Friday, April 27, 2012


Hallo
dada violeth pole na kaz ya kutushauri wanajamii.
Dada violeth mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28, nina boyfriend ambae ana mtoto mwenye mwaka mmoja na miezi nane.ila washaachana na huyo dada alozaa nae, mototo aliendelea kuishi na mama yakekwakuwa ni mdogo.

Sasa juz kati huyo dada kanipigia simu kupitia namba ya boyfriend wangu na kunieleza kuwa wapo wote moro, later nikancal huyo boyfriend na kuhoj kulikon akanambia mtoto anaumwa dats why yule mama mtoto kaenda huko moro .
nlimpigia tena kwa boyfiend wangu akapokea yule dada na kuniambai yupo kwa boyfriend wangu, nikamwomba niongee na mhusika akakata na kuniambia nisimsumbue mume wake. Basi later on nikampigia ma boyfriend na kumwambia yalojiri akanambia yule mwanamke kamfuata ofisini na mtoto kwa hiyo hakuona busara kumfukuza wakati ana mtoto wake. bac usiku alipofika bma boyfriend akanipigia simu na tukaongea wote watatu na boyfriend wangu akaprove mbele yetu wote kwamba hatoweza kuwa na yule dada na huyo dada akakubaliana na hali halisi na kwa mdomo wake akanambia kweli huyo kaka ananipenda sana mimi.
Mbaya zaidi Yule dada kaenda kwa wazazi wa boyfriend wangu Sasa bac Yule dada kapandikiza kule kijijini na kapandikiza maneno ya uongo kwa mama mkwe kiasi kwamba mama mkwe leo asubuhi kanipigia kupitia simu ya yule dada kanitukana matusi ya nguoni na kuniambia hataki kuniona wala kunisikia na huyo dada ananambia angekuwa hapendwi asingeenda kule kijijini.Ma boyfriend nimemcal ananambia hata yeye kishagombana na mama yake coz anataka kumchagulia mtu wa kumuoa. Huyo boyfriend wangu huwa anasema hata asiponioa mimi hataweza kumuoa yule dada coz hawatowezana.
sasa nifanyaje



Tuesday, April 24, 2012

POLENI NILIWATUPA WAPENDWA WANGU-

Jamni, mnisamehe mwenzenu, nilikuwa busy kweli, yani kila kona nilikuwa nimebanwa.. but now im back na niko fresh kabisa,...... (mnisamehe bure mlioomba ushauri, sijapost kutokana na ubusy niliokuwa nao,) sijwaignore hata kidogo, sasa naanza kupost ujumbe mmoja baada ya mwingine,

PAMOJA SANA DEARS..........................

Friday, April 6, 2012

KANUMBA HATUNAE TENA HAPA DUNIANI


KANUMBA HATUNAE TENA DUNIANI, NI MMOJA KATI YA WATU WANAOMILIKI BLOGU ZAO WENYEWE,  NA KWA UPANDE WANGU, YEYE NDIE ALIEKUWA WA KWANZA KUWEKA BLOGU YANGU KWENYE BLOG PROFILE YAKE...... NITAMKUMBUKA SANA, MOYO WANGU HAUTAKI KUAMINI KABISA KAMA NI KWELI AMETUACHA...... ALIJIIMBIA NA DR REMMY, KWELI KIFO HAKINA HURUMA JAMANI, HAKIANGALII TAJIRI, MASIKINI, MFUPI, MREFU, WALA MAARUFU....... PUMZIKA KWA AMANI KANUMBA