Nisaidieni mwenzenu, niliolewa miaka 5 iliyiopita, ila mama mkwe wangu hakunipenda toka mwanzo, kwakuwa alikuwa ameshamuandalia mwanae mke wa kuoa, lakini mwanae akaforce kunioa mimi kwakuwa tulipenda sana,
Sasa toka nimeolewa, mama hanipendi mimi wala kizazi changu, yani anachukia wanangu kiasi kwamba akifika watoto wananywea kabisa, na hawataki hata kulala nae, nilijaribu sana kujiweka karibu nae, lakini wapi!
Some times huwa anasusa hata kula, anaweza akashinda hata njaa, sasa mimi hali hii sijazowea, natamani kupatana na mkwe wangu kama ambavyo wengine wanapatana nao, lakini huyu wangu aliwahi kunitamkia kabisa kuwa sitakuja kukupenda mpaka nakufa,
Nilimueleza mume wangu, akasema wewe si unajua tatizo mama hakupendi toka mwanzo? ila mimi nakupenda sana, wewe tulia, muache tu! Akae akichoka ataondoka,
sasa nishaurini wapendwa, maisha haya yananipa ugumu sana maana niko nyumbani muda mwingi, nashinda nae, nakosa raha kabisa, mara anitangaze nimemroga mwanae, wakati hata mganga simjui, mara mimi mchawi ndio maana mwanae haoni, wala haelewi, tena maneno haya anatamka kwa housegirl wangu, sasa kweli ni halali hii? na akija anakaa mwezi mzima,
mwenyewe anadai amekuja kupumzika, lakini mbona hapumziki ila analeta matatizo tu! Nifanyaje??? Akifika tu! Amani ndani inatoweka. Sometimes huwa nahisi labda yeye ndio ana mambo ya kishirikina, maana kuna siku mwanae (mr wangu) alimlazimisha kulala na mwanangu wa kike ana umri wa miaka 4,
mtoto usiku alilia sana, nilipoenda kumchukuwa mama akawa mkali, cha ajabu hata kumbembeleza hambembelezi, anasema mmezowea kudekeza watoto, akilia tu mnambeba ukiangali ni usiku wa manane, ilibidi nimchukuwe mtoto, nilivyomfikisha kwangu tu! Akalala, wakati siku zote huwa analala kule chumbani kwao pamoja na housegirl na wala hasumbuhi
Hali hii isikie kwa mwenzio tu! Ikikukuta unaweza kutamani hata kuacha mume ambae unampenda, nishaurini jamani