Wapendwa wangu leo nataka tuongee kidogo, pamoja na kuwa mikasa imekuwa miingi sana, nimeona ni vizuri kama tutashauriana pia ili tuone kama inawezekana kufanya hiyo mikasa kwenye ndoa zetu isitokee,
Katika mikasa mingi sana inawahusisha wanandoa, hasa wanawake, mara mume wangu nimemfumania, mara mume wangu kiburi, mara mume wangu mchafu na mengine mengi, lakini je hatuwezi sisi kama kina mama kuangalia ni jinsi gani tunaweza kufanya ili kuzuia? na pale yanapotokea basi iwe imebidi yatokee??? lakini sisi tusiwe chanzo
Tushauriane kwa pamoja, tufanye nini ili tupunguze hii kasi ya machafuko kwa wanandoa, nina amini kabisa kama kila mtu ataplay part yake kama mama mwenye hekima basi 80% ya ndoa zetu zitakuwa zimepona
(i) KUNUNA KUSIPITILEZE.
Kununa imo, lakini sio nongwa jamani, mtu ukinuna basi ndio lo!! Mwezi mzima, sasa tujiulize tunaponunia waume zetu mwezi mzima tunategemea nini??? Kama ana hamu na wewe si atapata nafasi ya kutoka nje? Maana akirudi home anaona kero, mama kanuna, tena wengine bila hata haya wanawambia watoto baba akija msimuamke mkalale, kha! Baba lazima ajiulize hivi kuna haja gani ya kuwahi nyumbani, bora nikae bar niliweeeeeee, matokeo yake anaanza kurudi usiku amechoka baba wa watu, na anarudi tu! kutimiza wajibu
|
Pale inapobidi kukasirika, yes! Show him kwamba hapa umekosea, ili nae ajuwe asikupande kichwani, kama umeamua kumtingisha kwa kununa basi huo mnuno wako uwe na kiasi, sio ndio kila akikusemesha umevuta mdomo, jamani tusipoangalia tutazipoteza ndoa zetu wakati bado tunazitaka,
pia tukumbuke katika yale mambo serios lazima tuwe serios kweli, mfano kuna mmoja alisema ameambiwa aache kazi, dada huyu anaweza kukaa namumewe kwa upole na upendo akamwambia tu! kwanini niache kazi? asikilize hizo sababu, ili nae apate muda wa kujitetea, pengine kazi inamtia kiburi anasahau majukumu yake kama mama ? pengine baba hapati huduma inavyostahili ? pengine housegirl ndio kila kitu ? hadi kusema hivyo lazima kuna reason, tusikimbilie kusema ondoka, au achana nae, we! usipime, mume mtamu jamani, mume anauma asikwambie mtu, ifike kipindi tujichunguze je tuna mapungufu gani sisi kina mama kwa upande wetu, kabla hatujaanza kulaumu waume zetu | |
Kinamama tunapoishi na waume zetu kwenye ndoa, baada ya muda huwa tunajenga mazowea, ambayo sometimes yanakuwa hayajengi bali yanabomoa, mazowea ya aina hii huleta kiburi ambacho kwa namna moja ama nyingine kina madhara makubwa sana, unakuta mwanamke anamdomo mchafu afadhali ya choo, anamjibu mumewe majibu machafu hata mbele za watu /watoto wao, kitu ambacho ni kibaya sana, sababu wale watu wanaowazunguka ninyi wawili watajua tofauti zenu, na mtatiana aibu sana maisha yenu yatakuwa nje, kila mtu atawaona vihoja kuanzia watoto hadi majirani, lo! tubadilike jamani.
Mume anataka kuheshimiwa, ili na watoto wajifunze heshima kupitia kwa mama yao, lakini utakuta mtu akiudhiwa anaropoka hovyo maneno makali ambayo baada ya ugomvi wao kuisha inageuka kuwa aibu kwake,
(ii) (MALIZENI TOFAUTI ZENU CHUMBANI KWENU )
Turejee mafundisho ambayo wengi wetu huwa tunapewa kwenye Kitchen Party zetu, malizeni chumbani migogoro yenu, au hata ukimnunia basi watoto wasijue, au majirani, mwingine akinuna basi ahata kama ni maji ya kuoga haweki, kama ni Chupi ndio hatafua tena, kama ni chakula ndio hatamuandalia tena, jamani jamani, tujitahidi
wanaume ni kama watoto wadogo, utakavyompenda mwanao na kumuweka karibu na wewe ndio atakupenda sana, lakini mtoto ukimfokea fokea tu atakuogopa na kukuchukia, ndio kama waume zetu, tukiwaweka karibu watakuwa marafiki kabisa,
NDOA TAMU jamani asikwambie mtu, tusifikiri ndoa inaweza kuvunjika kwa urahisi. Sometimes mkikosana, jaribu kukumbuka mmetokea wapi?? Kumbuka siku yako ya harusi, kumbuka mapenzi mliyo kuwanayo kipindi kileeee, halafu uya apply kwenye ndoa yako sasa, ndoa ina heshima yake kama mtaheshimiana, na hata kama mtapishana basi mmoja lazima akubali kushuka, ukijishusha mwanamke hutoonekana mjinga kama wengi tunavyofikiria, bali utaonekana mke mwenye busara asiyetaka kuibomoa nyumba yake kwa mikono mikono yake, KUJISHUSHA ni dawa moja nzuri sana, hata kama hujakosea, kwani ukikaa kimya au kama unamueleza ukweli yeye haelewi, no need kupigizana kelele weeeee, NI KUJISHUSHA TU ndio dawa pekeee,
Kwenu wadau wangu, leteni maneno yenu yenye hakma, tusaidianae nami nitayapost faster.
nawapenda sana na ninatamani kama ndoa zetu wooooote zingekuwa za upendo na furaha ili hata vizazi vyetu (watoto wetu) viwe vimerithi tabia njemba toka kwetu