Naomba ushauri dada,
Kuna shemeji yangu (x-boyfriend wa rafik yangu) anataka kunioa, waliachana na rafiki yangu miaka sita iliyopita, kipindi wako wapenzi nilijaribu sana kuwapatanisha, lakini rafik yangu alikataa,baada ya muda rafiki yangu aliniambia kuwa ana boyfriend mpya, sasa mazowea ya mimi na shemeji yangu yamebadilika, badala yake ananipenda mimi, na anataka kunioa kutokana na tabia zangu kuwa nzuri, dada Violet, najikuta namimi naanza kumpenda, nilimwambia rafik yangu, kuwa x wako anataka anioe, akasema niwe na amani tu! Yeye hana neno,
Sasa nishauri dada vai, nikubali?? Maana na mie ninataka kuolewa na nimempenda, nina miaka 26, mwili wangu unahitaji kuwa na mtu, na nimempenda kweli huyu aliyekuwa shemeji yangu, nisaidie dada kunishaur