Friday, April 29, 2011

SEND OFF PARTY OF DIANA

Karibu kwenye maisha ya ndoa Diana, Mungu akutangulie na akutee, akayafanye magumu yote kuwa mepesi kwako, ndoa tamu mwaya,
akiwa bado anaendelea kupambwa








baada ya kupambwa
Hair Style yao


Bi Harusi mtarajiwa alinifurahisha sana, ana pozi za ukweli, haogopi camera hata kidogo


Nikiwa na Mtarajiwa baada ya kumpamba, nimechoka balaaa

Kazi inaendelea



Mama yake akifungwa remba
wewe njoo kama ulivyo, tunabandika na kucha pia
miguu hiyo







KAZINI


 Baada ya kazi (SMILE)
wadada wazuri sana hawa, wamenifurahisha mno, hawana hofu hata kidogo













Wednesday, April 27, 2011

RAFIKI WA MUME WANGU ANANITAKA- NA MKEWE NI RAFIKI YANGU SANA- NIMWAMBIE?

nisaidieni jamani,  kuna baba mmoja ni jirani yetu, ni rafiki sana na mume wangu, wanashirikiana mambo mengi sana, na karibu kila weekend huwa wako pamoja, urafiki wao umefanya mimi na mkewe kuwa marafiki wakubwa, mkewe ananipenda sana,
ninachoshangaa Yule baba anakuja kwa speed ya ajabu, sms kibao, zikiingia tu! Huwa nadelete moja kwa moja, nahofia mume wangu asizione, niliwahi muuliza namba yangu kapata wapi, akasema kachukuwa kwenye simu ya mkewe, nilimfokea  sana, na nilimtishia kuwa nitamwambia mkewe, lakini hakomi  na wala haogopi, kusema kweli hadi sa sa mume wangu sijamwambia, maana mh! Patachimbika,
sasa nahofia siku Yule mama kwa bahat mbaya akipekuwa simu ya mumewe na kukuta sms anazonitumia za mapenzi itakuwaje?? Na nikimwambia kwa sasa ili kujikinga na hatari hiyo atachukuliaje,  najiuliza nimwambie mume wangu au mkewe, au niendelee kuwa kimya,
msaaadaaaa please





Saturday, April 9, 2011

MWILI WANGU UNATOA HARUFU KALI SANA , NINANUKA MASAA YOTE, NAOMBENI USHAURI WENU NITUMIE NINI

Mambo Dada, please usirushe email yangu,
Mimi niko hapa dar, nina miaka 25, tatizo langu ni kwamba ninatoa harufu kali sana, mwili wote, jasho langu lina nunuka sana, kwapa, hata sehemu za siri nanuka pia,  hhali hii inaniumiza sana, inanitesa na kuninyima raha, nakosa kujiamini,

Niliwahi kwenda hospitali, wakafanyia check-up, wakasema nikazane usafi tu, ndio maumbile yangu, lakini sasa mbona hali hiizamani haikuwepo??? Ni miaka mitatu sasa tangu niwe hivi, unakuta hadi nikikaa na watu nahisis wananisema mimi ninavyonuka, kwenye pochi yangu hukos perfume au deodorant za aina 4, kila mara niko washroom najipulizia, hali hii ni ngumu, kwa usafi mimi ni msafi sana, sielezi ni nini hiki,
Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja hapa hapa dar, tulidumu kwenye mahusiano miezi mitatu tu! Yeye alikuwa ni msafi sana, sasa harufu yangu ika wa inamkera, nakumbuka kuna siku aliniambia bwana nakupenda, ila harufu yako mimi mmm, hapana siwezi kuvumilia,  nililia sana, sometimes hat akitandani alikuwa akijifunika shuka lake,  finally tukaja kuachana,  alinikwepasana, nikipiga sim hapokei, mara nikasikia anataka kuoa,

Please naombeni ushauri wenu jamani, nisaidieni mwanamke mwenzenu nakosa raha kabisa, muda mwingine huwa nalia peke yangu, serious naombeni msaada wenu, maana perfume zimenichosha sasa, nimetumia manukato yote, sasa nona yamenizowea harufu iko pale pale, sometimes huwa nahisi nimerogwa, nikaa na watu nahisi wote wananisema mimi, na wengine niliwahi kuwasikia kabisa wakinitaja na jina langu, inaniuma sana, bora ingeonekana ni ugonjwa niutibu kwa gharama yeyote,

Please dada usirushe email yangu.



Wednesday, April 6, 2011

JINSI YA KUNITUMIA MAONI / MKASA WAKO

Wapendwa, mliouliza namna ya kutaka kutuma ujumbe  wenu, email address yangu ikp hapo juu kulia kwenye profile yangu,  ni        violet.gerald@yahoo.com,    nitaipata na nitairusha, ila mtakuwa mmenisaidia sana kama mtaandika kwa kifupi,

Tuesday, April 5, 2011

INAPOBIDI KUJISHUSHA KINA MAMA TUJISHUJE JAMANI- TUACHE VIBURI ILI NDOA ZETU ZIPONE


Wapendwa wangu leo nataka tuongee kidogo, pamoja na kuwa mikasa imekuwa miingi sana, nimeona ni vizuri kama tutashauriana pia ili tuone kama inawezekana kufanya hiyo mikasa kwenye ndoa zetu isitokee,

