mara moja moja, na akifika tu! Anaanza vijembe, mara mwanangu ameisha sana, hali vizuri, mambo mengi sana, niliwahi kuongea na mume wangu, nikamwambia huyu jesca kwanini tusimpeleke kule wanakolea watoto wenye hali kama hii? Akakataa, akasema wanapelekwa wasio na ndugu, nimlee tu, na kama sitaweza niondoke mimi. Inaniuma sanahii, na nikiondoka nani atamsadiia


Mume wangu ni muislam, na mimi ni mkristo, kunasiku wote tulikuwa kazini, Yule binti mlemavu wa akili(wifi yangu) alipata kama kifafa vile, akaanguka na kutapatapa, housegirl wangu alikimbia kwenye nyumba ya jirani yetu(mlokole) wakaja kumfanyia maombi, alitulia, niliporudi ndio nikapewa taarifa ile, basi mimi nilimuhadithia mume wangu aliporudi kwania njema tu, violet nilipigwa mimi na housegilr wangu, tulipigwa sana, kesho yake msichana wangu aliondoka kurudi kwao, nikaachwa na mtoto wangu tu! Akaagizwa mama mkwe akaja, waliweka kikao walinisema sana

Nilimwambia mume wangu basi tuwe na wasichana wawili, wa kumlea huyu mdogo wako, na wakumlea mwanangu wote wawili nitawalipa mimi, lakini alikataa nakusema kuwa najifanya nina pesa, ataniachisha kazi, sasa jamani hadi sasa hvi mimi sijui cha kufanya, nilimshauri basi tumpeleke mtoto boding alikataa, sasa niambieni wanandoa wenzangu, nifanye nini? Hamna amani nyumbani, kila siku ugomvi, kipigo, mama mkwe anakazana tu kuwa nina roho mbaya, dini yao inaruhusu mimi kuachwa au kuolewa mke mwenza, na mume wangu anasema kama nimechoka kumuhudumia dada yke basi nikubali aoe mke mwingine wa kumuhudumia jesca, nawaza niondoke na mtoto wangu, au niendelee kukaaa? Au nifanyaje jamani? maana sometimes huwa nahisi kama vile wao ndio walimuharibu akili, kwanini hawataki apate msaada wa maombi





 

Friday, April 9, 2010

LO! SASA JAMANI HUYU DADA ANASHIDA GANI KWANI?

Lo!
nimejaribu kufikiria hii ni sababu ya nini, nimekosa jibu, nimejikuta nacheka sana,
mwenyewe sijui hajijui kama nyumba kumeharibika lo!

Thursday, April 8, 2010

MUME WANGU ANATABIA YAKUTEMBEA NA MAHOUSEGIRL WANGU- JE NIWE NAWAWEKA WAZI JUU YA TABIA YAKE KABLA??

Anayo tabia hiyo, mimi binafsi imeniumieza sana na kunifanya naiona hali ya kawaida tu,

Maana kila anaekuja anaondoka kwa sababu hizo hizo, mwanzoni sikuwa nilikuwa naumisa sana, nikawa naondoka moja kwa moja kwetu, ananifata narudi, kwa ajili ya watoto wangu tu!,

Kuna kipindi alimpa mimba housegirl wangu huyo alikuwa ni watano, nililia sana, maana kuna jirani yangu yeye ni nesi, ndio alieniambia kwamba nimchunguze, mimi kutwa nipo kazini, narudi usiku na watoto wanakuwa wamelala

Yeye huwa anawahi kurudi, basi kumbe ule mchezo wanaufanya kipindi ambacho sipo, basi nilipoanza kumchunguza kweli nikaona maziwa yanamjaa na anapendeza sana, ila kazi anafanya kama kawaida, sema alikuwa ananidharau kupita kiasi, mimi sina tabia ya kuongea ongea, ni mvivu sana kusema sema, lakini ilifika kipindi msichana ndio akawa kama mama,

Siku ya siku ilifika nikambananisha sana, nikiwa na Yule nesi jirani yangu, akampima, akakutwa na mimba, tukaanza kumuuliza ni yanani, alikataa kusema, baada ya kuamua kumfukuza ndio akasema ‘’ ntaenda wapi wakati muhusika ni baba’’ nilitaka kurukwa na akili kabisa

