Hallo
dada violeth pole na kaz ya
kutushauri wanajamii.
Dada violeth mimi ni msichana mwenye
umri wa miaka 28, nina boyfriend ambae ana mtoto mwenye mwaka mmoja na miezi
nane.ila washaachana na huyo dada alozaa nae, mototo aliendelea kuishi na mama
yakekwakuwa ni mdogo.
Sasa juz kati huyo dada kanipigia
simu kupitia namba ya boyfriend wangu na kunieleza kuwa wapo wote moro, later
nikancal huyo boyfriend na kuhoj kulikon akanambia mtoto anaumwa dats why yule
mama mtoto kaenda huko moro .
nlimpigia tena kwa
boyfiend wangu akapokea yule dada na kuniambai yupo kwa boyfriend wangu,
nikamwomba niongee na mhusika akakata na kuniambia nisimsumbue mume wake. Basi
later on nikampigia ma boyfriend na kumwambia yalojiri akanambia yule mwanamke
kamfuata ofisini na mtoto kwa hiyo hakuona busara kumfukuza wakati ana mtoto
wake. bac usiku alipofika bma boyfriend akanipigia simu na tukaongea wote
watatu na boyfriend wangu akaprove mbele yetu wote kwamba hatoweza kuwa na yule
dada na huyo dada akakubaliana na hali halisi na kwa mdomo wake akanambia kweli
huyo kaka ananipenda sana mimi.
Mbaya zaidi Yule dada
kaenda kwa wazazi wa boyfriend wangu Sasa bac Yule dada kapandikiza kule
kijijini na kapandikiza maneno ya uongo kwa mama mkwe kiasi kwamba mama mkwe
leo asubuhi kanipigia kupitia simu ya yule dada kanitukana matusi ya nguoni na
kuniambia hataki kuniona wala kunisikia na huyo dada ananambia angekuwa
hapendwi asingeenda kule kijijini.Ma boyfriend nimemcal ananambia hata yeye
kishagombana na mama yake coz anataka kumchagulia mtu wa kumuoa. Huyo boyfriend
wangu huwa anasema hata asiponioa mimi hataweza kumuoa yule dada coz
hawatowezana.
sasa nifanyaje