Katika mikasa mingi sana inawahusisha wanandoa, hasa wanawake,  mara mume wangu nimemfumania, mara mume wangu kiburi, mara mume wangu mchafu na mengine mengi, lakini je hatuwezi sisi kama kina mama kuangalia ni jinsi gani tunaweza kufanya ili kuzuia? na pale yanapotokea basi iwe imebidi yatokee??? lakini sisi tusiwe chanzo

Tushauriane kwa pamoja, tufanye nini ili tupunguze hii kasi ya machafuko kwa wanandoa, nina amini kabisa kama kila mtu ataplay part yake kama mama mwenye hekima basi 80% ya ndoa zetu  zitakuwa zimepona
(i) KUNUNA KUSIPITILEZE.
Kununa imo, lakini sio nongwa jamani, mtu ukinuna basi ndio lo!! Mwezi mzima, sasa tujiulize tunaponunia waume zetu mwezi mzima tunategemea nini??? Kama ana hamu na wewe si atapata nafasi ya kutoka nje? Maana akirudi home anaona kero, mama kanuna, tena wengine bila hata haya wanawambia watoto baba akija msimuamke mkalale, kha! Baba lazima ajiulize hivi kuna haja gani ya kuwahi nyumbani, bora nikae bar niliweeeeeee, matokeo yake anaanza kurudi usiku amechoka baba wa watu,  na anarudi tu! kutimiza wajibu
 
Pale inapobidi kukasirika,  yes! Show him kwamba hapa umekosea, ili nae ajuwe asikupande kichwani,  kama umeamua  kumtingisha kwa kununa basi huo mnuno wako uwe na kiasi, sio ndio kila akikusemesha umevuta mdomo, jamani tusipoangalia  tutazipoteza ndoa zetu wakati bado tunazitaka, 
pia tukumbuke katika yale mambo serios lazima tuwe serios kweli, mfano kuna mmoja alisema ameambiwa aache kazi,  dada huyu anaweza kukaa namumewe kwa upole na upendo akamwambia tu! kwanini niache kazi? asikilize hizo sababu, ili nae apate muda wa kujitetea, pengine kazi inamtia kiburi anasahau majukumu yake kama mama ? pengine baba hapati huduma inavyostahili ? pengine housegirl ndio kila kitu ? hadi kusema hivyo lazima kuna reason, tusikimbilie kusema ondoka, au achana nae,  we! usipime, mume mtamu jamani, mume anauma asikwambie mtu, ifike kipindi tujichunguze je tuna mapungufu gani sisi kina mama kwa upande wetu, kabla hatujaanza kulaumu waume zetu

 Kinamama tunapoishi na waume zetu kwenye ndoa, baada ya muda huwa  tunajenga mazowea, ambayo sometimes yanakuwa hayajengi bali yanabomoa, mazowea ya aina hii huleta kiburi ambacho kwa namna moja ama nyingine kina madhara makubwa sana, unakuta mwanamke anamdomo mchafu afadhali ya choo, anamjibu mumewe majibu machafu hata mbele za watu /watoto wao, kitu ambacho ni kibaya sana, sababu wale watu wanaowazunguka ninyi wawili watajua tofauti zenu, na mtatiana aibu sana maisha yenu yatakuwa nje, kila mtu atawaona vihoja kuanzia watoto hadi majirani, lo! tubadilike jamani.

Mume anataka kuheshimiwa, ili na watoto wajifunze heshima kupitia kwa mama yao, lakini utakuta mtu akiudhiwa anaropoka hovyo maneno makali ambayo baada ya ugomvi wao kuisha inageuka kuwa aibu kwake,

                                  (ii) (MALIZENI TOFAUTI ZENU CHUMBANI KWENU )
Turejee mafundisho ambayo wengi wetu huwa tunapewa kwenye Kitchen Party zetu, malizeni chumbani migogoro yenu, au hata ukimnunia  basi watoto wasijue, au majirani, mwingine akinuna basi ahata kama ni maji ya kuoga haweki, kama ni  Chupi ndio hatafua tena, kama ni chakula ndio hatamuandalia tena, jamani jamani, tujitahidi

wanaume ni kama watoto wadogo, utakavyompenda mwanao na kumuweka karibu na wewe ndio atakupenda sana, lakini mtoto ukimfokea fokea tu atakuogopa na kukuchukia, ndio kama waume zetu, tukiwaweka karibu watakuwa marafiki kabisa,

NDOA TAMU jamani asikwambie mtu, tusifikiri ndoa inaweza kuvunjika kwa urahisi. Sometimes mkikosana, jaribu kukumbuka mmetokea wapi?? Kumbuka siku yako ya harusi, kumbuka mapenzi mliyo kuwanayo kipindi kileeee, halafu uya apply kwenye ndoa yako sasa,  ndoa ina heshima yake kama mtaheshimiana, na hata kama mtapishana basi mmoja lazima akubali kushuka, ukijishusha mwanamke hutoonekana mjinga kama wengi tunavyofikiria, bali utaonekana mke mwenye busara asiyetaka kuibomoa nyumba yake kwa mikono mikono yake, KUJISHUSHA ni dawa moja nzuri sana,  hata kama hujakosea, kwani ukikaa kimya au kama unamueleza ukweli yeye haelewi, no need kupigizana kelele weeeee, NI KUJISHUSHA TU ndio dawa pekeee,

Kwenu wadau wangu, leteni maneno yenu yenye hakma, tusaidianae nami nitayapost faster.
nawapenda sana na ninatamani kama ndoa zetu wooooote zingekuwa za upendo na furaha ili hata vizazi vyetu (watoto wetu) viwe vimerithi tabia njemba toka kwetu