Mume wangu nilipomuuliza mara ya kwanza alikataa, nililia sana, nilipombana sana ndio akakubali na kuniomba msamaha,

Kusema kweli niliamua kurudi kwetu rasmi, nikamuelezea mama hali halisi, mama akaniambia nipumzike nyumbani kwanza, maana matatizo yalikuwa yamefuruliza sana,

Lakini nilipigiwa simu na kuambiwa mwanangu amelazwa, anaumwa sana, maana nikitaka kuondoka na watoto ananikatalia, hivyo niliondoka peke yangu, kwa ajili ya mwanangu nilirudi nikafikia kwa Yule nesi, rafiki yangu, nikawa namuuguza mwanangu, sasa kuna siku alinifata usiku yeye na ndugu zake na kunitaka nirudi nyumbani tukayaongee, niliwaheshimu sana, name nilimpigia simu mama yangu, akaja, tukayaongea huku Yule msichana arudishwe kwao, sasa sielewi, kabla yule msichana hajaondoka, tukiwa katika maandalizi ya kumsafirisha, nahisi kuna mchezo ulifanyika, maana baada ya miezi mitatu, Yule binti mimba ilitoka, akuwa anaumwa, nahisi alikunyw vidonge ili itoke, au mume wangu alimshawishi aitoe, kusema kweli niliamua kumrudisha kwao, mume wangu alisemwa sana na ndugu zake, na akaomba msamaha kutorudia,

Nilipoletewa mwingine tena, akamtongoza, huyu wa sasa alikuwa mwaminifu, akaniambia mama, baba kasema nilale nae atakuwa ananipa mshahara mkubwa na kuwajengea nyumba wazazi wangu, nilimsema sana, nilimuuliza mimi tatizo langu ni nini hadi utake kunifanyia wasichana wangu? Kwanini unanidharirisha hivyo? Hakujibu, isipokuwa alimchukia sana Yule binti, na kuna kipindi nilisafiri kikazi nikakuta amemfukuza nyumbani kamleta mdogo wake,


Sasa nahitaji ushauri wenu, niwe nawaweka wazi wasichana ninaowapata juu ya tabia ya mume wangu? Au nitakuwa namdharirisha? Ila hali hii imenifanya nijishushe thamani sana, kwanini asifanye nje huko? Kuna wazuri wangapi hadi ang’ng’ane na wasichana wangu?





Monday, April 5, 2010

NIMECHANGANYIKIWA- MCHUMBA WANGU ANANING'ANG'ANIA NIMFANYE KINYUME NA MAUMBILE

Nipo Mwanza ni kijana mwenye umri wa miaka 28 nina mchumba ambae yeye ana umri wa miaka 25.uchumba wetu umeanza miaka 3 iliyopita ambapo mpaka sasa hata kwao wananijuwa na nipo katika process za kufunga ndoa na mahari nimetoa, bado ndoa ambayo tulipanga kufanya tarehe 12/06/2010 katika kipindi chote cha uchumba tuliweka ahadi ya kutofanya mapenzi mpaka ndoa.

siku moja mchumba wangu alikuja nilipopanga, kama kawaida mkikaa chemba wawili wa jinsia tofauti, chochote kinaweza tokea. Tulijikuta tunaanza kuchezeana na tukajikuta tumevunja ile ahadi tuliyoweka ila mbaya zaidi mchumba wangu alitaka nimfanye kinyumbe na maumbile " NIMLE TIGO "

hapo ndipo mimi nilipohamaki na kumuliza je mchezo huo ameanza lini na alinijibu kwamba alitaka ajaribuuu kwangu tu.Tabia hiyo ilinichukiza mpaka nikamuwa kuachana nae ila aliniomba msamaha na kuniahahidi kutorudia kunitamkia hilo neno yaani kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Tatizo majuzi tu alikuja home kwangu tulale wote, usiku wakati mimi nimepitiwa na usingizi nilishituka ghafla baada ya kuhisi uume wangu unaguswa guswa, nikaamka, nilimkuta mchumba wangu amejiingiza uume wangu kwenye njia yake haja kubwa kwani mimi nilala chali na yeye ndio aliponikalia kwa matako na kujiingiza uume katika njia yake ya haja kubwa?

Nilishikwa na hasira sana, nikamuuliza kwa hasira, unafanya nini? na yeye alibaki kimya, nilikasirika sana na kuamua kumtimua kwangu usiku na nikamwambia simtaki tena .

Mbaya zaidi huyu binti nishamfanyia mambo kibao kwani nilimkuta hana mbele wala nyuma na mimi ndie niliyemsomesha amefika kidato cha sita na kupata kazi huku akitarajia kuingia chuo mwaka huu na tayari nimetumia ghalama nyingi kwa ajili ya ndoa.je ndugu zangu huyu mtu nimsamehe kama anavyodai yeye, kwamba hatarudia tena, au niendelee na msimamo wangu? Yani nimwache? Kumpenda bado nampenda sana. Nisaidieni ushauri

Friday, April 2, 2010

MUME WANGU NI MCHAFU SANA, ANANITIA HATA KINYAA- NISHAURINI NIFANYE NINI

Nimerudi jamani, mpanaaaaaaaaa, niliwamisi sana, thanks God nimemaliza mitihani yangu salama, nasubiri majibu tu! asante kwa mliokuwa mmenikumbuka, nami niliwakumbuka sana tu! sema mshika mawili moja au yote yaweza mponyoka, ikabidi niache kwanza huku ili nibase kwenye kitu kimoja, now im back to you dears, na nyie miliotuma sms hizi

1. umefulia wewe, huna jipya, story zako tumezichoka, unafikiri kuendesha blog ni kazi ndogo, huwezi
2. huwezi kuendesha blog wewe, unasingizia mitihani, waachie wenyewe, waTZ wote hamjui kuendesha blog, acheni  mnatukera ah!

NAPENDA kuwaambia hivi, nimewasamehe bure kwakuwa hamujui mlitendalo, pia huwa najua kuwa hakuna shamba litakalojaa mazao peke yake, lazima na magugu yawemo, basi watu wa style yenu wala haminipi shida, kuhusu blog za kitz kukukera, kwani umelazimishwa kusoma blog yangu, si usome hizo za nje? blog ziko kibao kwanini msisome hizo?? kuna wanaonufaika kupitia blog yangu, ushauri wa watu umewasaidia, wameweza kupata mwanga wa kutatua matatizo yao, ss kama wewe unaona haukufai, usiwe unaifungua blog yangu, waaachie wale wanaona inawafaa. OVER

(TURUDI KWENYE MKASA WETU WA LEO, NIMEIKUTA MINGI KIMTINDO, LAKINI TUANZE NA HUU KWANZA)]

Violet mambo vipi? mimi nina tatizo moja, na linaninipa shida sana, naomba ushauri wenu,
Nimeolewa, na mwanzoni tulikuwa tunaelewana sana na mume wangu, alikuwa na kazi, lakini baada ya muda akawa hana kazi tena, yeye ni mtu wa kukaa nyumbani tu! anasubiri mwisho wa mwezi nimgawie hela ili akalewee pombe,
shida inakuja hapa, akishalewa tu akirudi hata usiku wa manane anafikia chooni,(chumbani kwangu kuna choo) basi anachokijua yeye ni kuchamba tu! anakunya, mavi anaacha kama yalivyo, hadi ninapofanya usafi asubuhi, ndio nifrash, na hii ni tabia yake, ukimwambia anachofanya ni kosa, anafoka anasema yeye ni kichwa cha familia, hivyo tumsikilize yeye tu!,
shida ingine ni kwamba, yeye ni mtu wakurudi usiku tu, na akirudi ule usiku, anataka nimpe, sasa mimi huwa nasikia kinyaa sana, maana amelewa sana, mwili wote ananuka pombe, halafu anakuwa ananitaka, inanipa wakati mgumu sana, hii tabia ya uchafu wa chooni na hata kusex nae naona kinyaa, pia mume wangu si mtu wa kushaurika, hata umshauri vipi, hashauriki kabisa, sasa violet na wengine, naombeni mniambie nifanyaje mwenzenu, maana loh! inanikera sana mimi.